Tandu Anaezungushia Utandu katika Macho yetu.

Tandu Anaezungushia Utandu katika Macho yetu.

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,200
Sina Alama ya siasa ila matendo yangu na fikra zangu zina itikadi ya kisiasa.

Naichukia Siasa mnayoiita Democracy kwa lugha ya kizungu, siasa mnayosema inaleta Amani kumbe ndio chanzo kikubwa cha mauaji Duniani.
cf3857839c578424c7654203dc1ae676.jpg

Siasa au Democracy ni dubwasha lililoletwa na waloezi wa kizungu ili kufitinisha Amani na umoja katika jamii zetu.
47a0fe70dcc7fded672b2b236a8b798c.jpg

Leo hii siasa inataka kufanya Yule aliyopo Chadema kumchukia yule wa ccm ata kama ni Ndugu yake wa Damu eti ni kwa sababu ya tofauti baina ya vyama vyao na sio kitu kingine.

5ea359356f663302f56db994a417ab72.jpg

Tofauti ya kiitikadi inatufanya tuchelewe katika maendeleo ya Nchi yetu,tofauti ya vyama inaturudisha Nyuma Miaka 1000 zaidi .

Sina itikadi ya kijamaa ila ujamaa katika maendeleo ni Afya kuliko Democracy iliyojaa umimi ndani yake.
598ddd59b3dfd0e1780bded866405f96.jpg

Jana iliyotawaliwa na MTEMI AU CHIEF Katika Uongozi inaonekana ilikuwa bora kuliko Leo inayotawaliwa na cheo kilichopewa jina La Uraisi.

Japo hauwezi kushindana na Muda kwa sababu muda ndio ulioleta hayo yote unayoyaona.

Muda ulileta teknolojia hii tunayoitumia leo japo jana haikuepo sasa kwa sababu siku zinaenda basi huwezi kushindana na muda ata kama utakamata wote wanaojaribu kuhoji .


inawezekana labda aliyeanzisha Democracy alikuwa na nia Njema kabisa lakini shida ipo kwa hao wanademokrasia(Wanasiasa)

Sipendi kuichukia siasa lakini wanasiasa wanafanya mpaka naichukia siasa ,
Nikisikia maneno yao Matamu yaliyo na Ushawishi midomoni mwao ni tofauti kabisa na Matendo yao.
46c1580bb84927ae1c1ea2389f39e4c9.jpg

Democracy imekuwa ya kuendeshwa kwa publicity(matukio)na sio maendeleo tena kama ilivyo Aim(dhumuni) ya kuundwa kwake.
3d0e323fa1ea972c44dcd29ec41c7f2f.jpg

Democracy ndio inayoleta maandamano yanayoisha kwa mauaji pande zote za Dunia, Democracy ndio inayoibua makundi ya kigaidi kwa mgongo wa kudai haki kwenye Utawala.

Democracy ndio inayoleta utengano katika Jamii yetu kwa sasa.
65f5fd80ed3412cfcf1902a2ea7e377b.jpg

Kwa nini tusiwe Pamoja na kufanya kila kitu Kwa Umoja badala ya kuendeshwa na Dubwana hili linaloitwa siasa.

Mimi na wewe Ni ndugu kwa nini tugombane kwa sababu ya mihemko ya kisiasa,
Tuwaache wanasiasa wagombane wao kwa wao kwa sababu wanagombania kuyajenga Maisha yao na familia Zao.

0d59e81a557ce26044f1f0215dd05651.jpg

...........!
 
Huko kijijini kwetu kuna watu kutoka ukoo moja walikuwa wanagombea nafasi ya mwenyekiti wa kitongoji, kijana aliyekuwa anagombea kwa cdm akashinda ,aiaee mpaka muda huu naandika hapa ukoo uligawanywa kutokana na siasa. Wale walioshindwa ambao walikuwa Wa ccm wakaleta timbwili la ajabu. Kura za mwaka 2015 zimevunja ukoo. Wengine waliacha na kwenda makanisani kwasababu wachungaji na walimu wa dini walijihusisha too Much na siasa. Kwakweli kuna haja ya kufundisha raia wetu siasa na ukomo wake. Inaniuma sana kuona ndg waliokuwa wanaishi vzr wametengana kutokana na siasa
 
Mleta mada hivi kweli unajua maana ya democracy kweli au umeandika ilimladi tyu?
 
Bro thinking yako iko juu sana ila wajinga watakupinga but umestate vema na ulichomaanisha kiko wazi hata kwenye jamii yetu leo.asante kwa mada na upeo.
 
Back
Top Bottom