A
Anonymous
Guest
Hali si shwari ndani ya Shirika la Hifadhi za Taifa maarufu kama TANAPA, baada ya kubainika kuwepo matumizi mabaya ya mabilioni ya fedha za shirika.
Balaa hilo limegundulika baada ya timu mbili za wakaguzi wa hesabu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya ukaguzi kwa maelekezo ya Waziri wa Wizara hiyo.
Sehemu kubwa ya fedha hizo zinatajwa kuchepushwa kupitia Kampuni tanzu ya TANAPA ijulikanayo kama Tanapa Investment Limited (TIL).
Kuna taarifa za matumizi mabaya ya fedha, ambapo timu ya kwanza ya wakaguzi kutoka Wizara ya Utalii ilibaini kiasi cha Sh Bilioni 14 lakini taarifa za uhakika zinasema Wizara ilituma timu ya pili wiki chache zilizopita, ambapo timu hiyo inatajwa kubaini Sh Bilioni 19.
Taarifa zinasema sehemu kubwa ya fedha hizo za umma, zilienda Kampuni ya Tanapa Investment Limited (TIL), kampuni ambayo Mtendaji Mkuu (CEO) wake ni Dkt. Matolo, akalazimishwa kukabidhi ofisi siku chache zilizopita, pamoja na taarifa kuwa kulikuwa na mkakati wa kumuongezea muda.
Pia, ubadhirifu huo umefanywa chini ya uratibu wa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TANAPA, Kunji ambaye naye amelazimishwa kustaafu ghafla baada ya ukaguzi huo wa wizara.
Kunji alipaswa kustaafu tangu Desemba 2025 lakini aliendelea kuwa ofisini kwa nguvu ya baadhi ya vigogo wizarani ambao nao wanatajwa kuwa wanufaika wa mnyororo wa fedha za ubadhirifu kutoka TANAPA.
Hata hivyo, kulazimishwa kustaafu ghafla kwa vigogo hao wawili wa TANAPA, kumeleta mshtuko kwa baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo, hususan wa Kurugenzi ya Fedha.
Mpaka sasa taarifa za uhakika zinasema kwamba Wahasibu wawili wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi.