GE2025 TAMWA: Siasa safi inawezekana na hoja ndizo zinazojenga taifa lenye maendeleo

GE2025 TAMWA: Siasa safi inawezekana na hoja ndizo zinazojenga taifa lenye maendeleo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimewataka wanasiasa na wadau kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 kuendesha kampeni kwa hoja badala ya matusi na maneno ya chuki, hususan dhidi ya wanawake. Wamesisitiza kuwa "siasa safi inawezekana" na hoja ndizo zinazojenga taifa lenye maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TAMWA, wakieleza kuwa lugha za kubeza na kutweza utu wa wanawake zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wanawake kushiriki kikamilifu kwenye siasa na nafasi za maamuzi.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

TAMWA imeeleza kuwa mazingira haya yanachangia kushindwa kufikia malengo ya ushiriki sawa wa wanawake katika uongozi, jambo linaloathiri pia maendeleo ya jamii kwa ujumla.

 
Back
Top Bottom