Tamko la wanachama wa CUF mkoa wa DSM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la wanachama wa CUF mkoa wa DSM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KING COBRA, Jan 4, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  CUF – CHAMA CHA WANANCHI
  TAMKO LA WANACHAMA WA CUF MKOA WA DAR ES SALAAM JUU HALI YA KISIASA NDANI YA CHAMA.
  Sisi wanachama mkoa wa Dsm,baada ya kuona hali mbaya ya kisiasa ndani ya chama na mwelekeo wa kunyongwa kwa Demokrasia ambapo maamuzi kandamizi yamejitokeza na yanatarijiwa kufanyika katika vikao vinavyoendelea hivi sasa ambavyo mazingira ya kuitishwa kwake vinaashiria dhulma zidi ya haki na utekelezaji wa matakwa ya mtu binafsi, ambapo viongozi wakuu wanaolalamikiwa hawakotayari kukosolewa badalayake wanatumia mamlaka waliyonayo kutoa maamuzi kandamizi.
  Sisi kama wanachama na wapenda haki tungependa HAKI SAWA KWA WOTE ionekane ikitendeka na sio kutajwa kinadharia.​
  Kutokana na hali hiyo tumeona kubainisha madhaifu yaliyopo na madai yetu ya msingi tukitaraji Uziwi na Ukaidi wa Viongozi wetu utakoma hatimae Chama kuleta mvuto mpya:​
  A: MADAI YA MABADILIKO YA KATIBA
  1. Uwepo wa Makamu mwenyekiti bara​
  2. Mwenyekiti Taifa na Makamu wake wawili waingie kwenye Kamati Tendaji Taifa​
  3. Pasiwepo ubaguzi katika uwakilishi wa wajumbe wa Wilaya wanaounda Mkutano Mkuu wa Taifa ambapo ukiondoa wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao ambao Zanzibar pia uzidi, wajumbe 20 wanatoka kila Wila ya Zanzibar wakati Tanzania Bara inatoa mjumbe mmoja tu.​
  4. Pawepo mabadiliko katika uwakilishi wa Wajumbe wa Balaza Kuu ambapo kwa sasa ,Wajumbe 25 wanatoka Katika Wilaya 123 za Bara na Wajumbe 20 Wanatoka katika Wilaya 10 za Zanzibar.Tofauti hii ya uwiyano na ugumu wa kuhudhuria vikaoni wajumbe wanaotoka TZ Bara kutokana ubovu wa miundombinu na umbali wa maeneo wanakotoka unatoa mwanya kwa Katibu mkuu kuitisha vikao kandamizi vyenye kupitisha matakwa binafsi ya Sefu Sharif na mfumo wa upendeleo wa Wapemba​
  5. Mfumo wa uteuzi wa viti maalum ubadilishwe kwa kuwa unaua bara , kutokana na kuzidi kujaza wabuge Zanzibar badala TZ Bara penye hitajio kubwa la wabunge wasaidie kujenga Chama na ikizingatiwa nafasi hizo ni hesabu ya kura tulizopigania watu wa Bara kwani Zanzibar kurazao ni chache.​
  6. Kuendelea kwa Chama kuitumia katiba ya zamani ya toleo la 2003 wakati mkutano mkuu wa taifa wa 2010 LAND MARCK HOTEL ulipitisha katiba iliyo na vipengele vipya haitumiki mpaka hii leo ni kuvunja sheria na ushahidi wa dharau kwa wajumbe wa mkutano mkuu na wanachama matawini.​
  B: UTAWALA NA UTENDAJI
  1. Mwenyekiti Taifa hana ofisi zanzibar wakati katibu Mkuu na makamu Mweyekiti wana ofisi Makao makuu Zanzibar na ofisi kuu bara.​
  2. Asilimia zaidi ya 80 ya ajira za madereva na wafanyakazi wengine wa ofisi kuu bara wanatoka zanzibar wakati hakuna madereva wanaofanya kazi zanzibar wanaotoka Bara.​
  3. Kuna matatizo ya mgawanyo wa raslimali za chama kati ya Bara na Zanzibar,mifano mgao wa Chama wa bajeti ya uchazi mkuu 2010 Zanzibar yenye wilaya 10 katika Mikoa 5 imepewa sh.500 milioni wakati Bara yenye wilaya 123 katika Mikoa 23 imepewa sh.70 milioni tu,fursa za Elimu na Mikopo,magali 5 ya Chama yameuzwa bila ya kufua taratibu za tenda.​
  C: UDHAIFU WA SEFU
  1. Amekua kiongozi hodari wa kufukuza au kusababisha kuhama kwa viongozi hodari wa Tanzania Bara kama:-​
  (a) Mhe. James Mapalala​
  (b) Mhe. Maiko Nyaluba​
  (c) Mhe. Slivesta Kasulumbai​
  (d) Mhe. Geoge Shambwe​
  (e) Mhe. Shaibu Akwilombwe​
  (f) Mhe. Richard Hiza Tambwe​
  (g) Mhe. Wilfred Lwakatare​
  (h) Mhe. Othman Dunga​
  (i) Mhe. Asha Ngende​
  (j) Mhe. Khamisi Katuga​
  (k) Mhe. Ashura Amazi​
  Kwa upande wa Zanzibar ni pamoja na​
  a.Naila Jilawi​
  b.Fatuma Magimbi​
  c.Juma Othuman​
  d.Salumu Msabaha​
  Watu wengi waliofukuzwa au kulazimika kuhama Chama ilitokana na mfumo wenye nguvu usio rasmi ndani ya Chama unaomkinga Maalim Sefu asikosolewe​
  2. Toka kuanzishwa CUF hajafanya ziara au vikao hata mara moja katika mikoa na wilaya nyingi za Tanzania Bora​
  3. Amekuwa bingwa wa kufanya maamuzi makubwa ndani ya Chama yeye binafsi nje ya katiba na utaratibu wa vikao mfano​
  Kumtambua Karume na kukiuka maamuzi ya Baraza kuu la Uongozi Taifa​
  (a).CUF imeambulia mawaziri 7 tu CCM ina mawaziri 9 lakini wakuu wa mikoa, wakuu wilaya na watedaji wote wa serikali ni wa CCM yeye analilridhia.​
  (b). Ilani ya inayo tekelezwa zanzibar ni ya CCM wakati inadaiwa ni serekali ya umoja wa kitaifa​
  (c).Ubaguzi wa upemba ndani ya chama.​
  Nahaya yanayoendelea Chama kumdhibiti Mh.Hamadi Rashidi ni uthibitisho juu ya Maalim Sefu kukiburuza chama anavyotaka ​
  a.Uundwaji wa kamati ya nidhamu na maadili kinyume na katiba ya chama.​
  b.kamati ya utendaji taifa imewajadili watuhumiwa bila kuwapa nafasi ya kujieleza ambapo ni haki yao kwa mujibu katiba​
  c.Kamati tendaji inaongozwa na Maalim Sefu akisaidiwa na wengi wa wajumbe wake ambao wameonyesha chuki za dhahiri na tayari wameshawahukumu watuhumiwa nje ya fikao mfano.E nail ya mwenye kiti wa kamati tendaji taifa sefu kwenda kwa mwenyekiti Prof.Lipumba ilishapanga namna ya kuwafukuza watuhumiwa ya 14.decembr 2012​
  d.Tamko la Naiba katiba mkuu bora julius mtatiro kwa press tarehe 13.12.2011 ofisi kuu buguruni la kuwatangaza watuhumiwa kuwa ni waasi na kuwapa kuwashuhulikia nje ya vikao katiba na taratibu za chama bila kuwapa nafasi ya kujieleza​
  e.Kauli za N.katibu mkuu Zanzibar Ismail Jusa makamu mwenyekiti Machano khamisi Ali katika maeneo mbalimbali na ofisi kuu kuwa tutawa wafukuza kama kama akina Mapalala​
  Hamad mwana wa haramu ni mwana wa haram tu,hata ukimuweka ndani ya chupa atatoa kidole nje ili aone kama!! Ambayo ni kashfa​
  c.Matumizi ya vitisho dhidi ya watuhumiwa yanadhihirisha kuwa wasioweza kutenda haki.​
  d.Kikao kilicho fanyika zanzibar cha kamati Tendaji ya Taifa inadhihirishwa kuwa lengo lake lilikuwa ni ubaguzi ilikikao kikifanyika yeye akawa hayupo basi kikao hicho kitaongozwa na Jusa Ismaili ambaye alisha watukana​
  Blue Guard Bara akiwemo mzee Juma wandwi kwamba wao ni mbwa wanatumiwa na watu wa Zanzibar katika ukumbi wa Diamond Tubilie,mwaka 2009 wakati wa mkutano mkuu​
  Baraza kuu limehitimishwa tarehe 4/01/2012 lina fanyika Zanzibar baada ya kikao cha kamati tendaji taifa tarehe 30 na 31 /12/2011 kutokana na mgawanyiko wa kijiografia wa wajumbe wa Baraza KuuTanzania​
  Baraza na hali ya miundo mbinu, Wajumbe wengi toka Tanzania Bara watashindwa kuhudhuria na hivyo kutoa nafasi ya wajumbe wa Zanzibar wanao muunga mkono sefu kufanya maamuzi kandamizi dhidi ya agenda za Tanzania bora​
  TAMKO LA WANACHAMA.
  Sisi wanachama, tuliokutana​
  Leo tarehe 1. 1. 2012 tuta hamasisha wanachama miko yote na hasa Tanzania Bara kuandamana kuelekea ofisi kuu ya CUF Buguruni kupinga mipango haramu ya kufukuzwa kwa wanachama wenzetu nje ya utaratibu wa kikatiba,​
  Tutachukua hatua za kisheria dhidi ya viongopzi wote wanao kiuka katiba halali ya chama.​
  Tunatoa rai kwa baraza kuu la uongozi Taifa kulimaliza suala hili kwa njia za kusuhulishana ndani ya vikao bila kufukuzana kwa njia zilezile zilizo tumika kukaa na wauji wa CCM serekali yake waliona wanachama wa CUF Bara na visiwani katika maandamano ya januari,26 na 27 na 2001 kuliko hatua wanazo tarajia kuzichukua za kufukuzana.​
  ................................................. …………………………………….
  Mwenyekiti Kamati ya Dharura Katibu Kamati ya Dharura
  Hamdan Ngulangwa (0715 552699) Mpenda I. Mpenda (0715 664913)
  ……………………………………
  Mweka Hazina kamati ya dharura
  Leyla Husein (0719 827047)
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  ................................................. …………………………………….
  Mwenyekiti Kamati ya Dharura Katibu Kamati ya Dharura
  Hamdan Ngulangwa (0715 552699) Mpenda I. Mpenda (0715 664913)
  ……………………………………
  Mweka Hazina kamati ya dharura
  Leyla Husein (0719 827047)
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Du!
  Kwa nje ni Ngangari, lakini kumbe kwa ndani kumechina.
  Bora hawa hawafukuzani!...Taratibu za chama zitumike, na maamuzi yawe ya makubaliano!
   
 4. P

  PACHOTO JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 1,139
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Hao wanatapatapa wote waliofukyuzwa walikuwa wazembe/ vibaraka ndio maana walifukuzwa, mbona hawukata rufaa au kwenda mahakamani kama walionewa?
   
 5. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,694
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Haya kelele za CDM wa kaskazini wanazopiga CUF wakilishikiana na waume zao CCM ziko wapi?
   
 6. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Kaka hao wengi uliowataja hapo walijiondokea wenyewe kwa hiari yao. wala hakuna chama kinachoweza kumzuia mwanachama wake pindi anapochukua maamuzi ya kuhama au kuachana na siasa. suala la kuhama hata vyama vingine lipo wala siyo CUF tu
   
 7. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,630
  Likes Received: 1,388
  Trophy Points: 280
  Ni mwendo wa matamko tu.. sijui tuaelekea wapi kila mtu aanakuja na tamko lake
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  tuzidi kusali ili wazidi kuvuana nguo mchana kweupe
   
 9. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  ubaguzi huo sio wa upemba na ubara pekee, hata dini pia...waliofukuzwa wengi ni dini flani....
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Safi sana naomba hizi vurugu match ziendelee,hapo ndio watakapo jua kipi ni chama cha ukweli.
   
 11. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  {TAMKO LA WANACHAMA.
  "Sisi wanachama, tuliokutana
  Leo tarehe 1. 1. 2012 tuta hamasisha wanachama mikoa yote na hasa Tanzania Bara kuandamana kuelekea ofisi kuu ya CUF Buguruni kupinga mipango haramu ya kufukuzwa kwa wanachama wenzetu nje ya utaratibu wa kikatiba..."}


  Uhalisia uko wapi hapa?! au alitaka kuandika wanachama wote wa Dar?? Hivi wako siriaz kweli hawa?!
  najaribu tu kujiuliza kwa sauti...
   
 12. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Matamko bila Vitendo ni sawa na Bunduki bila Risasi
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Wanaofukuzana ni Chadema na NCCR Mageuzi si ndio mkuu?
   
 14. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha tamko wala nini,kuna watu wanatafuta nafasi ya kujipenyeza kwenye mgogoro ambao upo na unaendelea kwa sasa CUF,tamko hili linaonekana kabisa halina ushirikishwaji wa wengi na ni kikundi tu cha watu wameamua kukaa na kuja na jambo kama hili.
  Tusubiri na tuone watafanya nini CUF wakifukuzana.
   
 15. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tahadhari na dhambi ya ubaguzi, lengo la chama cha siasa ni umoja ile kufikia malengo na sio kupigania shibe ya mtu mmoja.

  Na ndivyo inavyojaribu kuonekana hapa kwamba akishiba mtu mmoja wengine watajiju! hili haliwezi kuwa lengo la chama cha siasa.

  Ni vyema katiba ya chama ifuatwe ili haki iweze kutendeka, maamuzi ya mtu mmoja kuitwa ndio maamuzi ya chama ni kudanganyana na pia ni kuua demokrasia ya kweli katika chama. Kama chama kinakuwa na viongozi ambao hata wakikosea hakuna mamlaka ya kikatiba ya kuhoji kulikoni, hakuna chama hapo hicho ni kijiwe cha kahawa kwa maana kwamba anayelipa kahawa ndiye anayesikilizwa kwanza!
   
 16. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  CUF members,kuna room kwenye vyama vingine kama NCCR...
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tamko limejaa makosa mengi sana na nadhani is time kwenda shule na kuachana mambo ya madrasa yet unataka uongozi wa Umma .
   
 18. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Itungwe sheria kuwa mwanachama akihama/ kufukuzwa chama asijiunge na chama kingine kwa miaka kumi. Na eleze kwanini hakuwa amejiunga na chama hicho kama aliona kina sera nzuri. Pili aeleze kwanini sera za chama kipya zimeanza kumvutia baaada ya kufukuzwa. Pia achunguzwe kama kwa miaka mitano nyuma hakuwahi kukikashfu chama anachotaka kuamia. Hatutaki unafiki na kukosa nidhamu. Hapo tutaiona nidhamu.
   
 19. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,399
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Wamechelewa!!!!
   
 20. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama haya wayasemayo ni kweli walisubiri nini kuyasema mpaka kikao cha kumjadili Rashid? Hawa nao ni hawaelewwki, WATETEZI VIGEUGEU, WANA SIASA VIGEUGEU, WANATUGEUKIA.
   
Loading...