Tamko la Wabunge wa Jiji la DSM Kuhusu Kashfa ya Shirika la UDA

Pongezi kwa wabunge wa Dar es Salaam, wabunge wengine mikoani wanatakiwa kuiga huu mfano linapotea jambo la maslahi ya Umma mnaweka pembeni ukelekweta wa vyama
 
it is a good step foward, hongera saana wabunge wa DAR mkimaliza hilo nini kinafata?
 
Bado ninauliza hivi ofisi ya waziri mkuu ilikuwa haijui jambo hili kweli!!
Kwanini isundwe kamati ya bunge kuchunguza, na kazi hiyo anapewa Hosea wa PCCB aliyeshindwa madudu ya Richmond!
Kwanini taairfa itolewe kwenye kamati ya miundo mbinu na si bungeni
Uchunguzi utaanza na kumalizika lini, isije ikawa utaanza Jan 2012 na kumalizika Dec 2015.
Kwanini viongozi wa jiji na mwenyekiti wa bodi ya UDA wanakiburi cha kukiuka maagizo ya ofisi ya PM, sijui ni kwa miujiza gani ofisi ya waziri mkuu haiujui au haihusiki!!!!!!!

Ninachowapongeza wabunge ni kukaa pamoja japo kuandika kitu lakini bila hatua zaidi, haya maandiko yenu yatabaki katika kumbu kumbu.
Tumeshaona tume na tume, uchunguzi na uchunguzi hakuna taarifa hata moja inayotoka wala watu kuchukuliwa hatua.

Sitawaelewa nitakaposikia mkisema tulitoa tamko na mengine ni ya serikali.
Hivyo vyombo vya dola mnavyopongeza sina imani navyo kabisa. Hivyo ni kwa ajili ya vibaka si Mafisadi wanaoogopwa na Mh Waziri mkuu Pinda(alitamka bungeni).

Ngoja tuone igizo hili litaishaje!
 
Kama huu ndiyo usanii basi uendelee tu, kwani ndani ya usanii kama huu sisis wananchi tunapata uelewa wa mambo ya sirini.
 

Kaka Maggid, hapo kwenye red,hiyo kalenda ndo mnayotumia huko Msamvu?
 

Conflict of interest, huwezi kuwa mwenyekiti wa bodi halafu ukajipa kazi ya consultancy. Mwenyekiti wa bodi akishakuwa mmoja wa wazabuni, hivi kweli UDA wanaweza kumnyima kazi hata kama hakushinda? Jamani tuwe na uzalendo, hata kama ana kampuni hiyo ya ushauri akafanyie pengine sio UDA ambapo yeye ni mwenyekiti wa bodi.
 
Mokongoro ni mjomba wake masaburi na ni wabia wa chuo cha ugavi kule chanika
 

Wabunge wa Dar kwa pamoja walau wameanza kufanya kazi kwa niaaba ya wananchi;

Waheshimiwa Myika na Mdee nafikiri mmo humu JF, naomba muwahurumie wana dar hasa wafanyakazi na wanafunzi, hili swala la usafiri dar ni issue inayoweza kutatulika tena mapema sana, hebu himizeni sio kila siku tupo kwenye mpango! ooo Mchakato mpaka lini!? wananchi wanataka kutatuliwa hizi kero zao on time, tunaomba muwabane wahusika waseme hadi sasa nini kimefanyika na ni lini usafiri dar utakuwa umeimarika, watoto wanaamka saa kumi na moja asubuhi! unategemea watasoma shule hawa?, watakua Vizuri hawa? hawajamaa wa waserikalini hawapati hizi taabu kwa sababu wana magari ya serikali; la kumpeleka baba kazini, la watoto shule na la mama Saloon, so hawajui balaa la daladala, hili ni tatizo kubwa sana tena huwa nahurumia sana watu mitaa ya Posta unakuta mtu anakimbilia daladala kama hana akili na jamaa wa serikali wapo kwenye V8 wanakula viyoyozi na sisi wengine wenye vimikweche tunaingia ghara za mafuta bila sababu kwa kuwa ukikiacha home utafika office shati lako jeupe lina tope, kwa nini watu wajazane kwenye daladala kama wanyama.

please wabunge unganeni kwenye kero za msingi za dar sio kuuza sura tu!, angalia masaki hakuna maji Chole road why? kisa miradi ya wakubwa ya malori ya maji!? amkeni tupendezeshe miji yetu uwezo tunao na pesa TZ ipo.

halmashauri zinashindwa hata kutengeneza mazingira safi! e.g weka vitofali kuzuia vumbi, tope nk, kuweni wabunifu jamani sio kunenepesha matumbo tu.
 
Tunashukuru kwa wakati kama huu wabunge wote kutoka vyama tofauti kushikamana kwa pamoja kwa maslahi ya Taifa hili TAJIRI,tuzidi kupamba na kushikamana kwa maslahi ya Taifa hili
 

Makongoro si Mbunge wa Dar es Salaam mbona simuoni kwenye tamko?
 
Mokongoro ni mjomba wake masaburi na ni wabia wa chuo cha ugavi kule chanika

Mkuu si angetoa tu tamko hata kama Masburi ni mjomba wake. Angedeclare tu kwamba Masaburi ni mJomba lakini alichokifanya ni batili. Duh nimesoma Gazeti la Majira Ndg Simba akijitetea na pia nimesoma Tamko la Kisena kwenye Gazeti la Mwananchi nimebaki nimeduwaa!! Hivi Nchi hii inaenda wapi sasa kila mtu anapora kilichokaribu naye. Kila kukicha huyu kapora hiki huyo kapora kile ili mradi tu nchi inakwenda shagilabagala!! MZAWA Simba anasema ati kalipwa kwa kutoa Consultancy kwa Simon Group na hivyo kulipwa million 300!! Simon Group ndio wananunua UDA wakati Simba ni Chairpeson of the Board of Directors; bonge la conflict of interest!! Sitaki kuamini kuwa Simba; msomi aliyebobea, mwanataaluma na mtumishi wa siku nyingi wa mashirika ya kimataifa hajui kwamba hapo kulikuwa na Bonge la conflict of interest. Nimeamini kwamba fedha mwanaharamu na inaweza ikakufanya ifanye chochote ambacho hukiamini!! Idd Simba a.k.a Mzawa amekula vya wazawa!!!
 

Mkuu hata mtoto mdogo asingekubali kuishauri kampuni ambayo inataka kununua shirika ambalo wewe ni kiongozi. Hapa kuna inside dealing ambayo inakatazwa!
 
Je serikali itawashitaki kweli?siku kumi za jairo bado hazijatimia?dpp ameshapata jarada la chenge ili ashitakiwe?au ndo funika kombe mwanaharamu apite?tusubili tuone japo kwa mfano nini kitatokea ingawa bado ninawasiwasi na hawa magamba.
 
Safi sana wabunge wa Dar. Utaifa kwanza. (Sijui kama yule dada yetu Faizafoxy na kaka yake Ms watachangia hii mada...!)
 
Kumbe kuna issues wapinzani na chama tawala mnaweza kukaa na kukubaliana? Safi

Ukisikia uwajibikaji wa namna hii kweli wabunge wengi mtaendelea kulinda hadhi kwenye majimbo yenu, Muungano na tamko la pamoja na ingelikuwa hivyo hivyo kwa mikoa mingine tunge iweka serikali yetu kati majibu ya kipuuzi na kutufanya sie ni watoto yasingelikuwepo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…