Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,890
- 141,552
I'm the most open minded person... natofautiana na wewe mara nyingi unapozungumze with haste generalizations and condemnations. Huna balance unapokosoa kitu kwako kitu ni either x or z hakuna abcde... Na hata hicho ulichokisema tumeshanyoshea kidole mara kadhaa hapo nyuma ndiyo maana nilitaka nisikie Waziri Mkuu amesema nini kuliko kusoma kwenye magazeti tu watu wakaja kunilaani kuwa nataka ninunue habari ili iwe nini.
Huo hapo ndipo mfano ninaouzungumzia... tayari press imekuwa "yenu".. sasa kama ni yetu kwanini usiiache tu?
umeisoma ile taarifa mwanzoni na mwishoni nimeandika nini. Of course not.
kaisome tena...
Naamini itabidi ifike kipindi tutofautishe "symphathy na sheria" tunaendekeza sana sentiments katika swala ambalo liko straight forward.
Wengi wetu humu tunamtetea Pinda kwa sababu "kaomba msamaha". Lakini jamani tunaelewa mtu kama Pinda nafasi yake katika jamii yetu? Tunajua kwamba Pinda ni Waziri Mkuu? Tunajua kwamba ni huyu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi yetu? unajua kwamba Katiba inawalinda wahalifu na wasio waharifu? What message are you sending unaposema kwamba watu wauawe?
Lets go back, tunaposema utawala wa sheria tunakuwa na maana gani? au ni yale yale..tunakuwa na double standards. Kwamba fulani kaomba msamaha kwa hiyo aachwe apumzike? By the way..wengi mnalichukulia hili kama utani..lakini Prime Minister kusimama jukwaani na kusema fulani akiua auawe..somthing is wrong . very wrong. Implication yake ni kubwa. Jiulize watu watamfikiriaje akiongelea kitu kama Human Rights au Death Penalty? kesho Pinda akienda Umoja wa mataifa atasimama kwenye podium kulaani matumi ya nguvu dhidi ya watu fulani? media za zinaweka kumbukumbu. I mean..implications ya kauli kama za akina Pinda ni kubwa mno. Hatuwezi kukaa na kusema kwamba jamaa "aachwe kwa sababu kaomba msamaha"
Accountability demands consequences. Leo Lowassa, Yona, Mramba et al..wakisema tunaomba msamaha..tulifanya makosa..tutawasamehe? au Pinda anasamehewa kwa sababu alitoa kauli tuu ambayo "haidhuru"
Personally I respect and admire Pinda.
Lakini watanzania wenzangu tuache double standards. When we see the Prime Minister advocating for the breach of the rule of law..na sisi tunaingia mkenge na kuanza kumtetea..nadhani tunaset precedent mbaya sana.
All in all, this should be a lesson kwa wengi wetu. Tunapolilia utawala wa sheria au Rule of law..ni mambo kama haya! Sheria na huruma havina ukoo. Personally I cant take him serious when he is advocating the breach of our sacred document! Katiba.
I can ASSURE YOU, hii ingekuwa huko Europe au kwingineko..Pinda wouldnt have gone away with it!
Anyway tuliache. Ila tujifunze kitu katika hili swala zima.
Masanja,
Ahaaa! Sasa nimesikiliza hiyo sijui hotuba au maelezo yake bungeni. Kwa jinsi watu mnavyoiweka hapa ni kama vile Pinda alikuwa analia (bawling) uncontrollably. Hapana, Pinda alikuwa choked up. Kuna tofauti kubwa sana kati ya ku choke up na ku bawl.
Sasa watu wengine hapa mnafanya ionekane kama vile Pinda alibubujikwa na machozi. Hapana bana. Kwangu kulia sio hoja hata kidogo. Hoja na kilicho cha msingi hapa ni hatua gani za dharura zilizochukuliwa kukomesha unyama huu.
Mmekuwa so caught na huko so called kulia hadi mmesahau yaliyo ya muhimu. Kwa mfano, ni waziri yupi hasa anayehusika moja kwa moja na usalama wa wananchi? Yeye katoa tamko gani?
Kosa la Pinda sio kuzidiwa na hisia bungeni. Kosa lake ni kauli alizotoa. Na kama bado hajazikana (kuzifuta hawezi kwa sababu keshazitoa) na kuomba radhi, basi hapo mimi nalia naye mpaka kieleweke.
]................Majanga yanayowapata Maalbino nchini yameishtua dunia na matamshi ya awali ya Waziri Mkuu yamezidi kuchochea moto na kuionyesha hiyo dunia kuwa nchini Tanzania hakuna utawala wa sheria.[/SIZE]
Kama kuuwawa kwa Maalbino kumetuaibisha kama taifa, matamshi ya Pinda yameshindilia msumari hiyo aibu................Tungekuwa na utawala wa sheria na uwajibikaji, hivi sasa nafasi ya Waziri Mkuu ingekuwa wazi.[/quote]
........Mag3..
kula tano mkuu.........halafu bado kuna watu hawaoni/kufikiria ujumbe kama huo hapo........long way to go...dah
................Ni mara ngapi tumesikia Rais Bush akisema Osama akipatikana auawe!.. Je, hii ina Bush alikuwa akivunja sheria kwa kutoa maelekezo ya kisiasa pale sheria inapotakiwa ama alikuwa akizungumzia adhabu ya juu kutolewa kwa mtu kama huyu............
Ogah,
Nakusoma vizuri sana isipokuwa bado kidogo hujanipata.. yes kuna political correctness ktk kutoa habari ambayo ni tangulizi ya maamuzi ya korti. Hata Saadam Hussein alipokuwa akitafutwa kuna wale waliosema ata face justice na wengine wakasema atauawa wakiwa na maana in a process ya hiyo hiyo justice haina maana kuwa atakapo patikana tu auawe.. Lakini hizi zote ni lugha tu, ukweli unabakia kwamba wote wanataka mtu huyo anyongwe!..
Hata huyo Bush unayemsema leo alifuata sheria pamoja na kwamba alichosema ni kuuawa kwa Saadam.. nina hakika ndivyo alivyo mean hata kwa Osama. hivyo message zote hizi zinahusu ku face justice ila inategemea na wakati aki present hiyo message..
Kwa hiyo mkuu wangu binafsi sina matatizo ya message kama hizi zinazotangulia sheria kwa sababu haina maana zipo nje ya sheria isipokuwa ni pendekezo la adhabu ya juu kwa wahusika hata kama mahakama ipo!..
Pinda kachemsha kweli lakini tuwe makini zaidi ktk kutafuna habari kama hii kwa sababu navyofahamu mimi kiongozi yeyote anaweza kutanguliza kauli inyohusiana na sheria isipokuwa kama tungekuwa hatuna hukumu ya kuua hapo ndio ingekuwa zengwe la kufungia kengele..
Trust me hata mimi hapa nasema hao walioua Albino sioni hukumu ya haki isipokuwa nao wahukumiwe kifo -IF found guilty!
Now, ikiwa nimetoka nje ya sheria kwa kutoa maoni kama hayo then nadhani sheria yetu ingetakiwa isiweke hukumu zake wazi yaani wanasheria na mahakimu tu ndio wajue nini hukumu ya kosa fulani..
Niliwahi kusema huko nyuma, serikali yetu inaendeshwa kijanjajanja. JK na timu yake wote longolongo kibao. Huwezi kutueleza kuwa Tanzania ni nchi inayoendeshwa na utawala wa sheria. Utawala wa sheria maana yake NONE IS ABOVE THE LAW.Suppose kama angekuwa ni Dk. Slaa katoa maneo yale, mmmh sijui ingekuwaje. Yaani wangetumia nafasi hiyo kummaliza na kumuondoa katika ramani ya siasa Tanzania. Yangeletwa mashitaka mbele ya jaji kuhusu uvunjaji wa AMANI, angepelekwa Ukonga kunyea ndoo. Serikali haitakiwi kuwa biased, kama Pinda kachemka na kuchochea uvunjaji wa AMANI, then awajibike au awajibishwe na si kuleta mchezo wa kuigiza wa kutoa machozi bungeni watu wajue kuwa una uchungu na maalbino.
Kama kweli ana uchungu na Maalbino kwa nini asimkalie shingoni Waziri masha na IGP????????? Watu wamekalia deal ya ID lakini wanasahau binadamu wengine wanaendelea kuuawa kwa sababu ya uzembe katika suala la ulinzi. Serikali iko kimbelembele kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani lakini viongozi hawako tayari kutoa maagizo na ufuatiliaji mkali kuhusu vifo vya albino.
Nakumbuka kipindi fulani kiongozi wa juu wa serikali aliwahi kuoa maagizo kuwa mtu akifa kwa njaa basi Mkuu wa wilaya ajiuzuru. Ok, kwa nini order kama hii isitolewe kwa wakuu wa wilaya na OCDs kuhusu ALBINOs????
Pinda, onyesha ukomavu katika uwajibikaji na watu wataendelea kukuheshimu.
Mkuu Obama hakuja kupinga usemi wa Bush wala hakuwahi kusema ule ni Ujinga... hakuna kiongozi hata mmoja aliyempinga Bush katika usemi ule...na hakika record itaonyesha hata yeye Obama alisema akisikia Osama yuko mahala fulani ndani ya Pakistan ataruhusu majeshi yake akiwa kama C in C, kumuua bila idhini ya Pakistan ikiwa wao watashindwa...We will defeat Al Qaeda ndio usemi wake mkubwa na mwenye kuelewa maana anajua kinafuata kipi..Lakini hapa tunamuongelea Waziri Mkuu! Na kama Ogah alivyosema huwezi halalisha ujinga wa Bush kwa ku-compare madhambi ya Pinda..Ndo maana leo Obama anabadilisha kila kitu cha Bush..kwa sababu hata wanaomsupport Bush..wana-admit kwamba jamaa alichemka.
Mkuu Obama hakuja kupinga usemi wa Bush wala hakuwahi kusema ule ni Ujinga... hakuna kiongozi hata mmoja aliyempinga Bush katika usemi ule...na hakika record itaonyesha hata yeye Obama alisema akisikia Osama yuko mahala fulani ndani ya Pakistan ataruhusu majeshi yake akiwa kama C in C, kumuua bila idhini ya Pakistan ikiwa wao watashindwa...We will defeat Al Qaeda ndio usemi wake mkubwa na mwenye kuelewa maana anajua kinafuata kipi..
Hayo ni ya Marekani, lakini my point inapinga jinsi sisi wananchi tunavyochukua maamuzi yetu haraka bila kufikiria na binafsi hata tamko letu AJIUZURU linatangulia sheria hivyo naweza kusema tumekosea..
Nakumbuka Mwinyi kuna wakati aliwahi kusema kule Songea akiwahamasisha wananchi walime Korosho alisema hivi:- Wananchi kazaneni ktk Mikorosho na watu wakaichukulia out of context..Unajua tena yaliyofuata..
Mkuu nakubali Pinda kashemsha isipokuwa najaribu kuwafahamisha kwamba hii ni cheap shot kisiasa na hata ukitazama vibaka wanaokamatwa na kuuawa nchini hakuna kiongozxi hata mmoja aliyesimama na kusema wauliwe, sisi wananchi wenyewe tunachukua sheria mkononi na hii inaendelea hadi kesho.. Double standard ni pale tunapoweza kuua vibaka kwa kuwapiga mawe lakini tunapinga kauli tu ya Kiongozi ambaye mimi binafsi nimemsoma alikuwa akimaanisha kitu gani, besides kama sikosei kawaomba samahani ikiwa amewapotosha...
Tukirudi ktk issues nyinginezo tumezungumza humu kuhusu Lowassa, Mkapa na wengine wafilisiwe, waende jela na kadhalika haya yote ni maneno yanayotangulia sheria lakini haina maana tuna maanisha wafungwe na kufilisiwa bila sheria..Mkapa aliwahi kusema kuhusu Machafuko ya Zanzibar kutumia nguvu ya Dola na akatumia kweli lakini sikusikia Mtanzania (hasa Wabara) wakisimama kuom,ba ajiuzuru, Wauaji ya Mwembechai, Mrema na majambazi haya yote ni matendo machafu ambayo hayakufuata sheria tulishindwa kuyakemea badala yake tuliwasifia viongozi hawa, leo Pinda kasema tu wanaoua Zeruzeru wauawe imekuwa kosa kubwa ambalo halina hata msamaha kwetu..
Double standard ni sisi wananchi mkuu wangu, Pinda kasema alosema na hakuna mtu hata mmoja ambaye kisha chukua hatua ya kuua watu ovyo, ikiwa na maana wananchi wanaelewa kuwa Mh. Waziri mkuu hakuwa akizungumza na wananchi direct kuwaambia wachukue sheria mikononi mwao..lakini on the other hand sisi tunaendelea kuua vibaka bila hata kuuliza sheria inasema vipi na hakuna heading hata ktk gazeti moja likiwaomba wananchi kuacha vitendo hivyo!.. Kesho ukienda Kariakoo na ukaitiwa Mwizi watakuua...Hii law imepasishwa na wananchi na sisi tumeshindwa kuwakemea viongozi wetu kuhakikisha vitendo hivi havifanyiki..
Nazidi kusema ni kawaida ya binadamu kutanguliza hukumu inayotakiwa kulipa maovu ya mhusika hata kama wanafahamu ni lazima mhusika atinge Kisutu kwanza..Kuna maneno mengi yamesemwa na kina Mbowe kuhusiana na Utawala huu, kama vile kuingia msituni, afadhali ya Mkoloni na hata Dr.Slaa ambaye kama nakumbuka vizuri alisema kipigo alichopata Mtikila huko Tarime ni size yake..Haya ni maneno ambayo yanatangulia sheria haina maana kabisa kuwa kiongozi huku anasisitiza watu waendelee kufanya madhambi hayo...
Pinda alichemsha?.. Ohhh Yes, lakini kosa lake ni swala la kufahamu tu kuwa hakuwa na maana zaidi ya wito kwa sheria kutumika kutoa adhabu kali...