Tamko la Chama Cha Walimu(CWT)

Olesambai

Member
Joined
Jul 31, 2012
Posts
39
Reaction score
4
Kufuatia hukumu iliyotolewa hapo jana na mahakama ya kazi ya kuwataka walimu kurejea kazini na kuwaamuru viongozi wa CWT kutangazia Umma kuwa mgomo umekwisha, Chama kimesema kitatoa tamko leo saa 4:00 asubuhi. Tamko hilo litaeleza kama chama kimeridhika na hukumu au wanakata rufaa. Taarifa hiyo haijaweka wazi kama walimu warejee kazini ama laa. Mtoa taarifa amewataka walimu kufuatilia vyombo vya habari saa 4 asubuhi. Nawaomba wadau mtakaopa updates mtuwekee humu. Karibuni.

=============
UPDATE
=============
 
Haya,,,,ila mgomo baridi si unaruhusiwa kama wa mhimbili?????
 
Huhitaji kuwa Sheikh Yahaya kulitambua tamko litakalotolewa. Waalimu wataagizwa warudi kazini wakati chama kinaendelea na taratibu za rufaa!
 
Watakata rufaa na watarudi kazini ila wtajua wao nini cha kufanya......
 
Haya,,,,ila mgomo baridi si unaruhusiwa kama wa mhimbili?????
Yeah, sasa walimu watajifunza kusaini mahudhurio na kujisomea magazeti au kula story chini ya mti wakipunga upepo mpaka kitakapoeleweka. Jana nimesikia walimu hawajawekewa pesa kwenye account zao kwa makusudi, ni kweli?
 
Huhitaji kuwa Sheikh Yahaya kulitambua tamko litakalotolewa. Waalimu wataagizwa warudi kazini wakati chama kinaendelea na taratibu za rufaa!

Hapo ndipo ninapoona walimu au viongozi wao hamnazo endapo watatepeta.
 
Hapo ndipo ninapoona walimu au viongozi wao hamnazo endapo watatepeta.

Nilazima warudi kazini kwanza ili kutii amri ya mahakama. Swala la rufaa ni kutetea haki yao maana hawajaridhika na hukumu. Mbona ipo wazi sana na wala sio kwamba wana surrender!?
 
mkoba ni mnafiki mno.
Walimu wanatumika kuzima madai ya madaktari
 
Yeah, sasa walimu watajifunza kusaini mahudhurio na kujisomea magazeti au kula story chini ya mti wakipunga upepo mpaka kitakapoeleweka. Jana nimesikia walimu hawajawekewa pesa kwenye account zao kwa makusudi, ni kweli?

hapana wamewekewa,labda baadhi ya halmashauri,ila most of my frends r tichaz tangu juzi wanakenua akaunt zao zimevibrate,,,,usipowawekea je wale wanaofanya kazi watajisikiaje?????
 
natamani wasiache kugoma ili nione plan B ya serikali
Sembuli, plan B ni ipi? Kufukuza wote na kuandaa Bilion mbili za kuwalipa wachina waje kufundisha? Maana najua hiyo pesa zinapatikana kirahisi serikalini kuwalingishia wananchi.
 
kiwango cha taaluma kwenye mitihani ijayo ya taifa inaweza kushuka kwa % kubwa
 
kiwango cha taaluma kwenye mitihani ijayo ya taifa inaweza kushuka kwa % kubwa

Huko ndiko tuendako, inatisha sana taifa hili litakuwa la wajinga na vilaza wakubwa siku za uson.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…