enzi za ujinga nilidhani dereva akikupigia honi barabarani na wewe usisikie au ukachelewa kumpisha anaruhusiwa kukugonga na gari lake....
nilipokuwa napata uelewa na baadaye kwenda shule ya udereva nikajua kuwa kumbe ni jukumu la dereva kuhahakisha hamgongi mtu hata kama amekataa kutoka barabarani....!!
Mwaka 2001 wakati wa mauaji ya Pemba tuliambiwa na wauaji wa pemba kuwa CUF waliagiza contena la visu kwa ajili ya upambana na polisi na hawakuishia hapo ila walienda mbali na kusema waandamanaji wa CUF walitaka kuteka ghala la silaha ndo wakawaua, nilikuwa mmoja wa wajinga waliowaamini polisi(Ngunguri) hao. Namshukuru Mungu aliyenipa upeo baadaye nikajua kuwa ni rahisi sana kudanganywa na polisi + serikali kuliko mtu mwingine yeyote kwa sababu wajinga wengi wanawaamini sana kuliko mama na baba zao.
Kule Arusha interest ya Waandamanaji ilikuwa kushinikiza kuachiwa kwa Mbunge wao na Mwenyekiti wa Chadema taifa ila polisi wanasema walitaka kuchoma moto kituo, mwenye akili hata kidogo tu kiasi cha mboga anajiuliza hivi wangechoma moto kituo si hata mpendwa wao mbunge angeungua na mwenyekiti wao pia!!??? unaona kabisa ni uongo uliokubuhu. Shame on them.
Kuna kijana alipigwa risasi akiwa amelala chali anaomba wamsamehe mbele ya masista kanisani ila alilambwa risasi ya mguu na kuachwa hapo mpaka Padre alipotoka na kumpigia askari anayemjua ili waje kumchukua ndipo wakaja baada ya dk zaidi ya 30. Mpumbavu bado anaona walistahili watu hawa kupigwa risasi eti polisi wanalinda ghala la silaha lisivamiwe....Siwalaumu sana labda muda wenu wa kuyajua haya bado haujafika ila kama mnatumikia mafisadi ili mpate makombo wanayosaza hakika mnachuma dhambi mbaya sana.
serikali ina vyombo vya habari radio,tv,magazeti,mazungumzo baada ya habari na hata vyombo vya vibaraka wao vinawatukana wananchi baada ya kuwaua! eti wapumbavu wanashangilia na kucheka !!?? Tunisia ilikuwa na utulivu wa kulazimisha huku wakiminya demokrasia na kudhani watu hawatakuja kubadilika ila ilifikia mwisho. Tanzania iko very close to that TAKE CARE YOU I.D.I.O.T.S!!!