Tamko la Benki kuu ya Tanzania

Tamko la Benki kuu ya Tanzania

SIMBA mtoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
204
Reaction score
100
Ndulu-2.jpg


The Bank of Tanzania (BOT) governor, Benno Ndulu.​


THE government declared illegal the growing trend of pricing goods and services for Tanzanians in US dollars, saying stern measures would be taken against those who continue with such practices.

Tamko hili lilitolewa na waziri wa fedha Ms Zakia Meghji katika kikao cha budget mwaka 2007. Leo hii imepita miaka 7 tangu serikali itoe tamko hili la kisiasa, mamlaka inayositahili kufuatilia wamejifungia kwenye ofisi zao za Mirambo bila kuchukua hatua zozote. Tangu taifa la Marekani kuruhusiwa sarafu yao iwe ndiyo fedha halali kwa malipo hapa nchini fedha yetu imekuwa ikiyumba sana na thamani yake inaporomoka kuliko maelezo.

Tunamtaka Benno Ndulu achukue hatua za haraka za kukamata na kushitaki mahakamani taasisi, na wafanyabiashara wote wanaotoa huduma kwa kutumia fedha za kigeni. Benno amekuwa chanzo kikubwa cha kudorora kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.


TAMKO LA SERIKALI KUHUSU

MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KULIPIA BIDHAA NA
HUDUMA KATIKA SOKO LA NDANI (DOLLARISATION)

1.0 UTANGULIZI

1.1 Mheshimiwa Spika, wakati wa kujadili Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2007/08 mwezi Juni mwaka huu, waheshimiwa Wabunge kadhaa walihoji hali isiyoridhisha ya ongezeko la matumizi ya fedha za kigeni, hasa dola ya Kimarekani, katika biashara hapa nchini yaani “Dollarisation” . Hoja hii ilijitokeza pia wakati wa kujadili mapendekezo ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji pamoja na Wizara ya Fedha. Aidha, suala hili limekuwa likijitokeza katika vyombo vya habari kutokana na wananchi kutaka kufahamu sababu za hali hii pamoja na athari zake kiuchumi.

1.2 Mheshimiwa Spika, “Dollarisation” katika uchumi inatafsiriwa kuonyesha kiasi cha matumizi ya sarafu ya Ki-Marekani (Dollar) kwa matumizi ya ununuzi wa vitu vya kawaida katika nchi nyingine. Kwa maana hiyo matumizi ya sarafu ya Ki-Marekani katika mauziano ya bidhaa mbalimbali nchini Tanzania, ni “dollarisation” ya uchumi wa Tanzania. Hali kama hii kisoko inazikumba nchi zenye chumi dhaifu, ambazo wananchi wake wanakuwa na imani hafifu katika sarafu ya nchi zao kwa sababu moja au nyingine, na kutaka kujikinga kwa kupokea na kuweka akiba zao katika sarafu ya nchi nyingine kutokana na kuwa na imani na uimara wa sarafu hiyo. Chumi kadhaa za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini zinakumbwa na hali kama hii.

2.1.3 Sababu mojawapo inayopelekea kupotea kwa imani na sarafu ya nchi, ni kushuka kwa haraka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo mara kwa mara. Thamani ya shilingi ya Tanzania imekuwa ikishuka kwa muda mrefu ikilinganishwa na thamani ya sarafu za nchi nyingi tunazofanya nazo biashara kubwa. Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa katika miaka mitano kabla ya kuondoa udhibiti wa fedha za kigeni (Exchange Control), thamani ya Shilingi ya Tanzania ilishuka toka Shillingi 125 kwa dollar moja ya kimarekani mwaka 1988 hadi Shilingi 335 kwa dollar moja ya kimarekani mwaka 1992. Hii ni kushuka kwa thamani kwa wastani wa asilimia 67 kwa kila mmoja wa miaka hiyo minne. Kushuka huku kwa thamani wakati Tanzania ilikuwa na sheria kali za kuthibiti fedha za kigeni kunaonyesha kuwa nguvu za soko kutokana na udhaifu wa uchumi wetu uliilazimisha Serikali yetu kupunguza thamani ya sarafu yetu kwa kiasi hicho. Katika soko, hali ya Serikali kudhibiti sana fedha za kigeni hutafsiriwa kuashiria upungufu mkubwa wa fedha hizo, na hivyo kupunguza imani katika sarafu ya nchi husika, hasa miongoni mwa watu au makampuni yanayohitaji fedha za kigeni kwa shughuli za biashara.

1.4 Baada ya kufungua soko la fedha za kigeni mwaka 1992, kasi ya kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ilipungua kiasi. Kati ya mwaka 1993 na 2000, thamani ya Shilingi ya Tanzania ilishuka kwa wastani wa asilimia 12.9 kwa mwaka, na kati ya mwaka 2000 na 2006, thamani hiyo ilishuka kwa wastani wa asilimia 5.9 kwa mwaka.

3 1.5Kwa kuzingatia takwimu hizi, na tukifahamu kuwa masharti ya udhibiti wa fedha za kigeni yamelegezwa sana hivi sasa, ni dhahiri kuwa thamani ya Shilingi hivi sasa ni kielelezo halisi cha hali halisi ya uchumi wetu unavyotafsiriwa na soko la fedha za kigeni. Kwa mantiki hiyo, ni wazi kabisa kwamba imani katika sarafu ya Tanzania inaongezeka siku hadi siku, ingawa bado kuna baadhi ya watu hawajawa na imani sawasawa na shilingi yetu.

2.0 SHERIA KUHUSU UMILIKI NA MATUMIZI YA FEDHA ZA

KIGENI NCHINI

2.1 Mheshimiwa Spika, usimamizi wa umiliki na matumizi ya fedha za kigeni una historia ndefu hapa nchini. Awali, ilikuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki fedha za kigeni isipokuwa tu kama amepewa ruhusa na Benki Kuu kwa ajili hiyo. Katika kipindi hicho, palikuwa na upungufu mkubwa wa fedha za kigeni hata nchi kushindwa kulipia mahitaji yake kutoka nje. Kama nilivyoeleza, hali hiyo ilibadilika mwaka 1992 baada ya mabadiliko ya sera na sheria ambapo wananchi waliruhusiwa kupokea, kumiliki, na kutumia fedha za kigeni kwa shughuli zao za kiuchumi.

2.2 Mheshimiwa Spika, kifungu cha nne (4), kifungu kidogo cha (b) cha Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 (The Foreign Exchange Act, 1992) kinamruhusu mtu yeyote kumilki kiasi chochote cha fedha za kigeni au dhahabu ghafi humu nchini; kuuza fedha za kigeni kwa duka la kubadilisha fedha (Bureau de Change)

au wakala aliyeruhusiwa na Benki Kuu kwa ajili hiyo; na kuwa na akaunti ya fedha za kigeni katika benki iliyoruhusiwa na Benki Kuu kwa ajili hiyo.

Mheshimiwa Spika, kanuni zinazohusu uendeshaji wa maduka ya fedha za kigeni, yaani (The Foreign Exchange (Bureaux de change) Regulations, 1999) zinawataka wageni wa muda mfupi hapa nchini wanaoishi katika hoteli au nyumba za kulala wageni kulipia gharama zao za malazi na huduma nyingine katika hoteli hizo ama kwa fedha za kigeni au shiling za Kitanzania ambazo zimepatikana kutoka katika maduka rasmi ya kubadilisha fedha. Vile vile, kifungu cha 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006 kinachotoa madaraka ya kuchapisha na kutoa fedha za Kitanzania kwa Benki Kuu pekee kinaelekeza kuwa shilingi ya Tanzania ndiyo fedha pekee ambayo hakuna mtu au kampuni yoyote nchini inayoruhusiwa kuikataa kwa malipo yoyote (legal tender).

2.4 Mheshimiwa Spika, vifungu vya Sheria nilivyovinukuu hapa vinajumuisha mambo ya msingi yafuatayo:

(1) Hakuna kipingamizi chochote cha kisheria dhidi ya wananchi kumiliki fedha za kigeni, iwe ni taslimu au akaunti katika benki;

(ii) Shilingi ya Kitanzania ndiyo fedha pekee ambayo haiwezi kukataliwa kwa ajili ya malipo hapa nchini. Kwa hiyo, ni kosa kwa mtu yeyote kukataa malipo kwa fedha za Kitanzania au kumlazimisha mtu yeyote kufanya malipo kwa fedha tofauti na shilingi za Kitanzania; na

(iii) Wageni wasio wakazi hapa nchini wanaweza kufanya malipo kwa fedha za kigeni au shilingi za Kitanzania, mradi shilingi hizo ziwe zimepatikana kupitia duka halali la

kubadilisha fedha za kigeni au benki iliyoidhinishwa na Benki Kuu.

3.0 MATANGAZO YA BEI KATIKA FEDHA ZA KIGENI

3.1 Mheshimiwa Spika, kutangaza bei za bidhaa zetu katika fedha za kigeni hakukatazwi na Sheria yoyote ya Tanzania. Mlango huu uliachwa wazi kuwasaidia wazalishaji kupata masoko ya mazao wauzayo nje ya nchi, ili wanunuzi wa bidhaa hizo waelewe kirahisi bei za bidhaa au huduma hizo. Kipengele hicho kimekuwa kikitumika vile vile ndani ya Tanzania kwa kuwalenga wageni, hasa watalii, kwa malipo ya hoteli na huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na “import handling fees” na kadhalika.

3.2 Mheshimiwa Spika ,dhana hii ya kurahisisha ujuzi wa thamani ya bidhaa na huduma tunazouza kwa wateja wa nje au kwa wasio wakazi wa Tanzania inapoteza maana yake pale kila mchuuzi hapa nchini anapotoa tangazo la bei za bidhaa zake katika fedha za kigeni na pale mnunuzi au mlipaji anapolazimishwa kulipia bidhaa au huduma kwa fedha za kigeni, aidha kwa kukataliwa kuuziwa bidhaa, au kwa kupewa kiwango cha juu sana cha kubadilisha pesa za kigeni kisichoendana na hali halisi ya soko. Kama nilivyoeleza awali, kitendo cha kukataa malipo kwa shilingi ya kitanzania ni kuvunja Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006.

3.3 Mheshimiwa Spika,Aidha ni muhimu vile vile ifahamike kuwa utekelezaji wa sera ya fedha katika uchumi huathiriwa pale ambapo sarafu inayotumika kwa mauzo nchini ni ya nchi nyingine, au pale fedha za nchi nyingine zinapoweza wakati wowote zikawa mbadala wa fedha inayotolewa na Benki Kuu ya nchi husika.

4.0 TAMKO

4.1 Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia haya, na kwa kuzingatia kwamba Waheshimiwa Wabunge wamelizungumzia sana suala hili linaloonekana kuwa ni kero kubwa kwa wananchi, Serikali inaagiza kwamba bei zote nchini zitangazwe kwa fedha ya Tanzania, yaani Shilingi ya Kitanzania. Aidha, na hasa kwa zile bidhaa na huduma zinazowelenga watalii au wateja wasio wakazi wa Tanzania, matangazo ya bei yanaweza yakawekwa kwa sarafu mbili, yaani Shilingi ya Kitanzania na fedha ya nje na malipo kupokelewa kwa sarafu ambayo mlipaji atakuwa nayo.

4.2 Pili: Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili iwekwe wazi na isizidi ile ya soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani katika soko la fedha za kigeni.

4.3 Tatu: Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote hapa nchini kwa fedha za kigeni. Mtu alipe kwa fedha za kigeni akitaka yeye mwenyewe, na kwa hiari yake.

5.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika , napenda kumalizia kwa kuwakumbusha wananchi kuwa suluhu ya kudumu ya kuimarisha thamani ya sarafu yetu ni kuongeza uzalishaji na kukubali kutumia zaidi bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini. Thamani ya sarafu ni kielelezo cha uwezo wa uchumi kukidhi mahitaji yake ya msingi, ikiwemo kulipia mahitaji ambayo hayana budi kuagizwa kutoka katika nchi nyingine. Kwa hiyo, tutakuwa tumechangia kuimarisha sarafu yetu iwapo tutaongeza mauzo yetu nje, na kupunguza matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nje ya nchi yetu. Kila mmoja wetu ana mchango wa kutoa katika jambo hili.

WIZARA YA FEDHA

DODOMA
AGOSTI 2007
 
huyu gavana ananipa wasiwasi
....zingatia aliyemtangulia yuko ,'malta'
 
As a BOT governor he has failed miserably; just look at our external debt!
 
Hii itakuwa ngumu sana, wanaoendesha biashara zao kwa fedha za kigeni, ndio hao hao wanaojidai kukataza matumizi yake.
 
picha yake haijakaa poa, naona kama tai imemkaba vile,,,macho yamemtoka
 
NSSF na PPF wanachaji rent kwa dola za kimarekani. Wizara ya utalii wanalipisha kwa dola. Na watu binafsi wataendelea kuitumia ijapo inaangamiza uchumi mpana.
 
Leo exchange rate ni 1USD for Tsh1805. Hii Nchi ishawekwa mfukoni na akina Rizi, mambo hayaendi mipango inakwama Tsh imekuwa makaratasi.
 
mbona amechelewa sana?

yaani leo ndio anakuja kuongea haya na watu tunaumia kila siku!!
 
Bogus tu hana lolote huyo Gavana. We ngoja mwezi wa tano watu wakianza kuvuna mazao utasikia ' mfumuko wa bei umepungua na Uchumi unakua'
 
Anategemea nn fedha zote zinapokua sarafu magonjwa kweli huyu kila siku tunabadili mfumo wa hela ndio ilivyo....?
 
Hili ni Bomu jingine tu. Namkumbuka wakati akifafanua ubora wa Noti mpya (Quality of the paper and printing ).
Minoti yetu yote mibovu, haikawii kuchakaa mpaka wameamua kuitoa noti ya 500 na kuweka sarafu. Jamani kama kuna mtu ameona noti za Jirani zetu Msumbiji, ni nzuri kweli ( High quality )
 
Tamko hili la serikali lina udhaifu mkubwa, linajichanganya sana.

Naomba kambi ya upinzani bungeni na wanasheria wapitie tena hili tamko, lirudi tena bungeni aidha kwa kuaanda muswada mpya wa kisheria utakaobadilisha baadhi ya vifungu, ili sheria itamke waziwazi kuwa ni kuvunja sheria kufanya biashara ya aina yeyote nchini Tanzania kwa sarafu ya nchi nyingine.
 
Hili ni Bomu jingine tu. Namkumbuka wakati akifafanua ubora wa Noti mpya (Quality of the paper and printing ).
Minoti yetu yote mibovu, haikawii kuchakaa mpaka wameamua kuitoa noti ya 500 na kuweka sarafu. Jamani kama kuna mtu ameona noti za Jirani zetu Msumbiji, ni nzuri kweli ( High quality )

Nakubariana na wewe Msumbiji wana noti nzuri.yani Nchi yetu kila kitu siasa tu. uchakachuaji mtupu,waliambiwa mapema hii noti ya sh.500 mbovu wakasema ooh sababu ipo kwenye mzunguko mkubwa wakati zile za zamani hazichakai kama hizi mpya. Mwisho wa siku wamekubari na kuleta silver na hiyo tayari ni kishusha thamani ya hela
 
Back
Top Bottom