TAMISEMI yafanya uhakiki wa walimu

TAMISEMI yafanya uhakiki wa walimu

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Dar es Salaam. Serikali imeanza uhakiki wa walimu wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu wanaofundisha shule za msingi.

Uhakiki huo ulioanza Januari 22,2018 unatakiwa kukamilika Januari 31,2018 na unasimamiwa na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu Januari 29,2018 Katibu Mkuu- Tamisemi, mhandisi Mussa Iyombe amesema uhakiki huo unalenga kupata idadi ya walimu wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu waliopo shule za msingi ili kuwa na taarifa zao na watakapohitajika sekondari wapelekwe.

“Tunataka tupate idadi kamili ya walimu wenye masters (Shahada ya Uzamili) ambao wapo shule za msingi,” amesema Iyombe.

Maelezo ya Iyombe yanatokana na barua yake ya Januari 22 aliyoitoa kwenda kwa makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara iliyokuwa na kichwa cha habari ‘orodha ya walimu wenye shahada ya uzamili ya elimu wanaofundisha shule za msingi.”

Katika barua hiyo, Iyombe anasema “Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu. Ofisi ya Rais -Tamisemi inafanya zoezi la ukusanyaji wa taarifa muhimu za walimu wote wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu waliopo katika shule za msingi.”

“Kwa barua hii, mnaombwa kuwataka wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ndani ya mikoa yenu kukamilisha taarifa za walimu hao kwa kuzingatia muundo (template) wa kukusanyia taarifa hii (umeambatishwa).”
Iyombe ametaka taarifa hizo ziwasilishwe Ofisi ya Rais- Tamisemi kabla au ifikapo Januari 31.
Chanzo:Mwananchi
 
Hizi figisu hizi zinachekesha saana, leo Hii wanataka watoke tena Primary wapelekwe Secondary? Hakuna other priorities? Mfano, Shule hazina vitabu vya kutosha, miundo mbinu mibovu, umeme, ukosefu wa chakula cha mchana kwa watoto, wanafunzi wenye mahitaji Maalumu nakadhalika, wewe unakomaa na Walimu tuuuu
 
kwa maoni yangu naona ni sawa kwa kiasi fulani tukiachana na habari za ajira mpya. Mwalimu mwenye shahada ya uzamili kuendelea kufundisha shule ya msingi ni kumdhalilisha. waende hatua ya juu zaidi wakafundishe Secondari.
 
Wa art(stashahada nk) sekondari wanashushwa msingi kufundisha na wenye shahada za uzamili(art pia ?)walioko msingi wanapandishwa sekondori kufundisha !.Msingi watabaki wa vyeti na stashahada,mbona hii itakuwa vurugu kazini? Wa vyeti watajihisi ni wanyonge dhidi ya wenye shahada.Staff zitagawanyika linapokuja suala la uwajibikaji.
 
sawa kabisa
 
Kama una cheti una cheti tu haitabadilika kama hujaenda kusoma zaidi.Staff kamwe hatagawanyika kwasababu kila mmoja ameajiriwa kwa elimu aliyokuwa nayo.
 
Kumuacha mwalimu mwenye Msc,afundishe shule ya msingi,ni ubadhrifu wa taaluma
 
kwa maoni yangu naona ni sawa kwa kiasi fulani tukiachana na habari za ajira mpya. Mwalimu mwenye shahada ya uzamili kuendelea kufundisha shule ya msingi ni kumdhalilisha. waende hatua ya juu zaidi wakafundishe Secondari.
wengi wao hawapendi
 
Hawajalazimishwa kunako huko, wengi wanapenda na hawataki kabisa kusikia sekondari. Kwa kuwa ngazi za mishahara ni zile zile kutegemeana na elimu na muda uloanza kazi. Sasa kuna haja gani?
 
Madaraja walimu wasahau kabisa kwa mwenendo huu,maana mwaka huu ni hamisha hamisha mpaka uishe,labda 2019 tena.
 
wengi wao hawapendi
ni kweli. wengi wao vichwani wapo empty sana pamoja na kuwa wana Masters. si unajua shule zao wengi ni za kuunga unga kuanzia QT, Grade A, Diploma, then Bachelor na Masters za Open na akina Eckernforde University na wengine wanaofanana na hao.
 
Hawajalazimishwa kunako huko, wengi wanapenda na hawataki kabisa kusikia sekondari. Kwa kuwa ngazi za mishahara ni zile zile kutegemeana na elimu na muda uloanza kazi. Sasa kuna haja gani?
ni kweli. wengi wao vichwani wapo empty sana pamoja na kuwa wana Masters. si unajua shule zao wengi ni za kuunga unga kuanzia QT, Grade A, Diploma, then Bachelor na Masters za Open na akina Eckernforde University na wengine wanaofanana na hao.
 
Dar es Salaam. Serikali imeanza uhakiki wa walimu wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu wanaofundisha shule za msingi.

Uhakiki huo ulioanza Januari 22,2018 unatakiwa kukamilika Januari 31,2018 na unasimamiwa na Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Akizungumza na MCL Digital le ? KAo Jumatatu Januari 29,2018 Katibu Mkuu- Tamisemi, mhandisi Mussa Iyombe amesema uhakiki huo unalenga kupata idadi ya walimu wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu waliopo shule za msingi ili kuwa na taarifa zao na watakapohitajika sekondari wapelekwe.

“Tunataka tupate idadi kamili ya walimu wenye masters (Shahada ya Uzamili) ambao wapo shule za msingi,” amesema Iyombe.

Maelezo ya Iyombe yanatokana na barua yake ya Januari 22 aliyoitoa kwenda kwa makatibu tawala wa mikoa Tanzania Bara iliyokuwa na kichwa cha habari ‘orodha ya walimu wenye shahada ya uzamili ya elimu wanaofundisha shule za msingi.”

Katika barua hiyo, Iyombe anasema “Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu. Ofisi ya Rais -Tamisemi inafanya zoezi la ukusanyaji wa taarifa muhimu za walimu wote wenye Shahada ya Uzamili ya Elimu waliopo katika shule za msingi.”

“Kwa barua hii, mnaombwa kuwataka wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa ndani ya mikoa yenu kukamilisha taarifa za walimu hao kwa kuzingatia muundo (template) wa kukusanyia taarifa hii (umeambatishwa).”
Iyombe ametaka taarifa hizo ziwasilishwe Ofisi ya Rais- Tamisemi kabla au ifikapo Januari 31.
Chanzo:Mwananchi
HILI SIONI KAMA NI KITU CHACKUTANGAZIA WANANCHI NDIO KAZI ZENU ZA KILA SIKU
 
Uhakiki usiokwisha ni kichaka cha kupigia pesa awamu hii..
 
ni kweli. wengi wao vichwani wapo empty sana pamoja na kuwa wana Masters. si unajua shule zao wengi ni za kuunga unga kuanzia QT, Grade A, Diploma, then Bachelor na Masters za Open na akina Eckernforde University na wengine wanaofanana na hao.
Na mimi ndo nashangaa eti wapelekwe sekondari na elimu zao za kuunga unga. Secta ya elimu ndo ina watu ufahulu hafifu ila sababu kuu ni kutokana na kuwepo malipo kiduchu.
 
kwa maoni yangu naona ni sawa kwa kiasi fulani tukiachana na habari za ajira mpya. Mwalimu mwenye shahada ya uzamili kuendelea kufundisha shule ya msingi ni kumdhalilisha. waende hatua ya juu zaidi wakafundishe Secondari.
Tatizo wanaweza wapandisha na kuwapeleka secondary lkn malipo yao yakawa ni yaleyale.

Kuna shemeji yangu ana shahada ya uzamili huu ni mwaka wa tatu sasa anafundisha primary school na mshahara ni uleule wa diploma.
 
Back
Top Bottom