TAMISEMI: Tume ya Utumishi wa Walimu, fanyeni msawazo wa walimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuweka uwiano

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
Waziri Ummy - Fanyeni msawazo wa waalimu nchini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameielekeza Tume ya Utumishi wa waalimu nchini kuhakikisha wanafanya msawazo wa waalinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuweka uwiano sawa wa waalimu nchini.

Akiongea na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa waalimu Jijini Dodoma Waziri Ummy amaesema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa baadhi ya shule kuwa na waalimu wengi huku nyingine zikikosa waalimu, hivyo ni wajibu wa tume kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa kwa wakati

Waziri Ummy amesema kuna baadhi ya shule zina watoto wengi lakini waalimu ni wachache huku shule nyingine zikiwa na waalimu wengi wanafunzi wachache, ni vyema kukawa na uwiano ulio sawa katika shule zote nchini.

“Tunafahamu kuwa zipo shule ambazo zinawaalimu wachache hasa maeneo ya vijijini, lakini nyingine zinawaalimu wengi, suala hili halikubaliki, suala hili linahitajika kufanyiwa kazi ingawa mara nyingi serikali inaangalia idadi ya wanafunzi “amesisitiza Waziri Ummy

Waziri Ummy ameendelea kueleza kuwa kutokufanya msawazo hatuwatendei haki wanafunzi walioko vijijini hasa katika maeneo ya pembezoni ni wajibu wa tume kuhakikisha shule zote zinakuwa na idadi sawa ya waalimu

Aidha amewaelekeza Tume ya Utumishi wa Waalimu nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika kutatua kero za waalimu nchini ili kupunguza changamoto hizo kwa haraka na kutoa mrejesho kwa waalimu kwa wakati
IMG_20210908_201444_229.jpg
IMG-20210908-WA0072.jpg
 
Mawazo haya ni mazuri lakini bado Ummy kama Waziri mwenye dhamana lazima ajue yafuatayo;

Hakuna tofauti ya kimaslai kati ya mwalimu wa mjini na yule wa kijijini. Swali ni rahisi tu; kwanini mwalimu akae mjini na sio kijijini?

Serikali lazima iweke jitihada za kipekee kwenye kudeal na walimu wa vijijini. Kungekuwa na jitihada makusudi za kiserikali mathalani hata posho tu au miundombinu mizuri mbona kijijini walimu wangeenda wenyewe bila hata kuswagwa.

Lakini hata katika zile privileges tu kama malipo ya fedha za uhamisho, rikizo n.k nadhani walimu wa vijijini wangepewa upendeleo kabla ya wale wa mjini ungeona kama kuna mwalimu angekaa mjini tofauti na hali ilivyo sasa.

Mwisho, hata madaraja ingetakiwa mwalimu akiwa kijijini apande daraja haraka na kwa muda mfupi kuliko wale wa mjini ambao ndio wapiga magumashi na wanapanda faster tu.

Sasa kama hamna strategies yoyote hata kwa ufinyu wa budget iliyopo huwezi kubadilisha chochote

Vita ili upigane vizuri ni lazima uwe na mbinu na sio kusema tu na kutoa maagizo. Vitendo huongea vizuri zaidi kuliko maneno
 
Aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa, sasa msawazo wanini kwa waliopo ,Ni Bora wafanye msawazo kwa kuongeza walimu pale penye upungufu ili huo msawazo upatikane
 
Aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa,Sasa msawazo wanini kwa waliopo ,Ni Bora wafanye msawazo kwa kuongeza walimu pale penye upungufu ili huo msawazo upatikane

Walimu wanakuwa na mikataba ya ajira ambayo haioneshi vituo vyao vya kazi? Utaratibu ule mwl kufanya kazi ambapo na mweza wake yuko wameupatia mwarobaini?
 
Leo ndiyo usingizi umekata! Watu tunashangaa kwanini shule x ina walimu 2 na shule y ina walimu 70? Tuko serious kweli kama nchi? Hata baba.
 
Kwa akili hizi tatizo la uhaba wa walimu halitakuja kuisha milele na milele.

Yaani waziri badala ya kuajiri walimu wapya kukabiliana na upungufu uliopo anaagiza halmashauri zifanye msawazo. kwa walimu gani waliopo?

Huyu waziri kumbe naye chenga
 
TSC wanahusikaje sasa na kupanga walimu kwenye vituo??? Unajua TAMISEMI inahitaji waziri muekewa wa karibia kada zote.... Ummy anayumba kama gwajigeli.
 
Bado Sana,kuweka msawazo wa walimu Tanzania.
Mwalimu wa vingunguti A primary school,ambae Ana uhakika wa kuuza ubuyu na vinamba na kupata sh 35000 kwa siku na ikija zamu ya kufanyisha mitihani jumamosi anapata laki tatu,atakubalu vipi atoke sense shule ya msingi kwediboma? Handeni Tanga
 
TSC na kupangia walimu vituo ni sawa na jwtz na kwenda kuongoza magari barabarani.


mamlaka ya uhamisho ndani ya halmashauri ni mkurugenzi mtendaji.


je, ummy hana kitu kichwani isipokiwa mfumo umembeba.
 
Back
Top Bottom