TAMISEMI mmesahau kuwapangia shule vijana waliohitimu kidato cha nne?

Kwani

JF-Expert Member
Jan 12, 2016
455
562
Ni miezi minne sasa tokea matokeo ya kidato cha nne yatoke lakini hadi leo hamjapanga shule kwa wanafunzi hao.

Kwa elimu ya kidato cha tano hamjafuta michango sasa mnafikiri mzazi anawezaje kujiandaa kwa wiki mbili?

RAI: Toeni hayo machaguzi ya shule haraka wazazi tujue mbivu na mbichi.
 
Ni miezi minne sasa tokea matokeo ya kidato cha nne yatoke lakini hadi leo hamjapanga shule kwa wanafunzi hao. Kwa elimu ya kidato cha tano hamjafuta michango sasa mnafikiri mzazi anawezaje kujiandaa kwa wiki mbili?
RAI:toeni hayo machaguzi ya shule haraka wazazi tujue mbivu na mbichi.
Hapa ni kazi tu-sasa hivi wako busy kudhibiti Chadema na Ukawa kwenye halmashauri, wakimaliza watarudi kwenye hilo...!
 
Siku hizi kidato cha tano wanaingia mwezi wa saba kama zamani?

Au nini kimetokea?

Usishangae wakaingia hata mwakani
Since 3 years ago. Si lazima uwe unasomesha. Kujua kinachoendelea kwenye sera za umma ni wajibu kwa wananchi.
 
Hapa ni kazi tu-sasa hivi wako busy kudhibiti Chadema na Ukawa kwenye halmashauri, wakimaliza watarudi kwenye hilo...!

Hivi wanaanda wanafunzi wanaojua kukariri au wanafunzi wabunifu.
Kufaulu masomo sio kipimo cha ubunifu.
Tuandae wanafunzi wabunify watakao endana na changamoto za mabadiliko ya sasa sio wanafunzi wa kukariri firmula na notes zilizopitwa na wakati.
 
Since 3 years ago. Si lazima uwe unasomesha. Kujua kinachoendelea kwenye sera za umma ni wajibu kwa wananchi.
Asante kwa taarifa.

Tatizo mfumo wetu wa elimu unachezewa mno kila mara inavurugwa haiko stable kama nchi zingine
 
Back
Top Bottom