Tamisemi imeitosa manispaa ya ilala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamisemi imeitosa manispaa ya ilala

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shanat, Mar 5, 2012.

 1. S

  Shanat Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza nawapa pole sana watumishi wote wa Manispaa ya Ilala kwakuingiliwa na hawa wanao jiita waheshimiwa maana kama ni ulafi basi ndiyo wamekubuhu maana wanashindana kuchukua miradi na sasa wana shindana kuchukua vyanzo vya mapato kwa kisingizio cha ubinafsishaji. watumishi ambao ndiyo watendaji hawana haki wala sauti mbele ya wababe hao. kwakweli kwenye Halmashauri hiyo Madiwani wenye akili zao kama wapo basi hawazidi watano!

  Ukianzia na huyo wanaye muita Meya Kwa kweli hicho cheo kimemchanganya kabisa tatizo lake kubwa ni umri kwa kweli unapo msikiliza kwa dakika chache za mwanzo unaweza ukafikiri unaongea na mtu mwenye upeo mkubwa lakini kadiri unapo ongea naye issues za maana taratibu utaanza kumtoa nje ya mstari ameisha na anakusudia kuingia mikataba mingi mibovu kwa kushirikiana na mwanasheria wa Manispaa ambaye amekuwa akikaimishwa ukurugenzi mara kwa mara.

  Huyu meya kijana msimi wa digrii ya IT amekuwa ndiye Mkurugenzi wa manispaa kila kitu anaamua yeye mikataba yote anaingia yeye kwa kuanzia anampango wa kufukuza mgambo wote ili alete askari wa KK Security,maana hata jimboni kwake amehama amehamia Mtaa wa Bibi titi ambapo analindwa na kampuni ya ulinzi KK badala ya mgambo wa MANISPAA.

  Ameisha waingiza watu wake kwenye mpango wa kukusanya ushuru wa taka maana katika kata 26 za manispaa manispaa inakusanya kata tano tu zingine 21 anajua zinaenda wapi na hizo kata tano kuna watu wanakusanya pesa hizo lakini ni mgao wao hao wanao jiita wakubwa mfano kuna pesa inakusanywa na Maltinet haijulikani inaenda wapi.Meya huyu ameingia mkataba na DCB kukusanya fedha ya Huduma za Jiji kinyume na agizo la serikali.

  Meya huyu amechukua tenda ya vyoo vya umma,meya huyu ameikodishia manispaa gari lake ambalo analipwa kila siku wakati gari hilo halina kazi yoyote.meya huyu amegeuza ofisi yake kama danguro maana kuna wakati huingia usiku na vimada wake na kukesha humo mpaka alfajiri ,hivi ofisi ya serikali chumba, kitanda,bafu vya kazi gani ofisini?

  Ukusanyaji wa mapato umekuwa siasa ukienda kudai kodi kwa jamaa wa hao madiwani unajitafutia mgogoro mkubwa madiwani wengi wana biashara zao lakini hawataki kulipa kodi. OMBI KWA TAMISEMI kamakweli Tamisemi inataka Halmashauri zijiendeshe basi wafikirie upya muundo wa hizo Halmashauri Maana madiwani ni mzigo!bora halmashauri zikawa kama TRA kazi itafanyika kama enzi ya TUME YA KEENJA!

  Najua TAMISEMI kuna watu wenye uelewa mkubwa kama Bw.Katanga (katibu mkuu) wanaweza kuokoa jahazi hili ikiwa ni pamoja na kuweka wazi mipaka ya kazi Madiwani maana wamekuwa ni tishio kiasi kwamba Mkurugenzi hana kauli kabisa mbele ya wababe hao.

  Bahati mbaya taarifa yangu inaweza kuwa sijaiandika katika utaratibu mzuri hata hivyo naomba kuwasilisha!
   
 2. S

  Shanat Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na cha kushangaza zaidi Meya anapo jibu hoja nyingi humu jamvini huwa anajibu mambo ambayo hayamuhusu(mambo ambayo anatakiwa ajibu mkurugenzi) mfano sakata alilolianzisha kwa Mhesimiwa Magufuri alidai mabango yakiondolewa mapato hayatapatikana ,mara ooh! kuna watu tutawapeleka mahakamani ,hivi kweli meya kazi yake ni kuzungumzia mapato? au kuwapeleka wakwepa kulipa kodi mahakamani? Mkurugenzi kazi yake ni nini?
   
 3. m

  mymy JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ukweli kuna mambo yanatendeka hayaeleweki. manispaa ya ilala mapato makubwa maendeleo zero. kuna kipindi wakusanyaji kama miezi 3 gari la kukusanya taka halikupita mtaani kwetu lakini ushuru wakaja kukusanya, hatukuwapa tuliwagomea kabisa
   
 4. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukisikia wivu ndio huo sasa kama jamaa anapiga tenda ili ajipatie kipato bila kuathiri matumizi mabaya ya madaraka kunatatizo gani? yani ata mimi ningekua meya alafu napata oportunity ya kupata tenda unataka nimuachie nani?tatizo lenu nyie watanzania mna wivu wa maendeleo ,nenda kaangalie meya wa jiji la washington then uje apa kulaumu
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ndefu sana nitarudi baadae
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  ndo maana ufisadi hauishi.......
   
Loading...