Tamil tigers

Echolima

JF-Expert Member
Oct 28, 2007
3,826
2,057
Kwa kipindi kirefu tumekuwa tukisikia vita vinaendelea kati ya majeshi ya syri-lanka na waasi wa Tamil tiger,juhudi nyingi sana zimefanywa kuweka suluhisho lakini juhudi hizo zimekuwa zikizimwa na serikali ya syri-lanka kwa kukataa suluhisho lolote la Amani hivyo kusababisha janga kwa raia wasio na hatia,wakati huo huo jumuia ya kimataifa imekaa kimya bila kufanya juhudi zozote za maksudi kama walivyoishinikiza Israel wakati wa vita vyake na Hamas.
Kitendo kama hiki kisifumbiwe macho maana maisha ya watu wasiona hatia wanakufa bila msaada wowote.
 
Hawa Tamil tigers waliisumbua sana serikali ya Sri Lanka kwa zaidi ya miaka 20,sasa hivi serikali imewabana kwenye eneo dogo la km 10 za mraba na hawataki kusikia la mtu wanaona hii ni nafasi ya kumaliza tatizo.
Tamil tigers pia ni wavumbuzi wa bomu la kijitoa muhanga 'suicide belt' linalosumbua sana dunia kwa sasa.
 
Kuwa mwanzilishi wa kujitoa mhanga haihalilishi Wa-Tamil kuuliwa bila huruma kumbuka kuna raia watoto kwa wanawake wanateseka kwa kunyimwa chakula maksudi na majeshi ya serikali.World must do something to save human life.
 
Sikatai kuwa maisha ya raia yanapotea,nilikua nakupa wanavofikiria serikali ya Sri Lanka, halafu silaha hizo za serikali wamepewa na nchi za Magharibi ambao wamewatangaza Tamil Tigers kama 'Terrorist group'.Nchi hizo zinaogopa kuongea sasa.
 
Back
Top Bottom