Tambua mambo 7 kutoka katika tamaduni za watu Wa Maori

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Habari za asubuhi wakuu, Idd mubarak wadau. Ni matumaini yangu kuwa umzima wa afya. Kwa wale wagonjwa mpate afya njema na ahueni.

Naomba kuleta kidogo uzi kuhusu mambo nayoyajua kuhusu jamii ya watu wa Maori. Karibuni sana:

Maori ni jamii inayopatikana katika nchi ya New Zealand, na ni wa asili ya jamii za Polynesian ya mashariki. Inasemekana kuwa Jamii hii iliingia New Zealand katikati ya miaka ya 1250 na 1300, kwa kutumia majahazi.

Kutokana na kuwa wapweke sana Jamii hii ilipofika katika pwani ya New Zealand walianzisha tamaduni yao ya kipekee, mfumo Wa Lugha, sanaa ya kipekee pamoja na hadithi zenye kubeba historia yao.

Hapa chini ni mambo saba ambayo nadhani wengi wetu hatukuwa na ufahamu nayo:
1. Ta moko ni mtindo Wa kitamaduni wa jamii ya Maori, wa kuchora tattoo au chata katika mwili. Cha ajabu kuhusu Ta moko ni kuwa tattoo hizi uonesha au uhakisi mambo yanayomuhusu mhusika yaani anayechorwa. Kwani kupitia tattoo hizi huweza kuonesha ujuzi Wa mtu, nafasi yake ndani ya jamii. Mfano: Ta moko atakayochorwa Chief ni tofauti na Mvuvi. Mwanzoni Tattoo hizi zilikuwa zikichorwa kwa kutumia kitu kama mfupa uliochongoka mwishoni ambao ndo hutumika kuchora kwa mtindo Wa kupigwa au kudonolewa katika ngozi.

2. Je unajua kuwa Maori hawakuwahi kuwa na lugha ya maandishi. Kabla ya ujio wa walowezi wa ulaya, jamii hii ilikuwa na mtindo mmoja wa mawasiliano, yaani mawasiliano kwa njia ya mdomo tu. Masimulizi, elimu pamoja na historia yote ilifundishwa kwa njia ya mdomo tu. Hii ilipelekea kupatikana kwa wataalamu wa kusimulia na watunza kumbukumbu wazuri sana. Yaani ukiangalia wasimuliaji hodari kumi wa hadithi basi hautowakosa Watu kutoka Maori saba.

3. Ulishawahi kula msosi uliopikwa chini ya ardhi. Maori wanao wapishi hodari sana. Hasa katika upishi wa nyama inayoitwa "Hangi" ambayo ni mchanganyiko wa nyama pamoja na mboga za majani. Kwa wale watalii hupata kuonja utamu wa nyama hizi wakiwa kwenye utalii ndani ya New Zealand. Mawe yanapashwa moto mpaka mengine kuwa mekundu kabsa, halafu uchimba chini na uyapanga mawe hayo kisha chakula kama ni nyama ya mbuzi au kitimoto uwekwa kwa juu, baada ya hapo kitu uiva chenyewe.

4. Salamu ya kipekee sana. Ndani ya utamaduni wa Maori utakutana na salamu yenye utofauti na jamii zingine. Hii huitwa "Hongi" ambapo mtu usalimiana na mwenzake kwa kugusanisha sehemu ya mbele ya vichwa vyao pamoja na pua, wakati huo wamefumba macho na kupumua kwa Nguvu. Ni ajabu eehh, lakini wao wana sababu yao kusalimiana hivi. Kwani hii umaanisha mnashirikishana na kupokezana pumzi ya maisha ambapo roho hukutana.

5. Kwa wale wageni na watalii ukitaka kuingia ndani ya jamii hii au kuitembelea basi lazima ukaribishwe kwenye uwanja wa "Marae" na ili uingie kwenye uwanja huu kuna jaribio ni sharti ulipitie "Powhiri" ambapo unakutana na shujaa mmoja wapo wa Maori, hii uhusisha kuimba, pamoja na kupiga stori pia ni kwa nia ya kuonesha kuwa unataka kufanya mjumuiko wa amani na wao.

6. Jamii ya Maori ni kati ya zenye hadithi nyingi sana duniani. Hii ni kutokana na hoja niliyoieleza hapo juu (2). Hadithi kuhusu milima, wanyama, mito, mizimu, uchawi, asili yao na dunia, pamoja na mambo mengi sana. Hadithi nyingi hutumika kufundisha watoto na Vijana kuhusu kuwa na tabia njema pamoja na kuelezea ufumbuzi wa matatizo mbalimbali.

7. Hii ni kwa wale wafuatiliaji wa michezo ya Rugby. Ni kawaida kushuhudia kabla ya mechi yoyote ya timu ya taifa ya New Zealand kucheza dance. Hii dance inaitwa "Haka" na huashiria baraka & ushindi kabla ya vita. Lakini ijapokuwa watu wengi wanadhani ya kuwa "Haka" ni kwa ajili ya vita, laah ni zaidi ya hivyo Kwani ndani ya jamii hii kuna aina mbalimbali za "Haka". Hii hutokana na aina ya tukio, msiba, sherehe za kichifu, sherehe za mavuno, zote hizi hutofautiana namna na uchezaji.

Mpaka hapo sina cha zaidi.

Asante sana.
I stand to be corrected anywhere.

Mead-Norton-Mitai-138sm0-1.jpeg
TVns9HXsQEZXWBbTBL9_mQeDRChKNw3A87JCYiksGDqMao5poTcIVifdleETztULeeAjHWOZtUZM6y890S8glHvJKq5Eh...jpeg
o1AJ9qDyyJNSpZWhUgGYc3MngFqoAMfoy4D3dv8UFdX2umjYz.jpeg
mor-1920x1080.jpeg
Whakairo-Ta-Moko-SIZED.jpeg
 
Kuna uzi humu unarlezea habari ya kifaa fulani kinaitwa 'Koteka'. Hawa ndio wahusika!??
Koteka ni kifaa kinachotumika kufunika uume Wa watu wenye jinsia ya kiume. Hii utumika sana kwa jamii za Papua New Guinea mkuu. Hawa hawana hii kitu...

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mwaka wanapokea watalii kiasi gani wanaokwenda kuangalia urithi huo wa kiutamaduni ?
Huku wana rekodi njema sana ya kupokea watalii kwani kufikia mwaka 2018 mwezi wa Machi ilikuwa imeshaingiza watalii zaidi ya milioni 3.82. Hii ni kwa mujibu Wa Stats NZ. Kwa kawaida uingia zaidi ya watalii milioni 2.5
 
Huku wana rekodi njema sana ya kupokea watalii kwani kufikia mwaka 2018 mwezi wa Machi ilikuwa imeshaingiza watalii zaidi ya milioni 3.82. Hii ni kwa mujibu Wa Stats NZ. Kwa kawaida uingia zaidi ya watalii milioni 2.5
Dr Kigwangala ana la kujifunza kutoka kwao
 
Dr Kigwangala ana la kujifunza kutoka kwao
Hawa Jamaa wamefanya kuendeleza baadhi ya vitu ama mila zenye kubeba mpaka alama ya New Zealand. Utalii wao ni mtalii anajifunza mpaka kuburudika na Wameboresha maeneo mengi kufanikisha au kuwavutia watalii wengi kila siku.
 
Back
Top Bottom