Tambua hatari na chukua hatua za kujikinga

Tambua hatari na chukua hatua za kujikinga

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,214
Reaction score
1,701
Mit 22:3 SUV
[3] Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.

Sio ajabu kumwona mtu anakimbilia jambo ambalo ameliona kabisa lina athari kwake, linaweza likawa na athari kwenye maisha yake ya kimwili au kiroho.

Tunaweza kuona ni kitendo cha kishujaa ila wakati mwingine ni ujinga, maana sio kila mtu anayechukua hatua ya kukimbilia au kuyaendea mambo mabaya ni jasiri.

Mtu mwenye busara, akiona hatari au mambo ambayo anajua yanaweza kumletea matatizo mabaya katika maisha yake, atajiepusha nayo mbali.

Mtu aliyekosa hekima au busara, hukimbilia mambo mabaya bila kuchukua tahadhari yeyote, jambo ambalo lina mwisho mbaya na kujikuta ameumia vibaya.

Mtu mwenye busara huyaona mambo kwa jicho la ndani kabisa, huona ishara za hatari kwenye hilo jambo, anaona madhara ya hilo jambo mapema.

Haishii kuona na kupuuza, huchukua hatua za kujikinga na hilo jambo lisije likamkuta na kumwangamiza, tofauti na mtu asiye na busara huyaendea mambo kwa pupa na kumwangamiza.

Mtu mwenye busara huona mtego mbaya wa dhambi, wengine wanaweza wasione au wakaona na kupuuza, mwenye busara hayawezi kupuuza jambo ambalo linaenda kuvunja uhusiano wake na Mungu.

Mit 27:12 SUV
[12] Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha; Bali wajinga huendelea mbele wakaumia.

Tunapaswa kuwa na tahadhari na hekima, hii itatusaidia kutoingia kwenye mitego ya adui, hatupaswi kunaswa na mtego mbaya wa kutuangamiza katika maisha yetu.

Jambo lolote la hatari hupaswi kulichukulia kawaida na kulipuuza, kama unaweza kulishughulikia fanya hivyo, na kama unapaswa kuliepuka mbali usiache kufanya hivyo.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 
Back
Top Bottom