Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 740
- 828
Naam habari za wakati !
Tambiko ni ibada maalumu ya jadi inayofanyika ili kuomba jambo fulani toka kwa nguvu zisizoonekanika kwa macho ya kibinadamu, watu wengi hupendelea kuita nguvu hizi mizimu. Inasemwa kuwa, wakati mwingine matambiko hufanyika ili kuituliza mizimu hiyo inapokuwa imekasirika.
Binafsi yangu sina uzoefu sana lakini yasemwa kuwa, aghalabu ibada za matambiko huambatana na kafara za aina mbalimbali kama vile; uchinjaji wa wanyama na ndege kama vile njiwa, kuku, mbuzi, kondoo na ng'ombe. Lakini pia wakati mwingine pombe, chakula, vitenge pamoja na nafaka.
Ibada za matambiko zipo na zinafanyika sehemu zote ulimwenguni, lakini ajabu ni kuwa ikifanyika ama ikifanywa na mtu mweusi wajinga hudhani kuwa ni kosa kifalsafa au hata kisheria.
Kwa nafasi ya kipekee kabisa, naomba nitumie jukwaa hili kuwapongeza Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa mtwara, wakiongozwa na mwenyekiti, kamarada Abuu Athumani Yusufu (chanzo cha majina sio cha uhakika), kwanza, kwa kukumbuka mila zetu sisi kama waafrika lakini pia kwa kumuombea afya na majukumu mema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakika hili ni jambo la faraja na upendo.
UHALALI WA KUFANYA TAMBIKO KWA MUJIBU WA KATIBA.
Katiba yetu haijataja neno tambiko moja kwa moja, lakini kwa vile tumesema kuwa tambiko ni ibada, na ibada ni shughuli ya kidini, ibara ya 19 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeelezea uhuru wa mtu kuamini ama kuabudu katika dini yeyote aitakayo.
"19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake."
Baada ya nukuu hiyo, ninawiwa kusema kwamba vijana waliofanya tambiko la kumuombea Rais wa nchi wamefanya tukio halali na hawapaswi kutajwa kama kitu cha ajabu.
KADA WA CHAMA CHA SIASA NI NANI?
Kada ni mwanachama wa chama cha siasa ambaye ameandaliwa na anategemewa kukitumikia chama kwa weledi mkubwa na kwa viwango vya hali ya juu. tafsiri hiyo ya kada ni muhimu ili chama kiendelee kukua kiitikadi, wingi wa idadi ya wanachama pamoja na uwezo wa chama husika kuweza kushinda uchaguzi. ili hayo yote yafanyike basi chama hakipaswi kuadimika kwenye akili na masikio ya wananchi.
Walichokifanya UVCCM MTWARA, ni shughuli ya kukuza chama kiroho na hii ni kutupa taarifa kwamba, Chama Cha Mapinduzi, si tu kinategemea misingi inayotokana na fikra za kibinadamu kama vile uwazi na uwajibikaji bali hata pia kinatanguliza nguvu kubwa kubwa za kiroho mbele. Jambo ambalo linaweza kugarantii uhai wa chama miaka mingi hapo baadae.
Ibada hiyo iliyofanyika mtwara na UVCCM, inapenya moja kwa moja na inatosha katika vigezo vya ufia chama, weledi, na viwango vya hali ya juu kabisa vya kukitumikia chama kiimani na kivitendo.
Kwa kumalizia, Tambiko lililofanywa na UVCCM ni mbinu ya hamasa kwa wanachama. taarifa kama hizi hukifanya chama kisipotee kwenye masikio ya wananchi na ndio uhai wenyewe wa chama huo. Mikoa mingine nayo wafanye ibada hiyo kwa wingi kwani wingi wa ibada ndo wingi wa usalama wa taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki UVCCM.
YUSUFU R H SABURA
0750883466/0717934194