Wakati maandalizi ya Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025 yakipamba moto wake, hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan nayo imekazia amani na utulivu kipindi cha uchaguzi.
Akihutubia kwenye Baraza la Eid El Fitr kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar, Rais Samia amewataka viongozi wa dini kuomba amani kuelekea Uchaguzi Mkuu na kukemea viongozi wenye matamko yenye kushiria vurugu.
Hotuba ya Rais imekwenda sambamba na wazo la Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama kuandaa tamasha la kuombea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Kwa mujibu wa Msama, lengo la tamasha hilo litakalofanyika Mei, 2025 ni kumlilia Mungu ili taifa la Tanzania lipite salama kwenye kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu na siku yenyewe hadi kuapishwa rais ajaye.
Mbali na Rais Samia kusisitiza hayo kwa viongozi wa dini, pia alisema licha ya kuwepo kwa vyombo vya ulinzi kusimamia wajibu wao lakini viongozi wa dini waendelee kuhubiri amani ya nchi.
Aidha, akizungumza katika Baraza hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert John Chalamila naye aliwahakikishia wananchi wa Dar es Salaam na nchi nzima (kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzake) nchi ipo salama, ina amani hivyo, wafanyabiashara wakubwa hawana sababu ya kuondoa pesa zao benki wakiamini kutakuwa na vurugu.
Chalamila alisema katika mkoa wake (Dar) wamejipanga kwa kusimamia amani na utulivu katika kipindi chote cha kuelekea uchaguzi.