Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Marufuku mpya ya kutotoka nje ya Afghanistan ilitolewa na msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid, akisema zuio hilo linalenga kuwakinga waafghanistan na ugumu wa maisha wakiwa nje ya taifa hilo.
Uhamishwaji wa waafghanistan ulioandaliwa na mashirika ya kibinadamu au mataifa mengine umezuiliwa,na familia ambazo zinahitaji kuondoka kwa mbinu zao, zinahitaji kuwa na sababu muhimu tofauti na hivyo huzuiwa na mamlaka ya uhamiaji.
Msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid ameuambia mkutanbo wa wanahabari kuwa uamuzi wa kupiga marufuku raia kuondoka ulikuja kutokana na Taliban kupokea taarifa za maelfu ya Waafghanistan wanaoishi katika hali mbaya nje ya nchi.
Ameongeza kwamba serikali ina jukumu la kuwalinda wananchi hivyo uhamishwaji utasitishwa hadi watapopata uhakika maisha yao hayapo kwenye hatari.
Vikwazo hivyo vipya vya usafiri vinaleta wasiwasi kwa makumi ya maelfu ya Waafghanistan ambao wameahidiwa hifadhi nje ya nchi baada ya kufanya kazi na vikosi vya kigeni vilivyoongozwa na Marekani au mashirika mengine ya Magharibi wakati wa uasi wa Taliban wa miaka 20.