carbohydates
Senior Member
- Oct 13, 2026
- 197
- 391
Serikali ya Gabon imeondoa marufuku ya mitandao ya kijamii iliyodumu kwa miezi 8, kufuatia ukosoaji kutoka kwa Wananchi na upinzani.
Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano (HAC), Jean-Claude Franck Mendome, amesema uamuzi huo wa Oktoba 24, 2026 unarejesha huduma za Facebook, TikTok, YouTube na Instagram, zilizositishwa Februari 17, 2026.
HAC ilihalalisha marufuku hiyo kwa madai kuwa maudhui ya mtandaoni yalichochea migogoro na migawanyiko katika jamii. Hata hivyo, upinzani ulipinga hatua hiyo, ukiitaja kuwa matumizi mabaya ya madaraka.
Wakati wa marufuku hiyo, baadhi ya wananchi walitumia teknolojia ya VPN kukwepa vizuizi. Kampuni ya Proton iliripoti ongezeko la asilimia 60,000 la upakuaji wa programu yake siku moja baada ya marufuku kuanza.
HAC imesema inashirikiana na Meta, TikTok na YouTube kuboresha usimamizi wa maudhui. Serikali pia inawataka watumiaji kutoa taarifa rasmi za utambulisho wao.
Marufuku hiyo ilitekelezwa wakati Rais Brice Oligui Nguema akikabiliwa na malalamiko ya wananchi kuhusu gharama za maisha, ukosefu wa ajira na huduma duni za maji na umeme.
Hali hiyo ilisababisha migomo ya walimu na watumishi wengine wa umma waliokuwa wakidai kuboreshwa kwa mishahara na mazingira ya kazi. Katika mazingira hayo, wakosoaji waliitaja marufuku ya mitandao ya kijamii kuwa hatua ya kudhibiti ukosoaji wa serikali na kubana uhuru wa kujieleza.
Nguema aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 2023 yaliyomaliza utawala wa familia ya Bongo uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 na kuchaguliwa kuwa Rais Aprili 2025
Ingawa aliingia madarakani huku kukiwa na matumaini ya mageuzi ya kisiasa na kurejeshwa kwa utawala wa kidemokrasia, hatua za serikali yake dhidi ya wakosoaji zimeibua maswali kuhusu utekelezaji wa ahadi hizo.
Chanzo : Jambo Tv, Benini web TV