Nchi ya Dominican ndio nchi pekee duniani inayomruhusu mtu kutoa talaka bila kumpa taarifa mwenzi wake

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
238
659
Mwaka 1994, Mwamba wa kuitwa Gabriel alikutana na mrembo Christina katika party moja huko jijini New York, Marekani.

Walipendana na wakaamua kuoana, ingawa Gabriel alimzidi umri christina kwa miaka 30. Hata hivyo waliishi kwenye ndoa yenye furaha na upendo wa kila aina.

Miaka 20 baadae, Christina aliletewa documents za malipo ya kodi ya nyumba yao waliyopangisha huko Manhattan. Cha kushangaza jina lake halikwepo kwenye zile documents. Kwa mshangao mkubwa, christina alimwajiri mwanasheria ili achunguze lile jambo.

Baada ya uchunguzi, mwanasheria alikuja na jibu kuwa, Mwenzi wake Gabriel alishampa talaka miaka 20 iliyopita bila yeye kujua. Ilikuwa hivi, Miezi minne baada ya ndoa yao, Gabriel na Christina walienda nchi ya Dominican Republic kula maisha.

Nchi ya Dominican ndio nchi pekee duniani inayomruhusu mtu kutoa talaka bila kumpa taarifa mwenzi wake. Gabriel alijua fika kuwa Christina hamkupenda kwa dhati ila alikubali kuolewa nae ili apate mali, hivyo alimpa talaka mapema ili baadae asimje kudai mali wakati atakapoomba talaka.

Kwahiyo, waliporudi Marekani, Gabriel aliendelea kuishi na Christina kwa miaka 20 kama mtalaka wake bila Christina kujua.

Didas Tumaini

Polish_20240516_210812750.jpg
 
Sasa unaisha vipi na mtalaka kwa miaka 20? Sheria za huko Dominican republic zinasemaje hapo?
 
Back
Top Bottom