Takwimu zinavyoikaanga CCM uchaguzi 2015

Takwimu zinavyoikaanga CCM uchaguzi 2015

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,312
Reaction score
55,971
CCM ina wachama milioni 6.

Mwaka huu watanzania waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 23.

Tangu uhuru wastani wa wapiga kura niasilimia 75,japo mwaka 2010 waliopiga kura ni asilimia 42.6.

Mwaka huu huenda wapiga kurawakafikia asilimia 80 kutokana na mwamko uliopo ina maana watu milioni 18.4 watapiga kura kulinganisaha na wapiga kura milioni 8.6 wa mwaka 2010
kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 nusu ya watanzania ni vijana kuanzia miaka 15-35

Kama watu milioni 18 watapiga kura na CCM Kuzoa kura zote milioni 6 za wanachama wake na kuambulia kura milioni 2 za wasiowanachama maana yake itapata kura milioni 8 kura zilizobaki milioni kumi zikienda upinzani CCM itakuwa katika wakati mgumu sana.

vijana wengi ambao ndio wamejiandikisha kupiga kura na ambao kwa idadindio wengi wanaonekana ndio wapenda mabadiliko kuliko watu wazima wengi wao hawajawahi kupiga kura wanataka kujua kule kwenye chumba cha kupigia kura kunafananaje.

Takwimu hizi ndio zinafanya taasisi nyingi za utafiti kama Redet na synovate kuamua kukaa kimya kuogopa lawama kuwa zilisaidia upinzani ila hali ni mbaya kwa CCM kitakwimu.
 
Mara baada ya uchaguzi utakutana na magufuli anagongea fegi
 
Ukawa tume tume itawaangusha muwe makini sana. Kwani mnajua tume inawajibika kwani?
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu sana kuutabiri. Ingawa ni kweli kwamba wengi waliojiandikisha ni vijana ambao ndiyo wengi zaidi wanataka mabadiliko mpaka ya chama. Ila ni ukweli usiopingika vijana hawa wengi wamejiandikisha kwaajili ya matumizi mbadala wa kile kitambulisho cha kupigia kura, mfano: Kwenye kusajili line za simu, kuombea dhamana na hata kwa shughuli nyingi katika serikali za mtaa kinakubalika. Uzoefu unaonyesha Vijana siyo wapiga kura, huwa wanadhani ukishashangilia kule uwanjani na kusukuma magari basi ndiyo ushindi tayari, wengi hawawezi kuacha shughuli zao za kubangaiza wakaenda kupiga kura. Wapiga kura wengi ni kinamama na wazee kwa uchache wao.

Ugumu katika mwaka huu, ni kama kweli vijana watakwenda kweli kupiga kura? Kama kweli watakwenda, basi lolote linawezekana kutokea. Pia kitu kingine ambacho chama chetu kilifanya makosa ni kutofanya kampeni ya kuhamasisha watu kujiandikisha. Nafikiri wapinzani walifanya assignment yao vizuri katika hili, maana tuliwashuhudia wakiamasisha na kuwashawishi watu wakajiandikishe ili waje wawachague. Ingawa sasa hivi hawa wapinzani hawahamasishi sana watu wakapige kura, ila hata chama chetu nacho kipo kimya kwenye hili, naona kimefanya makusudi ili waende kina mama na wazee ambao wengi wao huchagua CCM. Ila ni kweli mpaka sasa chochote kinaweza kutokea hata kama kura zikipigwa leo.

Mwisho napenda kuchukua nafasi hii kwa kuwaomba wote kwa umoja wetu na imani zetu, tuliombee taifa letu la Tanzania ili lituvushe salama hasa kwenye uchaguzi wa mwaka huu ambapo kuna kila aina ya mbwembwe na ushabiki. Mungu ibariki Tanzania.
 
Ukawa tume tume itawaangusha muwe makini sana. Kwani mnajua tume inawajibika kwani?

UKAWA imejipanga vyema, matokeo ya kila kata na kila jimbo yatawekwa hadharani ili kila mtu ajionee mwenyewe kabla hata tume haijayatangaza. Sasa kama kila mtanzania ataona kura milioni 12 za Lowassa dhidi ya milioni tano za Magufuli, nani atamtangaza Magufuli kuwa rais, na nini itakuwa madhara yake. Eeeh Mungu wape CCM moyo wa kukubali matokeo na kwenda zao kuzimu
 
Tanganyika (Tanzania Bara) kuna majimbo ya uchaguzi 215. katika kura za maoni za ccm mgombea aliye pata kura nyingi kuliko wote Tanganyika ni Prof.Sospeter Muhongo ambaye alipata kura takribani 38000. ukichukuwa kwamba idadi hiyo ndo ya wanachama hai wa ccm na tuchukulie kwa wastani kila jimbo lina wanachama 38000 basi idadi ya wanacch haiwezi zidi 38000 x 215 = 8170000. hivyo idadi ya wanachama wa ccm kwa kadilio la juu ni 8,170,000. kwa kadilio la chini inaweza kuwa 215 x 27000 =5,805,000. hapa ni bila kuweka zile kata za nchi ya Zanzibar ambapo idadi haiwezi zidi 300,000
 
Hamuwezi kututisha na hizo takwimu pori

Hakuna anayewatishia watu wazima Nyau, Bali takwimu ni sayansi, ni ukweli and facts are ONE, indivisible and very very sturbon! Mdharau mwiba huota tende! Be warned
 
Back
Top Bottom