Takwimu za swali la kipimajoto la ITV

Takwimu za swali la kipimajoto la ITV

GIBA KB

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
367
Reaction score
111
Kituo cha televisheni cha ITV huwa kina mtindo wa kuuliza swali moja kila siku baada ya taarifa ya habari.Swali hilo linawataka watanzania kuchangia kwa jibu la NDIYO au HAPANA.Swali la jana lilihoji"Wajumbe wa bunge la katiba kususia vikao vya bunge hilo,Je,watanzania wategemee katiba mpya nzuri?"
Takwimu:70% wamesema NDIYO 28% wamesema HAPANA na 2% wamesema hawajui.
Hii inaonesha waTanzania wengi 70% wana imani na ukawa na wanaamini wanapigania maslahi yao
 
kama ni ndiyo ina maanisha watanzania hawana imani na kikundi cha UKAWA. Na ina maana watanzania wana amimi pamoja na kutoka kwao bado tutapata katiba !
 
Mkuu watu waliowengi wanahitaji Katiba iliyo na mfumo wa serikali tatu,hivyo wako tayari kumuunga mkono yeyote anayetetea maoni yao hata kama ni ccm. Tatizo kubwa ccm hawajifunzi kutokana na tafiti za namna hii, wao wamebaki kushikilia tu serikali mbili bila kujali wanao hitaji serikali mbili hawafiki hata mia

BACK TANGANYIKA
 
kama ni ndiyo ina maanisha watanzania hawana imani na kikundi cha UKAWA. Na ina maana watanzania wana amimi pamoja na kutoka kwao bado tutapata katiba !

Ndoto,nadhani ww na hao unaowasemea mna utaalamu mdogo wa sheria
 
Kituo cha televisheni cha ITV huwa kina mtindo wa kuuliza swali moja kila siku baada ya taarifa ya habari.Swali hilo linawataka watanzania kuchangia kwa jibu la NDIYO au HAPANA.Swali la jana lilihoji"Wajumbe wa bunge la katiba kususia vikao vya bunge hilo,Je,watanzania wategemee katiba mpya nzuri?"
Takwimu:70% wamesema NDIYO 28% wamesema HAPANA na 2% wamesema hawajui.
Hii inaonesha waTanzania wengi 70% wana imani na ukawa na wanaamini wanapigania maslahi yao

Mkuu mbona unajichanganya..soma vizuri takwimu zako na conclusion yako havishabihiyani kabisa...umeandikia kwa hisia na mapenzi bila kufikiri...!!
 
Acheni kujichanganyaa 70% ni watu wanaamini UKAWA WAPO SAHIHI NA WANALENGO LA KUETEA KATIBA YA WANANCHI WALIO WENGI. Na katiba inayotaka serikali tatu. HATA KISWAHILI KINAWASHINDA!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
ameandika vibaya bwana, iliuliza ivi-kitendo cha ukawa kususia bunge la katiba,ndio muafaka Wa kupata katiba mpya, na 70% wakasema ndio
 
Kipima joto si ndio hata ukisema sijui pia ni jibu na unapewa asilimia za kutosha?..kweli wenye akili timamu bado wanafuatilia ule utoto?
 
Hicho kipima joto ni vapour tu na maswali yao ya bushi/chekechea
 
Usifuate vipima joto vya ITV. Hawana tofauti na SYNOVATE. Data za kupikwa hazifanani na field
Sent from my RM-846_im_mea3_286 using Tapatalk
 
Usipende kupotoshapotosha mambo banaaaa!!! Swali ni hili hapa: SWALI LA KIPIMAJOTO:"KUSUSIA BUNGE MAALUM LA KATIBA. JE NDIO NJIA SAHIHI ZAIDI YA KUWAPATIA WATANZANIA KATIBA BORA"?
Takwimu:70% wamesema NDIYO 28% wamesema HAPANA na 2% wamesema hawajui.
Hii inaonesha waTanzania wengi 70% wana imani na ukawa na wanaamini wanapigania maslahi yao.

kama ni ndiyo ina maanisha watanzania hawana imani na kikundi cha UKAWA. Na ina maana watanzania wana amimi pamoja na kutoka kwao bado tutapata katiba !
 
Mkuu watu waliowengi wanahitaji Katiba iliyo na mfumo wa serikali tatu,hivyo wako tayari kumuunga mkono yeyote anayetetea maoni yao hata kama ni ccm. Tatizo kubwa ccm hawajifunzi kutokana na tafiti za namna hii, wao wamebaki kushikilia tu serikali mbili bila kujali wanao hitaji serikali mbili hawafiki hata mia

BACK TANGANYIKA
Duh... hapo umeniacha hoi.

Unaposema wanaotaka serikali 2 hawafiki 100, umepigaje hesabu?

Unataka kuniambia ukijumlisha akina JK, Wassira, Mwigulu Nchemba, Kinana, Nape Nnauye, William Lukuvi, Dr Mohamed Shein, Ptrofesa Shivji, Dr Benson Bana, wabunge wa CCM walioko kwenye bunge la katiba, plus wapambe wao na familia zao, idadi hiyo bado haitafika 100!!
 
Back
Top Bottom