Takwimu za Deni la Taifa kwa sasa

Takwimu za Deni la Taifa kwa sasa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,353
KWA TAKWIMU HIZI ZA DENI LA TAIFA HAKIKA TUNAANGAMIA.

01. Awamu ya kwanza chini ya Mwl. Nyerere alieongoza kwa miaka zaidi ya miaka 20.
-Deni la Taifa lilipotoka mwaka 1979 mara tu baada ya vita ya Kagera lilikuwa Trilioni 3.

02. Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza kwa miaka 10.
-Deni la Taifa lilipanda kutoka Trilioni 3 hadi kufikia Trilioni 18. Hii inamaana kuwa, Mzee Mwinyi alikopa fedha kiasi cha Trilioni 15 pekee ndani ya awamu zote mbili.

03. Awamu ya tatu ya Mhe. Benjamin Mkapa aliyeongoza kwa miaka 10.
-Mzee Mkapa alipoingia alikuta deni ni Trilioni 18. Mzee Mkapa akafanya jitihada za kupunguza deni hilo na kufanikiwa kulipunguza hadi kufikia Trilioni 10.
Mpaka anaondoka madarakani uchumi ulikuwa unakuwa kwa 6.7%
Kwa neno moja tu tunaweza kusema, Mzee Mkapa alikuwa ni "Mpiganaji wa uchumi".

04. Awamu ya nne chini Mhe. Jakaya Kikwete alieongoza miaka 10.
-Ameingi amekuta deni la Taifa ni Trillion 10. Lakini katika kukopa kwake mpaka anamaliza muda wake wa uongozi (awamu zote mbili) ameacha deni la Trilioni 35. Maana yake kwa miaka yote 10 amekopa kiasi cha Trilioni 25.

05. Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ambae mpaka sasa ana miaka minne (4) ya uongozi wake ikiwa hajakamilisha hata awamu moja ya miaka mitano.
-Ameingia madarakani amekuta deni la Taifa lililoachwa ni Mzee Kikwete ni Trilioni 35.
-Mpaka kufikia mwezi huu wa January mwaka 2019, deni la Taifa limefika Trilioni 61.8
*Kwa lugha rahisi ni kwamba Rais Magufuli amekopa Trilioni 26 ndani ya miaka minne (4) tu.*
Hivyo basi, ni dhahiri kusema kuwa, Rais Magufuli ndiye Rais pekee kati ya marais wote waliopita, aliyekopa pesa nyingi sana kwa muda mfupi sana.

Tuna wakati mgumu sana kama Taifa. Na hapa tulipofika ni hatari zaidi katika nchi hii ambayo watu wake wengi ni Wakulima na Wafanyakazi.
Ninajiuliza ikiwa kiasi hicho ni cha miaka minne tu, je, Rais huyu akipewa awamu ya pili tutaangukia wapi?

1567088792948.jpeg
 
Mimi nnaulizia Matokeo (Faida) ya ukopwaji huu mkubwa Pesa ambazo nntakuja kuzilipa ,ni kitu gani tumepata kama Taifa !!?
 
Chato International Airport
Bugiri Chato National Park
 
Hatuwezi kuwa na deni hilo wakati tunajenga miradi mikubwa kama SGR, Stigula goji, ndege tumenunua kwa cash yote hiyo ni kwa pesa yetu ya ndani tuliyoibana toka kwa nafisadi. Rais haendi nje tumebana matumizi sana. Sasa deni linaongezeka kutokana na nini?! Tafadhali rais itisha mkutano ikulu TBC live kukanusha uongo wa mabeberu hawa
 
Tuna wakati mgumu sana kama Taifa. Na hapa tulipofika ni hatari zaidi katika nchi hii ambayo watu wake wengi ni Wakulima na Wafanyakazi.
Ninajiuliza ikiwa kiasi hicho ni cha miaka minne tu, je, Rais huyu akipewa awamu ya pili tutaangukia wapi?

Mimi nnaulizia Matokeo (Faida) ya ukopwaji huu mkubwa Pesa ambazo nntakuja kuzilipa ,ni kitu gani tumepata kama Taifa !!?
Huoni Chato inavojengeka?
Huoni ndege znavyopishana angani?
Huoni Stiglaz goji?
Huoni standadi geji?

Yaani huoni ivo vyote chief,

Au wee unamtindio wa Macho?
 
Parojo za akina bashiru, polepole na maccm mengine
Ukweli nikwamba tupo hovyohovyo kiuchumi, kielimu, afya, democracy hata kijamii.....very poor cohesion between citizens.
Yaani hapa ndipo ninapoamini kwamba hawa vijana wa Lumumba wanaotoa mapambio kila siku na sasa kaka yao Pascal Mayalla kaamua kujiunga nao kuna chochote kitu wanakipata..maana kwa akili ya kawaida huwezi kuona mambo yanakwenda hovyo na ukasifu kwamba yanakwenda vizuri ni ukichaa wa hali ya juu kufanya hivyo
 
KWA TAKWIMU HIZI ZA DENI LA TAIFA HAKIKA TUNAANGAMIA.

01. Awamu ya kwanza chini ya Mwl. Nyerere alieongoza kwa miaka zaidi ya miaka 20.
-Deni la Taifa lilipotoka mwaka 1979 mara tu baada ya vita ya Kagera lilikuwa Trilioni 3.

02. Awamu ya pili chini ya Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza kwa miaka 10.
-Deni la Taifa lilipanda kutoka Trilioni 3 hadi kufikia Trilioni 18. Hii inamaana kuwa, Mzee Mwinyi alikopa fedha kiasi cha Trilioni 15 pekee ndani ya awamu zote mbili.

03. Awamu ya tatu ya Mhe. Benjamin Mkapa aliyeongoza kwa miaka 10.
-Mzee Mkapa alipoingia alikuta deni ni Trilioni 18. Mzee Mkapa akafanya jitihada za kupunguza deni hilo na kufanikiwa kulipunguza hadi kufikia Trilioni 10.
Mpaka anaondoka madarakani uchumi ulikuwa unakuwa kwa 6.7%
Kwa neno moja tu tunaweza kusema, Mzee Mkapa alikuwa ni "Mpiganaji wa uchumi".

04. Awamu ya nne chini Mhe. Jakaya Kikwete alieongoza miaka 10.
-Ameingi amekuta deni la Taifa ni Trillion 10. Lakini katika kukopa kwake mpaka anamaliza muda wake wa uongozi (awamu zote mbili) ameacha deni la Trilioni 35. Maana yake kwa miaka yote 10 amekopa kiasi cha Trilioni 25.

05. Awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ambae mpaka sasa ana miaka minne (4) ya uongozi wake ikiwa hajakamilisha hata awamu moja ya miaka mitano.
-Ameingia madarakani amekuta deni la Taifa lililoachwa ni Mzee Kikwete ni Trilioni 35.
-Mpaka kufikia mwezi huu wa January mwaka 2019, deni la Taifa limefika Trilioni 61.8
*Kwa lugha rahisi ni kwamba Rais Magufuli amekopa Trilioni 26 ndani ya miaka minne (4) tu.*
Hivyo basi, ni dhahiri kusema kuwa, Rais Magufuli ndiye Rais pekee kati ya marais wote waliopita, aliyekopa pesa nyingi sana kwa muda mfupi sana.

Tuna wakati mgumu sana kama Taifa. Na hapa tulipofika ni hatari zaidi katika nchi hii ambayo watu wake wengi ni Wakulima na Wafanyakazi.
Ninajiuliza ikiwa kiasi hicho ni cha miaka minne tu, je, Rais huyu akipewa awamu ya pili tutaangukia wapi?

View attachment 1192870
Kuna usemi siku hizi. Wanasema deni himilivu.
They don't give it a damn. Wakati wa kulipa hawatakuwepo.

Note: kupungua kwa deni wakati wa Mkapa kulitokana na juhudi za miaka mingi walizo fanya watu mashuhuri kama Mwl Nyerere ili kuzifutia madeni nchi maskini. Kwa hiyo sehemu kubwa hatukulipa per se, madeni mengi yalifutwa.

Sasa awamu hii inakopa kama vile hakuna kesho. Ipo hatari Rais ajaye hataweza kukopa zaidi ya kulipa mideni atakayoikuta.
 
Back
Top Bottom