Takwimu na siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu na siasa za Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ntemi Kazwile, Aug 9, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikijiuliza bila majibu kuhusu usahihi na ukweli wa takwimu zinazotolewa na taasisi zetu za umma. Nikiwa mdau katika soko la kuuza na kununua fedha za kigeni, nimeshindwa kuelewa ni vipi BOT wanakokotoa viwango vya kuuza na kunulia pesa za kigeni hasa hasa dollar ya Marekani.

  Kwa mfano leo tarehe 9 August 2010, BOT wanasema dolla moja imenunuliwa na mabenki kwa wastani wa Tshs 1,377.55 na kuuzwa kwa Tshs 1,405.46 niki-assume walitumia takwimu za soko la mwisho (kabla ya 09.08.2010) ambalo ni Ijumaa 06.08.2010 mabenki makubwa nchini yalitoa viwango vifuatavyo:
  • CRDB: kununua 1,460 kuuza 1,570
  • NBC: kununua 1,432.25 kuuza 1,552.25
  • CBA: kununua 1,510 kuuza 1,530 (9August 2010)
  • BOA: kununua 1,460 kuuza 1,533 (9August 2010)
  Ukiangalia kwa makini utaona hakuna uwiano wa takwimu hizi na zile zinazotolewa na Benki Kuu (BOT) na hivyo kupoteza mantiki yote yakuwa na takwimu kama hizo kwenye tovuti yao.
  Takwimu nyingi pia huwa hazifanani na ukweli uliopo, mfano ukuaji wa uchumi, maendeleo katika elimu, n.k

  Swali langu---- Je takwimu hizi huchakachuliwa ili kukidhi matakwa ya wanasiasa??? Kama sivyo naomba msaada kwa anayejua ni vipi BOT hukokotoa viwango vya kubadilishia pesa.

  Naomba kuwasilisha
   
Loading...