TAKUKURU yakamilisha uchunguzi Tanesco

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
[h=2][/h] Jumanne, Septemba 25, 2012 06:47 Na Arodia Peter, Dar es Salaam

hosea.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hosea

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseah, amesema uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), umekamilika.
Hata hivyo, amesema uchunguzi huo hauwezi kutangazwa hadharani, lakini tayari umekabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.

Dk. Hosea, aliyasema hayo jana katika kongamano la mwaka la wadau wa kuzuia na kupambana na rushwa nchini, lililofanyika katika Ukumbi wa Blue Peal, Ubungo, Dar es Salaam.

Dk. Hosea, alisema kwa mujibu wa sheria ya TAKUKURU, kifungu cha 37, jambo lolote linalochunguzwa haliwezi kuwekwa hadharani na taasisi hiyo badala yake taarifa hizo zinapelekwa kwa mamlaka husika.

Alisema uchunguzi huo unahusu watendaji kadhaa wa TANESCO, ambao walitajwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika Bunge la Bajeti mwaka huu.

Katika Bunge hilo, Profesa Muhongo, alizungumzia tuhuma mbalimbali zinazofanywa na watumishi hao, ikiwamo nguzo za umeme zinazozalishwa Tanzania ambazo baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu hugonga mihuri nguzo hizo zikionyesha kuwa, zinaingizwa nchini kutoka Afrika Kusini kupitia Mombasa Kenya.

Tuhuma nyingine ni uchakachuaji na udanganyifu katika sekta ya uagizaji vipuri kutoka nje ya nchi, ambapo kuna wakati iliagizwa kilo 50 za misumari ikionyesha ni vipuri kutoka nchini Uingereza.

Pia Profesa Muhongo alisema, baadhi ya wabunge wanafanya biashara na TANESCO jambo ambalo alisema haliwezi kukubalika na akawataka wabunge hao kuacha tabia hiyo.

Pamoja na Dk. Hosea kuyasema hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi William Mhando, amesimamishwa kazi na Bodi ya shirika hilo kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Katika mazungumzo yake, Dk. Hoseah alizungumzia mafanikio ya nchi ya Rwanda katika mapambano dhidi ya rushwa na kusema Tanzania haiwezi kujilinganisha na Rwanda, kwa sababu ya mazingira ya nchi hizo mbili kuwa tofauti.

“Staili ya uongozi wa Rwanda na Tanzania ni tofauti sana, uhuru wa mawazo nao ni tofauti sana japokuwa ni kweli mambo yamebadilika sana. Kule Rwanda, Rais Paul Kagame akiagiza barabara ijengwe kwa wiki tatu inajengwa.

“Pia kule wana utaratibu, kijana yeyote anayeanza kazi au aliyemaliza Chuo Kikuu kabla ya kuajiriwa anapelekwa katika kozi maalum ya kujifunza uzalendo, yaani wana JKT yao.

“Hii imesaidia sana kujenga utaifa wao, siwezi kusema staili hiyo tuifuate, lakini imewasaidia sana,” alisema Dk. Hoseah.

Wakati huo huo, alisema katika kipindi cha Januari mpaka Julai mwaka huu, taasisi yake imeokoa Sh bilioni 7 kutokana na mishahara hewa katika sekta ya walimu pekee na kurudishwa hazina.

Kuhusu fedha zinazodaiwa kuhifadhiwa nchini Uswis na baadhi ya vigogo hapa nchini, alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tayari amepeleka maombi katika benki zilizopo Uswis akiomba kupatiwa taarifa na majina ya wanaotajwa katika sakata hilo.

Kuhusu taarifa za baadhi ya watumishi wanaoishi maisha yasiyolingana na vipato vyao, TAKUKURU inaweza kuchunguza mali hizo kwa mujibu wa sheria.

Naye, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, aliyekuwapo katika mkutano huo, alishauri taasisi hiyo, kuhamasisha namna ya kupambana na rushwa kwa kutumia maandamano, ili kuyapa msisimko mpya.

[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
"Staili ya uongozi wa Rwanda na Tanzania ni tofauti sana, uhuru wa mawazo nao ni tofauti sana japokuwa ni kweli mambo yamebadilika sana. Kule Rwanda, Rais Paul Kagame akiagiza barabara ijengwe kwa wiki tatu inajengwa.

Nahisi alikuwa anapigia msitari kauli ya Mnyika kuwa tumefika hapa tulipo kwa sababu ya ......................
 
TAKUKURU nao wanapaswa kuchunguzwa maana ndiyo muhimili wa rushwa nchini. Kimsingi kwangu TAKUKURU ni Taasisi ya Kuimarisha na kutetea Rushwa finish.
 
Takukuru is paper Tiger kitendo cha mkurugezi kufananisha Rwanda na Tanzania ni kumaanisha wazi kuwa Mfumo
wa Tanzania hauwezi kuzuia rushwa. mtu anaitwa jina kubwa la mkurugezi wa takukuru lakini hana mamlaka yeyote
yuko pale kwa ajili ya mshahara tu. chombo hiki ilibidi kifutwe mara baada ya kuisafisha Richmond na kamati ya
mwakyembe kuja kugundua madudu kibao ambayo chombo makini kisingeweza kutoyaona.
 
Ni TAKUKURUPUKA
Yaani mnachunguza halafu inabaki kuwa siri!!!!
 
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Dkt. Edward Hoseah, amesema uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), umekamilika.

Hata hivyo, amesema uchunguzi huo hauwezi kutangazwa hadharani, lakini tayari umekabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika.

Dkt. Hosea, aliyasema hayo jana katika kongamano la mwaka la wadau wa kuzuia na kupambana na rushwa nchini, lililofanyika katika Ukumbi wa Blue Peal, Ubungo, Dar es Salaam.

Dkt. Hosea, alisema kwa mujibu wa sheria ya TAKUKURU, kifungu cha 37, jambo lolote linalochunguzwa haliwezi kuwekwa hadharani na taasisi hiyo badala yake taarifa hizo zinapelekwa kwa mamlaka husika.

Alisema uchunguzi huo unahusu watendaji kadhaa wa TANESCO, ambao walitajwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika Bunge la Bajeti mwaka huu.

Katika Bunge hilo, Profesa Muhongo, alizungumzia tuhuma mbalimbali zinazofanywa na watumishi hao, ikiwamo nguzo za umeme zinazozalishwa Tanzania ambazo baadhi ya watumishi wasiokuwa waadilifu hugonga mihuri nguzo hizo zikionyesha kuwa, zinaingizwa nchini kutoka Afrika Kusini kupitia Mombasa Kenya.

Tuhuma nyingine ni uchakachuaji na udanganyifu katika sekta ya uagizaji vipuri kutoka nje ya nchi, ambapo kuna wakati iliagizwa kilo 50 za misumari ikionyesha ni vipuri kutoka nchini Uingereza.

Pia Profesa Muhongo alisema, baadhi ya wabunge wanafanya biashara na TANESCO jambo ambalo alisema haliwezi kukubalika na akawataka wabunge hao kuacha tabia hiyo.

Pamoja na Dkt. Hosea kuyasema hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Mhandisi William Mhando, amesimamishwa kazi na Bodi ya shirika hilo kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili, ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.

Katika mazungumzo yake, Dkt. Hoseah alizungumzia mafanikio ya nchi ya Rwanda katika mapambano dhidi ya rushwa na kusema Tanzania haiwezi kujilinganisha na Rwanda, kwa sababu ya mazingira ya nchi hizo mbili kuwa tofauti.

"Staili ya uongozi wa Rwanda na Tanzania ni tofauti sana, uhuru wa mawazo nao ni tofauti sana japokuwa ni kweli mambo yamebadilika sana. Kule Rwanda, Rais Paul Kagame akiagiza barabara ijengwe kwa wiki tatu inajengwa.

"Pia kule wana utaratibu, kijana yeyote anayeanza kazi au aliyemaliza Chuo Kikuu kabla ya kuajiriwa anapelekwa katika kozi maalum ya kujifunza uzalendo, yaani wana JKT yao. Hii imesaidia sana kujenga utaifa wao, siwezi kusema staili hiyo tuifuate, lakini imewasaidia sana," alisema Dk. Hoseah.

Wakati huo huo, alisema katika kipindi cha Januari mpaka Julai mwaka huu, taasisi yake imeokoa Sh bilioni 7 kutokana na mishahara hewa katika sekta ya walimu pekee na kurudishwa hazina.

Kuhusu fedha zinazodaiwa kuhifadhiwa nchini Uswis na baadhi ya vigogo hapa nchini, alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tayari amepeleka maombi katika benki zilizopo Uswis akiomba kupatiwa taarifa na majina ya wanaotajwa katika hilo.

Kuhusu taarifa za baadhi ya watumishi wanaoishi maisha yasiyolingana na vipato vyao, TAKUKURU inaweza kuchunguza mali hizo kwa mujibu wa sheria.

via
MTANZANIA

Source:
Ripoti ya uchunguzi wa TAKUKURU kuhusu TANESCO yakamilika; yakabidhiwa - wavuti.com
 
Back
Top Bottom