Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Sep 13, 2008.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2008
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Takukuru yaenguliwa Timu ya EPA
  Na Mwandishi wetu

  BAADA ya Timu Maalum ya Rais ya kuchunguza wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania (EPA) kukabidhi taarifa yake kwa Rais Jakaya Kikwete mwezi uliopita, taasisi mojawapo kati ya tatu zilizohusika imeenguliwa.


  Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imeengiliwa kwa agizo ‘kutoka juu’.


  Hatua hiyo imechukuliwa na serikali ngazi ya juu kunatokana na mchango wa tasisi anayoiwakili mjumbe huyo kuonekana mdogo.


  Timu hiyo inatakiwa kukamilisha kazi yake mwishoni mwa mwezi ujao kama ilivyoelekezwa na Rais Kikwete.


  Kazi zilizobaki kwa timu hiyo ni pamoja na kusimamia urejeshwaji wa sh11 bilioni kutoka kwa makampuni yaliyohusika na ubadhilifu huo ndani ya Benki Kuu.


  Pamoja na kubakia na kazi hiyo, timu hiyo imebaki na jukumu la kusimamia upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia serikali kupata taarifa za makampuni ambayo yameficha mali zake nje ya nchi kwa kutumia ushirikiano wa polisi wa kimataifa ‘Interpol’.


  Taarifa za ndani ya serikali zinaonyesha kuwa Takukuru wameondoshwa katika timu iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika Mkuu wa jeshi la Polisi nchini, Said Mwema pamoja na Mkurugenzi wa Takukuru, Edward Hosea.


  Taasisi hiyo imeondolewa, haijajulikana bayana kama ni Rais Jakaya Kikwete ndiye alitoa maamuzi hayo.


  “Kimsingi ni kama Takukuru iliondoshwa katika mchakato huu katika hatua za mwisho, wakati timu ilikuwa inaandaa ripoti kwa ajili ya kuifikisha kwa Rais kama ilivyokuwa imeelekezwa,” kilisema chanzo chetu.


  Aidha chanzo hicho kilisema kitendo cha kuondoshwa kwa taasisi hiyo nyeti pengine inatokana na kazi za msingi za kamati hiyo kumalizika na kubakia majukumu ya kuwapeleka watuhumiwa mahakamani pamoja na kuwafuatilia walioficha mali nje ya nchi.


  Chanzo chetu kinasema lengo kubwa la kuwahusisha Takukuru ilikuwa ni kutumia uwezo wao wa kiuchunguzi kuisaidia timu hiyo kuharakisha mambo zaidi.


  Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa huenda Takukuru wameondolewa katika timu hiyo kutokana na kuvuja kwa kazi iliyokuwa ikifanyika.  “Baadhi ya siri za timu hiyo ilikuwa inaoongozwa na mwanasheria mkuu wa serikali zilikuwa zinavuja kila baada ya kikao, hivyo kuipa timu wakati mgumu wa kuendelea na kazi waliyopewa,” alisema.


  Pamoja na fununu hizo, lakini pia habari za uhakika zinasema hata mipango ya kuwasiliana na Interpol zimekuwa zinafanywa na watu wawili tu, ukimwondoa Hosea.  Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma, Rais Kikwete alisema timu ilikuwa imekusanya Sh 53,738,835,392


  Aidha Rais Kikwete alisema timu hiyo pia iliwabana baadhi ya watuhumiwa na kwamba wapo ambao wamekubaliana mpaka hadi Oktoba 31 mwaka huu wawe wameshalipa.


  Hali hiyo inaonyesha kuwa tayari kazi ambayo ilitakiwa kufanywa na Takukuru kwa kushirikiana na vyombo vingine ilikuwa imekamilika na kwamba mpaka hapo timu ilipofikia wanaweza kufanya kazi bila Takukuru.
  Source: Mwananchi
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Sep 13, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Hivi vichwa vya habari ni special kuuza magazeti, title inavutia na conclusion inaonyesha there was no anything bad for TAKUKURU kuondolewa! lakini katika paragraph za mwanzo mwandishi anakuwa kama eti hajui reasons za TAKUKURU kuondolewa. Mbaya zaidi inaonekana eti tuamini labda Kikwete amewaondoa TAKUKURU!

  Tutasema vingi au mengi ya kujipa moyo, mata BOT mafisadi wamechukuliwa hatua, Mara Mabadiliko makubwa yatakuja TAKUKURU mara hoo, watapelekwa mahakamani.Enyi watanzania mdanganywao nani atawaaminisha kuwa hakuna kitu chema kitakacholetwa na huyu RAIS? everything he does is just to magnetize society.

  Waberoya

  'Stand still'
   
 3. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ukiwa na crummy press kama hii lazima utaelekea kujenga Taifa la wajinga kwa sababu hakuna anaejua chochote kinachoendelea, hakuna press.
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Maelezo hayo hapo juu yanataka kuonyesha kwamba TAKUKURU hawahusishwi tena kwa kukiuka kiapo ama kuharibu uchunguzi, ama kutokubaliana na uchunguzi unaoendelea au kutokana na hatua ambazo pengine zinaandaliwa kuchukuliwa dhidi ya Dk. Edward Hosea. Hii inataka kuonyesha kwamba Hosea ni mhalifu kuliko hata Elisifa Ngowi ambaye amehusika moja kwa moja katika EPA na maskandali mengine ikiwa ni pamoja na "kumchuna" mamilioni Marehemu Daudi Ballali na wengine kwa kutumia vitisho na ulaghai akitumia kuwapo kwake TISS. Maelezo hayo yanataka kutulazimisha tuone sasa serikali iko makini na inawachukulia hatua watendaji wasio waadilifu.

  TAARIFA ZA KUONDOLEWA TAKUKURU NA YOTE KATIKA AYA HIZO KWA MAONI YANGU NI UPOTOSHAJI WA HALI YA JUU NA WENYE LENGO LA KUTUZUGA. WAKAMATWE WAHUSIKA NA KUPELEKWA MAHAKAMANI.


  Kama kazi ya TAKUKURU kiuchunguzi imekwisha basi kazi iliyobaki ni ya DPP kupeleka mahakamani na kwa upande mwingine kwa polisi kuwasiliana na polisi wa kimataifa, lakini TAKUKURU pia wana mahusiano kiutendaji na taasisi kama hizo za kimataifa kama vile za Uingereza na Uswisi pamoja na India ambazo zina uwezo wa kufuatilia mali na nyendo za wahusika wa EPA na kwa kuwa kazi za kiuchunguzi huwa hazina ukomo, huwezi kuwaambia wachunguzi wa TAKUKURU basi wafungashe virago, hiyo pia si kweli. Pia kuna taarifa za uhakika kwamba ni TAKUKURU pekee waliomhoji Marehemu Ballali kabla hajakwenda Marekani na ni TAKUKURU pekee wanaojua siri ya Kagoda kwa kuwa walichukua doc za CRDB zinazowahusisha vigogo halisi (si Halisi mimi) ambao wanahusika na kampuni ya Kagoda Agricultural kwa hiyo wachunguzi hao bado ni muhimu katika kukamilisha na hatimaye kusimamia ama kuwa mashahidi katika mashitaka dhidi ya wahusika kwa hiyo haiingii akilini kwamba wameenguliwa. HAINA MAANA KABISA.

  MAONI YANGU: Kwa maoni yangu ni kwamba naweza kuamini kwamba sasa huyo mtu wa JUU aliyetoa maelezo, amefanya uamuzi wa kuwasamehe kabisa watuhumiwa wa EPA tena baada ya kikao cha Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM kule Dodoma. Hiyo inaweza kuingia akilini na pengine NDIO UKWELI.

  Hii tena ni mbinu chafu tena zinazolenga kuwaingiza ama kuwatuhumu moja kwa moja TAKUKURU kuwa wanatoa siri na mwandishi kwa udhaifu wakeanatumika kutishia mbubujiko wa habari. Pia habari hii imetokea ndani ya TAKUKURU ukiwa ni ule muendelezo wa mapambano ya kutaka kumuondoa HOSEA na kwa hakika ni katika kuvuruga ushahidi wa EPA na ule wa Ballali ambao TAKUKURU ni taasisi pekee iliyo na ushahidi na maelezo ya kisheria kwani hata timu ya Mwanyika haijaweza kumhoji Ballali na hawajapata nyaraka zote za Kagoda wakati TAKUKURU walizipata hata kabla ya wakaguzi wa kwaza wa Deloite kugundua siri za wizi wa EPA.

  Mwandishi anatuambia 'watu' wawili, anataka kutuambia Mwanyika na Saidi Mwema, jambo ambalo si kweli. Kwanza hata katika timu ya Mwanyika, kiutendaji Mwanyika na Mwema hawakuwa wanafanya kazi wao moja kwa moja. Kazi zilikuwa zinafanywa na kina Manumba, Kasala, Ubisimbali, Samali, Huseni, Valentino, Kisai na wengineo kwa upande wa polisi na kwa upande wa Mwanyika (sheria) kazi kubwa ilikuwa ikifanywa na vijana wake akiwamo DPP Feleshi na timu yake kwa hiyo hata mawasiliano ya kimataifa yanafanywa kitengo cha polisi wa kimataifa na TAKUKURU hata Hosea hakuwa anafanya kazi zote pamoja na kuwa kama mwanasheria na mchunguzi alikuwa akifanya sehemu ya kazi mwenyewe kama ilivyo kwa Saidi Mwema kwa baadhi ya upangaji na utekelezaji wa mikakati ya kazi za kikachero.

  Waandishi na Wana JF siku zi nyingi tuanza kujiandaa na UZUGAJI MKUBWA kuhusu EPA na kesi kibao za UFISADI
   
 5. Wakunyuti

  Wakunyuti JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani tuweni serious kidogo na vitu tunavyovileta umu.....hivi vingine tutavisoma tu kwenye magazeti au hata kwenye website za hayo magazeti..kuleta humu habari kama hii ni maudhii sasa...
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ni kweli ni maudhi, lakini nadhani wanaoudhika wachangie ili wajue HATUZUGIKI
   
 7. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hiyo hatujali kwani ni kujisafisha staili na time will tell. Msijali tunawasha moto wakibanika wanakulana wenyewe. Ndio mbinu tunayotaka kutumia sasa hivi.
   
 8. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kampeni za Uchaguzi zinaanza mwishoni mwa mwaka ujao,ili Muungwana amalize ngwe yake ,tapiga danadana mpaka 2010 ,hapo ndio tutafahamu alikuwa anaenda kufanya nini marekani kila siku.
   
Loading...