TAKUKURU wavamia kikao

TAKUKURU wavamia kikao

Hiyo Taasisi ingefutwa tu,uwepo wake hauisaidii Tanzania hata kidogo,maana rushwa inazidi kushika kasi.
 
Umekunywa gongo au?

Jibu swali wewe kidudu washwa hao watu wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria!!!!!
Je walikiuka???!!!

Siasa haiwezi kusimamisha utekelezwaji wa sheria. Katika muktadha huu nini maana ya "kuvamia"??????!!!!
 
Kama ni kweli basi NCHI IMEKWISHA KABISA! JAMANI hivi kweli inaingia akirini kweli? Ndiyo maana hata wachangiaji wakubwa hapa JF akiri zao ziko kama hao jamaa. Iende kwa MSALANI and co
 
Kama ni kweli basi NCHI IMEKWISHA KABISA! JAMANI hivi kweli inaingia akirini kweli? Ndiyo maana hata wachangiaji wakubwa hapa JF akiri zao ziko kama hao jamaa. Iende kwa MSALANI and co

Sasa ukiulizwa nchi imekwisha vipi kwa kuunganisha na tukio hili unajibu nini???!?!
Nini hakiingii akilini???!!!

Tuache kulalama tu wakati maswali ya msingi tunayaruka!!!!!
Mfano; wamevunja sheria, kanuni au utaratibu wowote kwa kufika hapo????!!!!
 
Aibu hii. sasa kwenye muktano wa hiki chama kilichojiifia wanatafuta nini hao -------kuru? matumizi mabaya kabisa ya resources zetu katika historia ya nchi hii.
 
TAKUKURU WILAYANI YA MUHEZA WAMEVAMIA KIKAO CHATATHIMINI YA CHADEMA NI MSINGI MDA HUU NO 2.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya CHADEMA NI MSINGI Wilaya ya Korogwe tulikua na mjadala leo siku ya tar 11/07/2014 kujadili juu ya habari yenye kichwa cha habari “TAKUKURU WILAYA YA MUHEZA WAVAMIA KIKAO CHA TATHIMINI YA CHADEMA NI MSINGI” iliyoandikwa katika Mitandao ya kijaamii (hususani Jamiiforum) siku ya Jumatano tar 09/07/2014.
Wajumbe tulishangaa juu ya habari hizi zisizo na ukweli wowote, na tulimshangaa mtoa maada kwa aliyoyawaza. Lakini pia, tulishindwa kuelewa juu ya umakini wa mtoa taarifa, kwa kuwa ameandika kichwa cha habari zinazohusu Wilaya ya Muheza huku akiweka Picha ya maafisa wa TAKUKURU wa Wilaya ya Korogwe. Lakushangaza zaidi ni juu ya uzushi kuwa maafisa hao walivamia Ofisi ya CHADEMA.
Katika hili niseme kuwa, Sisi kama kamati ya Chadema ni msingi tukishirikiana na Makatibu wa Majimbo ya Wilaya ya Korogwetulitoa mualiko kwa Maafisa wa TAKUKURU, nao waliitikia wito kwa kujumuika na sisi siku ya Jumatano tar 09/17/2014. Maafisa hawa walitufundisha mengi juu ya kupambana na rushwa, na sisi tulihamasika kufanya nao kazi kutokana na juhudi zao za dhati za kupambana na rushwa katika jamii yetu. Nasisitza kuwa, TAKUKURU ni wenzetu na tutaendelea kushirikiana nao katika shughuli zetu za Siasa za kila siku katika Wilaya yetu, kwa kuwa Chama chetu kinafanana kimtazamo na taasisi hii katika suala zima la kukomesha rushwa nchini.
Mwisho kabisa, tuwatake radhi Maafisa wa TAKUKURU WILAYA YA KOROGWE kwa kudhalilishwa katika tukio hili, pia, tunamtaka aliyeandika habari hizi zisizo na uhalisia aombe radhi kwa watu aliyowadhalilisha na afute maneno yake, kwani tupo katika uchunguzi na tukimgundua tutamuadhibu kwa kufuata kanuni za Chama.
Taarifa hii ni kwa niaba ya Kamati ya CHADEMA ni Msingi Wilaya ya Korogwe.
Abdallah Khalid Maonga M/KITI BAVICHA-JIMBO LA KOROGWE MJINI
 
Back
Top Bottom