Inferior Complex
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 3,655
- 5,008
Toa avatar yako.kwanzaJuly 2017 niliandika waraka humu, kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na baadhi ya magazeti kuwa Mbowe anakidai Chama Cha CHADEMA deni hewa la Tsh bilioni 7 na ameanza kujilipa. Katika waraka ule niliamua kuwa Mwanachama mfu wa CHADEMA hadi Sept mwaka huu nilipojiunga na CCM.
Baada ya andiko lile miezi michache baadae katika ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni ilionekana kuna malipo yasiyo halali ya Tsh bilioni 2 katika hesabu za CHADEMA zilizokaguliwa hadi wakati ripoti ile inatolewa.Hakuna aliyewajibika hadi sasa. Naamini ripoti ijayo itabaini malipo mengine kama nyaraka zote zitakazowasilishwa zitachunhuzwa kwa kina kuepuka kugushi.
Rais John Magufuli mwezi huu amemteua Mkurugenzi Mkuu mpya wa TAKUKURU na miongoni mwa maagizo ni kwa taasis hiyo kuchunguza NGOs na Taasis nyingine za Umma. Nampongeza sana Mh Rais kwa agizo hili. Japo hakutaja Vyama vya siasa lakini naamini agizo lile linahusisha taasis zote za umma hususan vyama vya siasa.
Unawezaje kuacha taasis ambayo mpaka leo imeshapokea zaidi ya bilioni 10 fedha za umma na nyingine nyingi toka nchi rafiki? Haitakuwa haki kwa watanzani.
Sisi wapiga vita ufisadi tumeshapiga mluzi hadharani kuashiria ufisadi huu mkubwa. Tunaamini hakuna aliye juu ya sheria. TAKUKURU chukueni hatua tutatoa ushirikiano.
Sasa Mbowe na vijana wake wameanza kuumbuka kwa kukosa fedha za kampeni, mishahara ya watumishi na fedha za uendeshaji Chama, wanataka kuhamisha agenda ionekane Tume ndio kikwazo na propaganda nyingine kibao. Serikali lazima iwachunguze viongozi wa CHADEMA seriously ili kujenga nidhamu katika uendeshaji siasa na vyama nchini.
Vyama vina jasho, damu, muda, na kila aina ya kujitolea kwa watanzania mbalimbali. Ni dhambi kubwa kikundi kidogo cha watu kujinufaisha kwa sacrifice hizo bila kuwajibishwa.
TAKUKURU mkichunguza mtakomesha uzushi wote na kuwafungua macho watanzania.
Hapa Kazi Tu.
Benson Mramba