TAKUKURU wamkamate January Makamba

TAKUKURU wamkamate January Makamba

kipumbwi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
3,196
Reaction score
9,200
Tanzania hakuna haki,wenye haki ni waliopo CCM na serikali yake ambao hawazidi hata 5 million,ndio maana tunataka mabadiliko,CCM na mfumo wake ifutwe!

CCM na dola yake inaendesha nchi kwa unafiki na uzandiki,inabagua na kutesa wasio watu wao,ni kinyume cha haki na utawala bora,ndio maana tunaunga mkono mabadiliko!!

January Makamba ameripotiwa na magazeti karibu yote kutoa rushwa jana Uwanja wa Taifa na akatangazwa live uwanjani,TAKUKURU ipo wapi?!

Umma ukampinga hapo hapo uwanjani kwa kuonyesha ishara ya mbadiliko ambayo ni kauli mbiu ya Lowassa na UKAWa,polisi walikuwepo uwanjania na TAKUKURU pia walikuwepo,Makamba kachukuliwa hatua gani?! Makamba alitumwa na nani jana?! Kikwete?! Magufuli au CC ya CCM?! Tunaohudhuria Taifa tunajua kuwa Makamba hajagi uwanjaniNtunawaonaga wakina Ridhiwani,Mwigulu na Mwenzao Zitto,jana Makamba alitumwa na nani?!

January Makamba ameripotiwa kuiba mitihani ya Taifa akiwa Galanos School kule Tanga(ushahidi wa uzi upo humu zaidi ya 3yrs na hajawahi kuja kukana),huo sio uhalifu na mtu alie mwizi wa mitihani leo ni Waziri na tuliambviwa ni msafi kuliko Pinda,Bilal na wengine,kwa maslahi ya nani?!

Lema juzi kakamatwa Arusha kwa kuzidisha kampeni dakika 6 tu na kutupwa lupango,wakina Makamba,Tibaijuka,Chenge,Ngeleja na CCM yao vipi?! Ni miungu mtu?!

Vijana wa UKAWa 19 walikamatwa na kufikishwa mahakamani na kunyimwa dhamana kwa kuvaa fulana zenye maandishi yaliyobeba ujumbe wa Mwalm Nyerere,haki iko wapi?!

CCM imeratibu maandamano weekend iliyopita na kuwalipa vijana mamluki wajifanye CHADEMA katika Mkoa wa Dar,Arusha,Shinyanga na Mwanza huku wa Mwanza wakiandama hadi kwa mkuu wa Wilaya,hawakukamatwa wala kushitakiwa na huku audio clip ya Masaburi ikivuja na kusikika wameaandaa mambo hayo na wanajiaandaa tena,haki iko wapi?! Huu sio uvunjifu wa Amani?!

Albino wanachinjwa na kuuawa kama kuku,hawapewi ulinzi au makazi maalumu ila Slaa anayemfitini Lowassa leo analindwa na usalama wa Taifa na kulipiwa gharama lukuki na serikali-ikiwemo huo ulinzi,cha ajabu akiwa CHADEMA alipigwa mabomu,risasi na virungu huku akivunjwa mkono na hakulindwa na Usalama wa Taifa!!

Kwa nini tuzidi kuichagua tena CCM na kina Makamba wao wanaofunga watu kamba Uwanjani,bungeni,kwenye mitandao,wizi wa simu na vocha huku wakivaa suti na kutuita malofa na wapumbavu??!!
 
Jamaa alifanya jambo baya sana linaloashiria kuwashawishi wananchi wawapigie CCM kura
 
Ila alipata mrejesho muruwa wa Tanzania hawacheki na kima tena hawataki kuvuna mabuwa!!
 
Takukuru mkuu wake ameteuliwa na Rais wa chama tawala. Si Chombo huru. Kwa hiyo usitegemee itende Kazi kwa CCM. Takukuru, msajili wa vyama, na tume ya uchaguzi ni taasisi nyeti zinatakiwa ziwe huru. Vinginevyo ni Mali ya ccm.
 
Jana ndio imedhihirika rasmi watu wameichoka CCM na wanataka mabadiliko. Pia jana imedhihirika kuwa CCM inatapatapa.
 
Naona ujumbe wako umeishia njiani hujasema kwanini ashtakiwe na kosa lipi au unadhani wote waliopo humu ni wapenzi wa mpira au wote walikuwepo taifa jana au walifuatilia matangazo ya mpira wa jana.

Usiache dhamira njiani........
 
Kazi moja ni jambia la kuchinjia October
 
Andaa kichinjio tuwaondoe pepo wote tz

Kuandaa kichinjio haitoshi,lazima tupige kelele na kupinga hadaa na udhalimu,mfno mtu alievujisha ile video au taarifa za Slaa kukutana faragha na watu wa CCM angekaa kimya tu kuandaa kichinjio chake na alivyofanya ni bora zaidi!!
 
Naona ujumbe wako umeishia njiani hujasema kwanini ashtakiwe na kosa lipi au unadhani wote waliopo humu ni wapenzi wa mpira au wote walikuwepo taifa jana au walifuatilia matangazo ya mpira wa jana.

Usiache dhamira njiani........

Mkuu Mmanu,soma tena,vinginevyo niseme umeghafirika tu!!
 
Last edited by a moderator:
Tena huyu takakuru lazima wamshike alimuhonga mgombea wa ukawa apotee kabisa asirudishe foum , hii ilikua rushwa iko wazi kabisa, kama hawa takakuru kweli wanapiga vita rushwa basi hii ya kumhonga mgombe wazi ni rushwa ya uchaguzi. Takakuru wacheni kutumiwa fanyeni kazi yenu Bumbuli
 
Hawa maccm dawa yao ni kuwachinja kibudu kwenye sanduku la kura

Watanzania mwaka huu tumeamua kuwa rais wetu ni Lowassa, hakuna hila wala propaganda itatuzuia
 
Naona ujumbe wako umeishia njiani hujasema kwanini ashtakiwe na kosa lipi au unadhani wote waliopo humu ni wapenzi wa mpira au wote walikuwepo taifa jana au walifuatilia matangazo ya mpira wa jana.

Usiache dhamira njiani........

Tukuulize kama umesoma vema ujumbe?

Kosa la RUSHWA wakati wa uchaguzi

Kwani jana ndio mara ya kwanza stars kucheza na timu za nje? Kama FISI WENU walikuwa na nia ya kufadhili watazamaji kwanini wangoje mpakA kipindi cha uchaguzi? Ni rushwa, rushwa, rushwa!

Akamatwe mara moja kwa kosa la RUSHWA!
 
asante sana , hiyo ya galanos ndio balaa ! shukrani kwa wananchi kwa kujibu kwa vitendo jana uwanja wa taifa .
 
Tukuulize kama umesoma vema ujumbe?

Kosa la RUSHWA wakati wa uchaguzi

Kwani jana ndio mara ya kwanza stars kucheza na timu za nje? Kama FISI WENU walikuwa na nia ya kufadhili watazamaji kwanini wangoje mpakA kipindi cha uchaguzi? Ni rushwa, rushwa, rushwa!

Akamatwe mara moja kwa kosa la RUSHWA!

Takukuru hawana meno ya kuwakamata vigogo, wao wanadili na vidagaa tu!

Unless wangeanza na huyu hapa!
 

Attachments

  • 1441540713356.jpg
    1441540713356.jpg
    25.9 KB · Views: 479
Tuzidi kusali ili haki ishinde dhuluma hapo oktoba 25
 
Naisubiri October 25 kwa hamu. Tumeshajua mbinu zao chafu na zimeshindwa, hawafai. Tuwaondoe.
 
Natamani nipate kazi ya ku-clean data za bvr, zitatangazwa lini?
 
Back
Top Bottom