Lihakanga
JF-Expert Member
- Dec 17, 2016
- 4,823
- 6,401
Kwa haraka baadhi yenu mtasema mimi ni wale wa UKUTA. Kiukweli mimi ni wa mbele kwa mbele damu. Nimeuliza ili nipate msaada bila kujali ushabiki wetu wa kisiasa.
Chombo hiki cha umma sijaona kazi zake, au niseme sijui kazi zake. Kwa mfano; unaitwa na TAKUKURU tena toka mbali uende ofisini kwao. Halafu wanakuuliza umepata wapi hela ya kujisomesha chuo kikuu wakati mshahara wako ni wa kawaida.
Wakati wamefika hadi kijijini kwako na kukuona unagonga kokoto za kuuza. Na huko juu tunasikia Richmond, Escrow, Rada nk.
Ndipo ninapojiuliza, nini kazi za TAKUKURU?
Nisaidieni nielewe waungwana!