TAKUKURU mtaendelea kumchunguza mkurugenzi wa manispaa Musoma hadi lini?

Musoma Yetu

JF-Expert Member
Mar 11, 2016
2,633
2,297
TAKUKURU mkoa wa Mara, kushirikiana na wilaya, kila kukicha mnakuja kupeleleza kuwa kuna harufu ya ufisadi hapa Manispaa. Mnapewa nyaraka mbalimbali na mnaondoka. Je, ni lini upelelezi wenu utaisha na tupate feedback? Maana tumeshoshwa na hii hali ya kusumbuliwa sumbuliwa
 
Nadhani wanatengeneza mazingira ya kuwawezesha kupewa rushwa na hao wanaochunguzwa.
Na inawezekana walishaanza kupewa cha juu muda mrefu na wamegeuza hiyo kuwa mradi wao... Wakiishiwa tuu, wanatia timu na kujidai kuomba nyaraka ...
 
Hili la Takukuru musoma, kuna ukweli umejificha nyuma ya pazia. Takukuru makao makuu, tunaomba muwafatilie hawa jamaa kuhusu uchunguzi wao wanaoufanya. Maana upo ki geresha geresha vile
 
TAKUKURU mkoa wa Mara, kushirikiana na wilaya, kila kukicha mnakuja kupeleleza kuwa kuna harufu ya ufisadi hapa Manispaa. Mnapewa nyaraka mbalimbali na mnaondoka. Je, ni lini upelelezi wenu utaisha na tupate feedback? Maana tumeshoshwa na hii hali ya kusumbuliwa sumbuliwa
wewe utakuwa na chuki binafsi na huyo DED,wanachukua nyaraka kila siku unajua zinahusu jambo gani? Kwani zikichukuliwa nyaraka lazima awe DED ndo anachunguzuzwa kwani hakuna watumishi wwngine? Hata hivyo uchunguzi ni nchakato', hao TAKUKURU wakishaamaliza uvhunguzi wao wanasubiria kibali cha DPP, watanzania tujifunze kuelewa mambo kabla ya kuanza kubwabwaja
 
Tatizo mnaangalia uchunguzi tu je mnatambua kuwa mahakamani kuna kuthibitisha bila shaka tuhuma na wanaohukumu ni wengine siyo takukuru bwana!
 
Duwa la kuku halimpati mwewe. Utakesha kumuombea apatwe na masahibu mwisho yatakugeukia mwenyewe. Acha kuwa na roho kama shetani.
 
Kama weweumekamilisha uchunguzi wako na unaushahidi wa kutosha mfikishe mahakamani
 
Kuna phd holders wengi tu kwenye nafasi za uteuzi. Wanavutwa na malipo mazuri posho za kujipangia na 'madili' yanayopatikana huko. Siku vikidhibitiwa, taaluma itaheshimika na watarudi kwenye fani zao. Vyuo vinauhaba wa wahadhiri lakini ofisi za serikali wamejaa 'ma-dr' wakipanga mafaili, kusign barua, na kusubiri kwenda kufungua au kuweka mawe ya misingi kwenye miradi. Muda ukienda hawana kitu kichwani, taaluma imeyeyuka.
 
Usitegemee watafanya kitu hapo,Ndio SHIDA ya Kuwa na viongizi wazee kama Mkuu Wa Takukuru Wa Mara
 
Kuna phd holders wengi tu kwenye nafasi za uteuzi. Wanavutwa na malipo mazuri posho za kujipangia na 'madili' yanayopatikana huko. Siku vikidhibitiwa, taaluma itaheshimika na watarudi kwenye fani zao. Vyuo vinauhaba wa wahadhiri lakini ofisi za serikali wamejaa 'ma-dr' wakipanga mafaili, kusign barua, na kusubiri kwenda kufungua au kuweka mawe ya misingi kwenye miradi. Muda ukienda hawana kitu kichwani, taaluma imeyeyuka.
Hili nalo neno. Nafasi za uteuzi zinalipa zaidi ya PUTS ndiyo sababu. Yale ma-v8 nayo yanashawishi maana huko vyuoni Prof. hana hata secretary sembuse ofisi yenye AC. Sasa upate uteuzi na mazingira safi kwa nini usiende mkuu!!!

Kiujumla ni hasara kwa taifa maana uhaba wa senior staffs huko vyuoni unazidi kuwa sugu na succession plan bahati mbaya wazee waliiweka kando ili waendelee kuwa on top na wanapostaafu wapewe mikataba.
 
Inaonekana huyu Mkurugenzi kawabana sana Madiwani wa CCM,waliozoea kujigawia tenda zenye harufu ya ufisadi ndio maana wanakuja humu jukwaani kuanza kumchafua acheni figisu figisu zenu huyu ni mtaalamu na anatumia weledi katika kufanya maamuzi sahihi.
 
Chuki za Musoma yetu dhidi ya mkurugenzi wa manispaa zilianza wakati na baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu 2015. Matokeo hayo ni uamuzi wa wananchi wa Musoma na si vinginevyo.
Ukandarasi wa mfukoni hauna nafasi kwenye serikali hii ya JPm
na kampuni hiyo( ya mara...tu) lazima itumbuliwe
 
Back
Top Bottom