Takataka za gazeti Majira na Channel 10 hazitufai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takataka za gazeti Majira na Channel 10 hazitufai

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Watanzania, Oct 17, 2009.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NImesikitshwa sana na sikuamni macho yangu kuona 'takataka' za udini kuandikwa katika gazeti la Majira la Jumamosi tarehe 17.10.2009 ukurasa wa mbele siku tatu tu baada ya kumbukumbu ya baba wa Taifa letu. SItaki kurudia kuzieleza takataka hizi kwa sababu hazitufai Watanzania. Lakini ni jambo la kushangaza kwa vyombo vya habari kukiuka misingi ambayo Mwalimu Nyerere aliiweka ya watanzania kuwa wamoja katika kupigana na ujinga maradhi na umaskni. Kwa nini gazeti la majira muokote takataka barabarani eti ni habari ya kidini inayohusisha chama cha siasa siku chache tu baada ya kumkumbuka Mwalimu?. Na wewe mwandishi wa habari ile una nini na Watanzania?. Nawe mhariri wa gazeti la Majira umeshindwa kazi?.

  Hivi jukwaa la wahariri mnafanya nini kudumisha misingi ya umoja aliyoweka mwalimu? Takataka za namna hii huonyeshwa pia na CHANEL 10 ikiwemo ile ya kipindi cha mtu yuleyule na waalikwa walewale kilichorushwa tarehe 14.10.09.

  Sasa ni wakati wa watanzania kushughulika, kulaani na kuwasusia gazeti la Majira na Chanel 10 kutokana na takataka zao wanazolisha, hazitufai watanzania.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 17, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ch 10 yupo mzee Makwaia wa Kuhenga!
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  tuelezee na sisi takataka hizo sijakupata mkuu, sina kopi ya gazeti hilo
   
 4. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ningependa kukujibu kwa uwazi lakini kwa sababu habari haina maslahi kwa taifa ndio maana sikuiweka wazi. Lakini kwa ufupi ni kuwa huyo mwanandishi kaokota makaratasi yenye madai eti chama fulani chenye uwezo wa kulikomboa taifa letu kuwa kinaungwa mkono na sehemu moja ya imani. Sasa naomba niishie hapa. Lakini habari yenyewe ni ya kushangaza hasa ikizingatiwa kuwa tulikuwa bado tunamawazo mazuri ya mwalimu baada ya kumbukumbu yake. Badala ya Majira kuandika mambo yanayowaunganisha watanzania dhidi ya watawala wabovu wao wanaleta mambo ya hovyohovyo. Ninakuomba ulitafuta mwenyewe. Nimeanzisha thread hii ili kuwaonyesha majira na CHANEL 10 kuwa wasiandike takataka za kuwagawa watanzania kiimani kwa kuwa tunawaangalia matendo yao na tutawasusa na kuwalaani.

  Ombi langu ni kwa jukwaa la wahariri wawashughulikie Majira na CHANEL 10 nasi watanzania tuwafuatilie nyendo zao za uandishi na tuwakatae.
   
 5. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  mkuu mekupata, hata mimi huwa najiuliza waariri wetu wanafwatiliaje maandishi na kuyaruhusu yapite, hawa watu wasipo makini wataharibu nchi...na ndo maana hata watu wengine wanawalaum sana mfano tu walivyo sema sumaye ana trilion nne matokeo yake ikala kwao..sikumbuki lilikua gazeti gani
   
 6. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli na vilevile Mtanzania gazeti la RA la leo pia lina habari za uelekeo huohuo wa Majira, CHANEL 10, sijui hawaoni masuala ya kuwaunganisha Watanzania. Wanataka kusaidia kugawa watu ili watawaliwe vibaya. Nadhani kuna haja na kuunganisha nguvu ili kukataa hivi vyombo vya habari na uoza wao
   
Loading...