Takataka za bongo zinachukuliwaje?

Pape

JF-Expert Member
Dec 11, 2008
5,488
79
Kuna kijarida fulani nimesoma kutoka kwa wenzetu ambao kwao uchafu unabaguliwa kuanzia mapema (at the source)mfano vyuma, mabaki ya chakula, plastiki, n.k kwa kuweka mapipa ya takataka husika karibu kila kona za mitaa na katika sehemu zenye mkusanyiko wa watu wengi. Kisha wahusika wanachukua uchafu huo na kuufanyia kazi.

Je sisi wabongo mambo kama haya tunafanyaje? Tunamipango gani? Serikali yetu inamipango gani?

i1246_Image001.jpg

i1245_Image000.jpg

Habari ndiyo hiyo...
 
Ni ngumu sana kwa bongo, kwa sababu mambo mengine yanaanzia kwenye utaifa na elimu ya uraia. Waweza kuniambia kwamba naingiza siasa lakini wakati mwingine pamoja na kuwa ustaraabu ni hulka ya mtu. Jamii ya watu miongoni mwao wamekata tamaa huwa hawana cha kupoteza. Mfano mzuri utauona kwenye uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya maji, wapo watu wanaofanya hivi kwa makusudi na ukitokea kumuona na kumuuliza atakwambia atunze chanzo cha maji wakati hata hiyo kesho hajui kama ataiona (kwa kukosa chakula cha leo). Hivyo hivyo katika kujidaidia hovyo mifano ni hiyohiyo.

Ni mawazo tu, miongoni mwao watanzania tupo.
 
kudadeki

atunze chanzo cha maji wakati hata hiyo kesho hajui kama ataiona (kwa kukosa chakula cha leo)
 
Back
Top Bottom