Takataka ni mtu ambaye anataka mambo mengi

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,832
Reaction score
6,470
Je umewahi kusikia mtu anaitwa taka taka?Kama hujawahi kusikia au kukutana na mtu wa aina hiyo basi leo nataka tujadili kuhusu hii tabia ya watu kuwa taka taka.Sasa ili usitetemeke maana ya takataka hapa ni sambamba na maana ya omba omba.Kama ambavyo kuomba kupo asi hata kutaka kupo lakini unapokuwa wewe unatabia ya kuomba kila mara,kila kitu,kila mahali basi tunakuita ombaomba.

Ombaomba wapo wa aina nyingi na kuna wengine hali yao na uwezo wao unawafanya wawe ombaomba lakini kuna watu ambao wana nguvu,afya na uwezo ambao nao ni ombaomba hawa ni watu ambao wanapoteza muda na baraka zao nyingi kwa kuwa omba omba.Unapokuwa na tabia ya kuomba omba unapoteza baraka nyingi.Hii ni kwa sababu huku duniani hakuna cha Bure.Unapoomba ukipewa ujue kuna baraka unampatia yule anayekupa.Inaweza kuwa baraka ndogo au kubwa lakini kifurushi chako cha mema kinapungua.So kama wewe ni ombaomba unajikuta unabakia katika hali ngumu ya kuombaomba wakti wote mpaka siku utakapokuwa huna baraka za kuwapa tena ndipo unapoomba unaanza kukataliwa na kunyimwa.Ukifikia hatua hio basi unakuwa mwanzo wa kuanza kula msoto na kudharaulika.

Sasa turudi kwenye kundi la watu takataka.Maelezo hapo juu yalilenga kukupa mwanga wa mada hii ambayo ni ya kibiashara na kimaisha.Takataka kama nilivyoeleza ni mtu ambaye anataka mambo mengi na kila kitu.Yeye anataka utajiri,anataka kazi,anataka wanawake wote,anataka kila biashara afanye yeye,anataka kila nyumba anataka kila anachokiona.Tabia hii ya kutakataka huwa inapunguze uwezo wako wa kupokea/kuchukua kila unachotaka.Kwa mfano kama wewe ni mwanafunzi na unataka uwe mwalimu,uwe daktari,uwe engineer uwe sijui astronomer utajikuta unatakataka tu lakini hutafanikiwa kuwa hata kimoja.Watu wa aina hii wapo wengi sana.Watu wengi wamepoteza ramani duniani kwa sababu ya hii tabia ya kutakataka.

Kutaka sio tatizo ila kutakataka ni tatizo na linawakabili watu wengi sana.Wengi wamepoteza bahati,furaha na ndoto katika maisha kwa sababu ya kutaka taka.Unakuta kijana anataka kufanya biashara hii leo,kesho anataka kufanya nyingine na kesho kutwa nyingine.Kila biashara anayosikia inalipa anataka kuifanya yeye.Anaishia kujikuta anakosa zote.

Sasa utafanyeje kuepuka kuwa takataka?Kuna mbinu nyingi za kushinda hali ya kuwa takataka amazo unaweza kuzitumia katika maisha yako.Mbinu ya kwanza na ya muhimu ni kujua uwezo wako(Know your limits).Ukifahamu kikomo cha uwezo wako ni rahisi kutambua fursa sahihi inayokufaa.Mbinu ya pili kuongeza uwezo wako(Maximize your potential)Jiongeze uwezo kwa kuongeza maarifa,taarifa,ujuzi n.k.NDIO Mbinu pekee ya kupunguza kuwa takataka ni kuhakikisha una ujuzi wa kutosha kutumia fursa fulani kikamilifu.

Kama nilivosema zipo mbinu nyingi.Karibu tujadiliane zaidi juu ya mbinu bora unazoweza kutumia ili kuepuka kutakataka
 
Mkuu, hili ni wazo jema, lakini Usipotaka Hutaweza au Hakitafanyika kitu. Kutaka na kuthubutu ni mapacha. Mm nadhani ni lazima Ukitake kitu kwa kukitamani kiwe chako halafu uthubutu kukifanya/kutekeleza au kukiweka katika vitendo kihalali na kuona matokeo yake (hasi au chanya).
Inapotokea ni Hasi, basi unahamia tena kitu kingine.Hapo ndipo mtu anaonekana anataka hiki leo na kesho anataka kingine anakuwa ni mtu wa kutakataka. Hili sio jambo baya kwani asipokuwa takataka atakuwa amedumaa.Unaridhikaje wakati mwendo bado hujaumaliza? Ss inapokuwa mtu amepitiliza kiwango (too much) na anakuwa ni mtu wa kujaribujaribu kila kitu, huyo hajifunzi ila ana-fumble around na ni mbabaishaji. Kwa hiyo mtu takataka ni mtu anayechuchumalia kupata maendeleo kwa kasi lakini hajawa Focused .Itafikia siku atatulia au atajitafakari na kusema: "Natazama yote ni Batili" ametawanya tu, hajakusanya chochote, hajaridhika na moyo/roho yake haijatulia. Kuna mfano wa jamaa mmoja aliitwa Suleiman alijaribu kila mwanamke aliyemwona ni mzuri na mwisho wa siku alijikuta anao wake 700(mia saba) na michepuko 300(mia tatu) na alikuwa bado anataka........=takataka!
 
Back
Top Bottom