Tajiri Mkubwa ahukumiwa kifo China

Tajiri Mkubwa ahukumiwa kifo China

Polite

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Posts
1,095
Reaction score
816
140523102540_liu_han_chinese_magnate_512x288_reuters_nocredit.jpg

Tajiri mmoja anayeaminika kuwa mshirika wa aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini China Zhou Yongkang, amehukumiwa kifo.
Mahakama imewapata na hatia Liu Han na kakake Liu Wei ya kupanga mauaji ya aina ya kimafia.

Wanaume hao walikuwa miongoni mwa kikundi cha watu 36 walioshitakiwa na makosa sawa na hayo.
Hukumu dhidi ya Liu Han inaaminika kuwa sehemu ya mpango wa serikali kupambana na ufisadi.

Mahakama ilisema kuwa Liu Han alikuwa amefaidika kifedha kutokana na vitendo vya uhalifu.
Pia katika matukio mengi walifanya mauaji na vitendo vya uhalifu ambavyo waliwadhuru watu na hata kuwazuilia watu kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa mahakama Bwana Liu aliendesha shughuli zake kwa kusaidiwa na maafisa kadhaa wa serikali ili kuweza kudhibiti mashine za michezo katika mkoa wa Guanghan .

Liu, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya madini ya Sichuan Hanlong Group, aliorodheshwa katika nafasi ya 148 kwa utajiri wake duniani na jarida la Forbes mwaka 2012.

Kampuni yake iliwahi kujaribu kutaka kuinunua kampuni ya madini ya Australia Sundance Resources Ltd ingawa hilo halikufanyika.
Kesi hii bila shaka inazua maswali kadhaa kwa viongozi wa kisiasa nchini China.
Huenda mkuu wa zamani wa ujasusi Zhou Yongkang pia akashitakiwa kwa kushirikiana na Liu.

Ikiwa jambo hilo litafanyika, hesi dhidi yake itakuwa ya madai mabaya zaidi ya ufisadi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya china.

Chanzo:bbc
 
Natamani mfumo wa china (wa kupambana na ufisadi)
ungetumika hapa bongo naamini akina vijisent,el,na wengineo wangesha nyongelewa mbali, kitambo tungekuwa tushawasahau.
 
Mahakama imewapata na hatia Liu Han na kakake Liu Wei ya kupanga mauaji ya aina ya kimafia.
Wanaume hao walikuwa miongoni mwa kikundi cha watu 36 walioshitakiwa na makosa sawa na hayo.

Hukumu dhidi ya Liu Han inaaminika kuwa sehemu ya mpango wa serikali kupambana na ufisadi.

Mahakama ilisema kuwa Liu Han alikuwa amefaidika kifedha kutokana na vitendo vya uhalifu.

Pia katika matukio mengi walifanya mauaji na vitendo vya uhalifu ambavyo waliwadhuru watu na hata kuwazuilia watu kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa mahakama Bwana Liu aliendesha shughuli zake kwa kusaidiwa na maafisa kadhaa wa serikali ili kuweza kudhibiti mashine za michezo katika mkoa wa Guanghan .

Liu, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya madini ya Sichuan Hanlong Group, aliorodheshwa katika nafasi ya 148 kwa utajiri wake duniani na jarida la Forbes mwaka 2012.

Kampuni yake iliwahi kujaribu kutaka kuinunua kampuni ya madini ya Australia Sundance Resources Ltd ingawa hilo halikufanyika.

Kesi hii bila shaka inazua maswali kadhaa kwa viongozi wa kisiasa nchini China.

Huenda mkuu wa zamani wa ujasusi Zhou Yongkang pia akashitakiwa kwa kushirikiana na Liu.

Ikiwa jambo hilo litafanyika, kesi dhidi yake itakuwa ya madai mabaya zaidi ya ufisadi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya china.
 
Dah, Hawa wachina huwa hawana mchezo, Nakumbuka wale walio kuwa wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza maziwa ya kulishia watoto kwa sasa walisha tangulua mbele za haki, Huku wakina sijui nani wanatengeneza Dawa feki za Ukimwi na bado wana dunda mitaani na tena ni viongozi ndani ya Chama.
 
Natamani mfumo wa china (wa kupambana na ufisadi)
ungetumika hapa bongo naamini akina vijisent,el,na wengineo wangesha nyongelewa mbali, kitambo tungekuwa tushawasahau.

Kamwe mfumo huu hautekelezeki hapa Tanzania sababu mafisadi wenyewe ndio watunga shria unaona akina vijisent bado wanapeta tu we acha tu dawa ni kuwabadilisha hawa walio lewa madaraka noa wafanye kazi za vibarua
 
Dah, Hawa wachina huwa hawana mchezo, Nakumbuka wale walio kuwa wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza maziwa ya kulishia watoto kwa sasa walisha tangulua mbele za haki, Huku wakina sijui nani wanatengeneza Dawa feki za Ukimwi na bado wana dunda mitaani na tena ni viongozi ndani ya Chama.

Imagine! Mtu kama Madabida si wa kunyonga kabisa. Mtu anatengeneza dawa feki anaua wagonjwa wa ukimwi halafu eti bado hata kujiuzulu tu uongozi wa chama achilia mbali kunyongwa ikithibitika.
Yupo tu anakula bata na watu wanaona poa tu.
Akili za wa tz wengi ni kati ya Maajabu 10 ya Dunia aisee! I think its even beyond the most stupidity person in the world.
 
Hili limnawezekana Tanzania pekee
 
Mfumo mzuri sana huu,na hela zote hizo ingekuwa bongo watu wangeneemaka halafu mwisho wa siku hakuna kesi wala hata harufu yake hamuisikii
 
natamani mfumo wa china (wa kupambana na ufisadi)
ungetumika hapa bongo naamini akina vijisent,el,na wengineo wangesha nyongelewa mbali, kitambo tungekuwa tushawasahau.
loh tema mate chini wengine tungekuwa tushazika ndugu zetu
 
Dah, Hawa wachina huwa hawana mchezo, Nakumbuka wale walio kuwa wamiliki wa kiwanda cha kutengeneza maziwa ya kulishia watoto kwa sasa walisha tangulua mbele za haki, Huku wakina sijui nani wanatengeneza Dawa feki za Ukimwi na bado wana dunda mitaani na tena ni viongozi ndani ya Chama.

Wazee wa wachina waliweka miiko ndani ya serikali yao ndo mana hadi leo inafuatwa, ila hapa bongo wazee wameuliwa na wanavunja miiko
 
Natamani mfumo wa china (wa kupambana na ufisadi)
ungetumika hapa bongo naamini akina vijisent,el,na wengineo wangesha nyongelewa mbali, kitambo tungekuwa tushawasahau.

Angalizo ; kwa tanzania siyo kila usikiacho ni chakweli. Shirika linaweza kufilisiwa na moko ukaambiwa/ ukatangazwa wewe kuwa ndo umeliua......... be careful annual.
 
Back
Top Bottom