Tajadhari kwa wafanyakazi tarehe 2/5/2017

Tajadhari kwa wafanyakazi tarehe 2/5/2017

Mliobaki kuanzia sasa mmuanze kuchukua mkopo na kununua ardhi hapo ulipo au inakopatikana uanze kuwekeza kidogokidogo kwani hujui yajayo baada vyeti feki inaweza kuwa wenye elimu feki,yaani wenye vyeti lakini wanashindwa kumudu nafasi zao mf. Mwalimu aliyemaliza kidato cha nne na kuhitimu chuo cha ualimu,hata kumfundisha hisabati mwafunzi wa darasa la tatu hawezi.
 
Daaah, kweli.

Kesho asubuhi , mapemaaa kabla ya jambo lolote weka bundle la mtandao ulio mubashara ili upate ushilawadu na ubuyu wa ofisini kuhakikisha kama jina Lipo au mstari umeishapigwa na kubandikwa notice board.
 
Kale kanyimbo ndio muda wake sasa nitumieni .wacha waisome
 
Aisee serikali hii itaua watu kwa presha kuna bibi mmoja mwalimu kanifundisha enzi hizo leo hii eti nae jina lake limetajwa kamezeeka mpaka wamekarudisha kufundisha chekechea sijaamini sijui wanampango wa kudesa kiinua mgongo chake inatia huruma
 
BP imezidi kipimo. Miaka 31 kazini. Leo ametokea mtu yulee nilomchagua mwenyewe. Anaamuru ati niende nkalale bila hata shahara la mwezi ulopita (Sio huu unaoanza), hakuna hata kiinulia mgongo wangu, sikuwa mimejiandaa.
Halaf, kesho nisiende kazini, labda nikifika ni kuondoa tu ilee hirizi yangu nlopewa na mganga yuleee alokufa mwaka jana.
Yaani, nadhani kuanzia 15th May, vifo vya ghafla vitakuwa vingi sana. Hakika, mkuu amebuni mbinu mpya ya kupunguza idadi ya watu, Just by natural system (death caused by BP)
 
BP imezidi kipimo. Miaka 31 kazini. Leo ametokea mtu yulee nilomchagua mwenyewe. Anaamuru ati niende nkalale bila hata shahara la mwezi ulopita (Sio huu unaoanza), hakuna hata kiinulia mgongo wangu, sikuwa mimejiandaa.
Halaf, kesho nisiende kazini, labda nikifika ni kuondoa tu ilee hirizi yangu nlopewa na mganga yuleee alokufa mwaka jana.
Yaani, nadhani kuanzia 15th May, vifo vya ghafla vitakuwa vingi sana. Hakika, mkuu amebuni mbinu mpya ya kupunguza idadi ya watu, Just by natural system (death caused by BP)[/QUO

lazima mtu achekee chooni 🙂
 
Kwa kuwa rizki mtoaji Mungu, kama rizki ipo ipo tu !Mwenyezi Mungu kasha kadiria na kesha andika hatua utakazo pitia duniani, kukosa kazi sio ndio mwisho wa maisha bali mwisho wa maisha ni kufa tu!.
 
KUNA JAMAA KAANZA KUNITAFUTA ANANIULIZIA ''VIPI HAMNA MISHE YOYOTE UNAWEZA NIUUNGANISHA YOYOTE ILE'' NAKAMUULIZA UTAWEZA MIKIKIMIKIKI MAANA HUKU JUHUDI ZAKO NDO MLO WAKO AKANIJIBU ''UNAFIKIRI NTAWEZA KITU GANI KINGINE HAMNA NAMNA NIPO TAYARI'' ... KAWA MPOLE KWELI HADI HURUMA
Unataka kunambia kalegeza tai mara hii..
 
Back
Top Bottom