Taifa Stars vs Morroco October 9 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa Stars vs Morroco October 9 2010

Discussion in 'Sports' started by Lucchese DeCavalcante, Oct 4, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Haya tena weekend ijayo kutakuwa na mtanange kati yetu na Morroco pale National Stadium na hii itakuwa mechi ya pili ya kimashindano ya kocha Poulsen baada ya ile ya sare ya 1-1 dhidi ya Algeria and I hope tutaondoka na point (s) kama tukikaza msuli...


  [​IMG]

  TIMU ya Taifa ya Morocco inatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 8, mwaka huu tayari kwa mchezo wa awali wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2012 dhidi ya Taifa Stars.

  Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kwenye mtandao wa Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF), kikosi hicho kitatua nchini kikiwa na wachezaji 22 akiwemo Marouane Chamakh wa Arsenal ya England ambao watacheza dhidi ya Taifa Stars Oktoba 9, mwaka huu.

  Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili nchini siku hiyo ni makipa Karim Fegrouch (Wydad Casablanca), Nader Lamyaghri (Wydad Casablanca) na Ahmed Mouhamadina wa Olympique Khouribga.

  Wengine ni mabeki Mehdi Benatia (Udinese), Adil Karrouchy (Difaa El Jadida), Fettah Boukhris (FUS Rabat), Morad Ainy (Raja Casablanca), Rachid Soulaimani (Raja Casablanca), Michael Chr├ętian Basser (AS Nancy), Chakib Benzoukane (Sofia) na Hicham Mahdoufi wa Raja Casablanca.

  Viungo ni Adil Hermach (RC Lens), Mohamed Berabeh (Al Dhafra), Issam Erraki (Al Wahda), M'bark Boussoufa (Anderlecht), Karim Al Ahmadi (Feynoord Rotterdam) na Nabil El Zhar wa Liverpool.

  Washambuliaji ni Mounir El Hamdaoui (Ajax Amsterdam), Chamakh, Youssef El-Arabi (Caen), Adil Taarabt (Queens Park Rangers) na Youssef Hadji wa AS Nancy.

  Kocha wa timu hiyo, Mfaransa Dominique Cuperly amejigamba kuwa atahakikisha anaibuka na ushindi katika mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
   
 2. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Je ITV wataionyesha mechi hii?Kwa sisi tulio n'gambo tutaiangaliaje mechi?
   
 3. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  imekaaa njema hiyo mfyukuzi
   
 4. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kuna mkataba kati ya TFF na Star TV wa kuonesha mechi za VPL na kwa namna ambavyo hapa kwetu huwa hakuna utaratibu mzuri wa matangazo ya mpira kwenye Tv, tegemea yeyote kati ya ITV au Star TV kuonesha mechi hiyo.
   
 5. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nadhani hii mechi itaonyeshwa live na Supersport kama ile ya Uganda na Angola iliyopita will keep you posted
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  ssi mvuke mto rudini nyumban muangalie mrudi kama wakina henry joseph na dannymrwanda walio ngambo polen sana atutaruhusu chombo chochote kuonyesha mpira huu hasa kwa wakati huuu tukitafuta pesa za kuwatunisha mfuko wa SAIDIA TAIFASTARS ISHINDE
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,515
  Likes Received: 19,937
  Trophy Points: 280
  hakuna wachawi wamloge chamakh hata siku mbili tu zile ashikwe na tumbo la kuharisha
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kuna forward mmoja wa arsenal nimemuona jana kwenye mechi ya chelsea ni mchezaji wa Morocco na atakuwa kwenye kikosi kitakachokuja....
   
 9. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  MSHAMBULIAJI wa Simba ya Dar es Salaam, Mussa Hassan ‘Mgosi' ameenguliwa katika kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars' kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Morocco kuwania kufuzu fainali za Afrika.

  Mgosi ni miongoni mwa wachezaji 23 waliotangazwa kwenye kikosi cha Stars Jumatano wiki hii na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jan Poulsen raia wa Denmark kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Lakini habari zilizopatikana kutoka ndani ya timu hiyo zilieleza kuwa Poulsen amemuengua Mgosi kutokana na kukabiliwa na tatizo la goti aliloumia katika mchezo dhidi ya Polisi Dodoma wiki mbili zilizopita uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ambao ulikuwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Florian Kaijage alithibitisha jana kuenguliwa kwa Mgosi, ambaye Jumatano aliingia dakika za majeruhi wakati wa mchezo wa Simba na Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

  Kaijage alieleza kuwa licha ya kuenguliwa Mgosi, kocha huyo amesema hataongeza mshambuliaji mwingine ili kuziba pengo hilo.

  Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotangazwa wiki hii ukiacha Mgosi ni makipa: Shaaban Kado (Mtibwa), Kaseja (Simba) na Said Mohammed (Majimaji).

  Mabeki wa pembeni: Shadrack Nsajigwa na Stephano Mwasika (Yanga), Haruna Shamte (Simba) na Salmin Kiss (Polisi Dodoma), wakati mabeki wa kati ni Agrrey Morris, Erasto Nyoni (Azam) na Nadir Haroub (Yanga).

  Viungo ni: Henry Joseph (Kongsvinger-Norway), Shaaban Nditi, Salum Machaku (Mtibwa), Nurdin Bakari (Yanga), Jabir Aziz na Selemani Kassim (Azam), Idrissa Rajabu (Sofapaka-Kenya) na Nizar Khalfan (Vancouver-Canada).

  Washambuliaji ni Danny Mrwanda (DT Long An-Vietnam), Mohammed Banka (Simba), Mrisho Ngasa na John Bocco (Azam).

  Wakati huo huo, baadhi ya wachezaji wapya wa Taifa Stars wameelezea kufurahishwa kwao na kuitwa kwenye kikosi hicho.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana, wachezaji hao walielezea kufurahishwa kwao na kwamba watatumia kila uwezo kuhakikisha wanafanya vizuri.
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  mtumie appostle masa
  hiyo kama special request ama uongozi wa kempinsiki uajiri vile vishada vya kiarabu pale las vegas vifanye usafi hotelini kwa muda ni rahisi kuvimaliza..kama utawahahakikishia hela nzuri..wamoroco wanapenda sana ngozi za nje ya nyumban ..so ni wakati muafaka kuwapatia ajira na dada zetu wa lasvegas...siku moja kabla tuwawekee wawachannyie oral juice ..ama kuna dulucolax free wachanganye kwenye juice weeeee... hiyo nitaitoa mimi bure kuchangia timu yangu ishinde watakaoitaji naomba ni PM
   
 11. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Jamani kuna mtu anayeweaza kukonfirm kwamba ITV Tanzania itaonyesha mechi hiyo?
   
 12. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Chama la ushindi chini ya Mdanish Poulsen....

  [​IMG]
   
 13. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kuna anayefahamu tiketi zitaanza kuuzwa lini huko?
   
 14. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Tikiti zitaanza kuuzwa alhamisi mkuu
   
 15. Kilakshari

  Kilakshari JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2010
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
 16. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  maumivu yanakuja
   
 17. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  hahaha...inabidi kujiandaa tu na hayo maumivu, tutafanyaje sasa na wakati hicho ndio chetu. Tuombe Mungu yanaweza yakawa mambo mazuri :pray2:
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Naimani Taifa Star itafanya vema
   
 19. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kabla ya mechi kuchezwa wengine huwa tunakuwa na maumivu,lakini tukishaingia uwanjani na kuona game inavyokwenda,maumivu hupungua taratiiibu na baada ya matokeo tunajifariji kwa kutathmini namna game ilivyokuwa,na maisha yanaendelea maana game hiyo inakuwa imekwisha tunasubiri ijayo. that is how soccer life is.

  Sina hofu ya maumivu kwa game hii sababu tuna uzoefu wa kufanya vizuri tunapocheza na timu kubwa kama hii,ila sasa mechi ijayo ndo shughuli maana wachezaji wetu wasipoona jina kubwa ndo shida inakuja, wanashinda kabla ya kuingia uwanjani.Sijui kama huu ugonjwa bado utakuwepo.
   
 20. g

  gutierez JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 1,254
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  drogba na ramirez(wa chelsea) walishatufunga,sijui chamakh nae atakuwa na hasira za kushindwa kuwafunga chelsea j2 iliyopita atamaliza hasira zake bongo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...