Ninasikitishwa na matokeo tunayoyapata.Tunafahamu kwamba mpira una matokeo ya aina tatu yaan kushinda,kufungwa au sare lakini km tunataka kusonga mbele kwanza lazima tuweke mazingira ya namna yoyote kushinda mechi za nyumban.Tulitumia nguvu kubwa sn had tunafunga magoli mawili dhid ya timu bora km ivory coast na tunashindwa kufunga hata goli moja dhid ya uganda!!!Hii ni aibu na jambo la kushangaza sn kwa sisi tunaoamin kwamba timu yetu ya taifa inaimarika siku had siku.Naomba niongelee kwenye masuala ya ufundi though mimi sio mwalim wa mpira lakin kuna tatizo ambalo nimeliona na ninaomha sn benchi la ufundi iliangalie,Hatuna namba sita ktk timu yetu nasema hiv kwa sababu wengi wetu tunamfaham frank domayo ni mchezaj mzur sn na huwa anacheza vzr sn hata ktk klabu yake ya yanga lakin hachez namba sita bali ucheza namba nane!Haina ya soka wanayocheza kwa pamoja domayo na surr boy yapendeza sn kuitizama na muda mwingine wananifanya niwakumbuke viungo bora pale fc barca(xavi&iniesta),wanavyocheza na kuachiana moja moja.Mapungufu ya namba sita yanaonekana pale tunaposhambuliwa kwan wapinzan wetu uonekana ni hatar sn,Wkt huo km ni namba tatu anakuwa amepanda mbele sawa na namba mbili,namba sita anakuwa naye amevuka ktkat ya uwanja so nyuma anabak kelvin na aggrey/nabir haroub!Kwa aina hii ni lazima timu pinzan ionekane hatari kwetu.Ni soka ya wapi hii ambayo muda wote namba sita yupo juu ya mstali wa katikat??Hebu tumkumbuke shaaban nditi huyu ni moja ya natural defensive midfielders km coach/bench la ufund halipend kumtumia basi kwann athuman idd asicheze??Turejee aina ya magoli tuliyofungwa na moroco kwao anza na hile penati then mech na ivory coast ktk magol manne matatu ni km na moroco then tumalizie na uganda hii juz,unapigwa mpira mrefu mshambuliaj wao anakosea kuutuliza lakin anaukimbilia anatuliza then mpaka anageuka na kumtazama mwenzake anayetokea katikati/kiungo na kumpa pas yenye umakin mkubwa na anatufunga kwa akili na sio nguvu!!Naomba wachangiaji tuache uyanga na usimba ktk hili labda tukipata mawazo mazur wanaweza wakapita huku na kufanya mabadiriko kidogo ktk timu yetu ya taifa.
Naomba kuwasirisha.mods naomba mkawie kuutoa huu uzi