Taifa Stars na Bafana Bafana ya kichina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa Stars na Bafana Bafana ya kichina

Discussion in 'Sports' started by Mphamvu, May 14, 2011.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Leo timu yetu ya soka imecheza na Afrika Kusini, mechi ambayo imeisha kwa sisi kufungwa goli 1-0. Ingawa sikutazama mechi kuna mambo kadhaa yananikanganya, Bafana Bafana imecheza mechi ya leo bila nyota wake 11, Siphiwe Tshabalala, Reneilwe Letsholonyane, Steven Pienaar, Tsepo Masilela na Bongani Khumalo wakiwemo. Mechi hii haikuwa katika ratiba za FIFA na TFF wanajua fika ugumu wa kuratibu mechi hizi.

  Ndiyo, Kaizer Chiefs, Preston North End, Ajax Cape Town, Tottenham Hotspurs, Rubin Kazan na timu nyinginezo zenye wachezaji wa Bafana Bafana zisingeweza kuruhusu wachezaji wao kurudi hasa wakati huu ambapo ligi nyingi duniani zinaelekea ukingoni, tena kuja kucheza mechi ambazo hazitambuliwi na FIFA. Tatizo langu si kutotambuliwa kwa mechi, tatizo ni kucheza na timu moja chini ya mwavuli wa nyingine. Wote tunaijua Bafana iliyoichachafya Mexico pale Soccer City na baadae kuifunga Ufaransa pale Royal Bafokeng, kama vile haitoshi majuzi ikafunga Misri kwenye michuano ya kufuzu AFCON 2012.

  Je, timu iliyocheza michezo hii ndiyo tuliocheza nayo leo? Endapo tungeshinda mechi ya leo, mbwembwe za magazeti zingekuwa nyingi hapo kesho, ingawa ukweli ni kuwa hatujacheza na Bafana Bafana halisi. Kwao, mechi hii ina faida kwa kuwa wameitumia kujaribu kikosi chao cha pili, ila sisi tumejidanganya kwa kudhani kuwa tumecheza na Afrika Kusini, kumbe tumecheza na kikosi cha pili. Kama ni kucheza na timu za kiwango cha kati, tungeomba hata Rwanda au Kenya, na kama tunataka timu za kiwango cha juu, basi tucheze na timu halisi.

  Naomba kuwasilisha!
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Jana baada ya mechi niliweka uzi wenye utafiti, ukihoji uhalali wa Taifa Stars kucheza na Afrika Kusini iliyokuwa bila nyota wake 11. Mods wakaiunganisha kwenye updates za matokeo, nikaweka tena uzi kwenye jukwaa la ulalamishi, hiyo ndo ikafutwa kabisaa! Najua mnatingwa, ila ni vema kujua kutofautisha maudhui kati ya uzi na uzi. Naombeni uzi wangu urudi kwa ajili ya mjadala na wadau watoe maoni yao, natumia mobile hivyo siwezi kukopi na kupesti nitengeneze mwingine... Tutendeane haki!
   
 3. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pole kiongozi
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Inauma mkuu, uzi haujachangiwa siku ya pili sasa... Kisa wameuchanganya!
   
 5. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi naanza kuchangia hivi:

  Kwa kiwango gani tulichonacho hadi bafana walete nyota wao 11 kama timu B yao tu inatuchakaza? Unadhani wangekua wanaenda kucheza na black stars ama timu nyingine kali wangeleta yale mafotokopi yao?

  Suluhisho: tukuze kiwango chetu, kikipanda tutaombwa friendly matches na timu bora
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  May 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Hapana kaka, kosa lilikuwa la kwetu kuomba gemu ambayo FIFA hawaitambui, klabu zikagoma kuruhusu wachezaji wao, matokeo yake tukacheza na Bafana ya maboksi, mbona Brasil walileta kikosi full pamoja na ubovu wetu, Kodivaa pia walicheza wakiwa kamili, pia usisahau mechi yetu na Misri kule Aswan!
   
 7. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #7
  May 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi uzi ndo nini?? Uzee tabu kweli naomba ufafanuzi
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Uzi ndio kusema 'thread' kwa Kizungu, mwendelezo wa mada yenye maudhui yale yale. Pole babu/bibi!
   
 9. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana mie ni Babu nimekupata sasa yaani nilikuwa sijaelewa kabisa
   
 10. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Haikuwa vibaya kuomba mechi ile, ila matatizo yetu ni yalyale miaka nenda rudi, kushindwa kujumuisha wale vijana wa timu za chini hata katika mechi ambazo tunajua kuwa wenzetu watachezesha kikosi cha tatu!.

  Nadhani tulitaka kushinda ili tujisifu sana, kuwa tumecheza soka ya hali ya juu, Mrope ni noma, Bafanabafana yapata kiboko yake n.k.

  Tuendelee na mwendo huu wa kutaka kutengeneza Headlines, tuone mwisho wake, haikuwa vibaya hata kidogo kama tungechukua wachezaji 6 katika kikosi cha olimpiki kinachosubiri kucheza na Nigeria hata kama wangekuwa chini ya Jan.
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa N'gombe, lakini nadhani lengo la kucheza na Bafana ni kujaribu uwezo wetu na timu za kiwango chake. Ili kama tukiwafunga Misri, Kodivaa na Cameroon, kisha tukaenda suluhu na Algeria, Nigeria na Angola, na pengine Morroco wakatufunga kwa taabu, tuseme kuwa kiwango chetu kimepanda. Je, kama timu zote zitaleta kikosi cha tatu kwenye mechi za kirafiki, tukipangwa na timu hizo kwenye mashindano si kimeo?
   
 12. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kucheza na kikosi cha tatu kama ilivyokuwa mechi iliyopita, si vibaya kwa mazoezi, ila kwa maandalizi ya mechi za kimashindano naona haikai sawa kwa vile haituandai kiushindani, na pia unakuta hata wachezaji wetu ambao wengi huwa wanapenda kukamia wachezaji wenye majina makubwa kimtindo wanakuwa kama wameidharau mechi,wakati kiukweli wanapaswa kutambua kuwa hakuna mechi ndogo, so ukiwajumuisha na yoso kidogo na wao(wakongwe) itabidi waendane na spidi ya mchezo.
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Naungana na wewe kwa asilimia zote, ile mechi kidhima ina manufaaa kwao kwa vile wanajaribu plan B zao. Kama ni mazoezi ya kawaida, tungeomba na timu kama Kenya, Rwanda, Uganda n.k ambazo ni bora maradufu ya kikosi B cha Afrika Kusini na timu hizo zingetuheshimu kwa kuleta vikosi vya kwanza.
   
 14. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe mkuu. Tunaomba mechi si kwa lengo la kukuza na kuimarisha kiwango cha timu bali kwa kutafuna upenyo wa kufanyia propaganda (ikiwa tutabahatisha matokeo mazuri katika mechi husika)
   
 15. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #15
  May 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh, kaaaazi kweli kweli! Kumbe haikua katika ratiba! Ni bora basi mechi ile isingekuwapo kabisa. Na Nakuunga mkono hoja yako, Mara mia tungecheza na uganda ama kenya iliyokamilika kuliko kucheza na south africa B. Kwa mtaji ule wao south africa ndio waliofadika zaidi na mchezo ule
   
 16. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi kaka. Siasa za kuchumia tumbo zimekuwa nyingi pale TFF, wanaleta timu kubwa ili wapange viingilio vikubwa, wanajua wakileta Uganda pesa ya mlango haitakuwa kubwa hata kama game ina manufaa kwetu. Hakuna hata siku moja Kaijage alifanya press conference akasema mikakati ya ushindi, always viingilio, viingilio!
   
 17. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Ndio, game haikuwa kwenye ratiba za mechi za kirafiki za kimataifa. Sheria ya FIFA ni kuwa kama gemu wanaitambua, timu ya taifa ina haki ya kumchukua mchezaji wao wakati wowote hata kama wana mechi na Mbinguni FC, kama ni kinyume chake, hawakupi mchezaji, na kashtaki popote!
   
Loading...