Taifa stars mmetuangusha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa stars mmetuangusha.

Discussion in 'Sports' started by ipogolo, Sep 4, 2011.

 1. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,058
  Likes Received: 2,939
  Trophy Points: 280
  Bila ubishi mechi ya jana ya kufuzu katika mashindano ya AFCON 2012 kati ya Taifa Stars v/s Aljeria ilikuwa nyepesi sana kwetu kama utulivu,umakini na weledi(proffessionalism) ungekuwepo. Tuliwapa support ya kushangilia lakini wachezaji mmetuangusha jamani. Mnataka nini? Tumekosa magoli muhimu sana. KWA UJUMLA MECHI ILIKUWA YETU. Mwalimu Poulsen usiogope kushambulia ukiwa uwanja wa nyumbani.
   
 2. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndio vipaji tulivyonavyo hivyo!
   
 3. M

  Madaraka Amani Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni mambo ya ajabu hivi unafikiri Tanzania katika miaka ya karibuni watafikia angalau kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa no rafiki yangu usijidanganye soka la Tanzania halipandi kwa sababu nyingi mno. mpaka hapo wabongo watakapokaa chini na kuzifanyia kazi sababu moja baada ya nyingine ndipo tataanza kuona raha ya mchezo wa mpira wa miguu,. Nataka nikupe baadhi ya sababu kwanza viongozi wa vilabu wengi wameomba uongozi kuganga njaa au kujipatia kipato. kwa hali hiyo jitihada kubwa na mtazamo ni fedha.yuko tayari kuhonga wachezaji ili timu yake ishindwe iwe sababu ya mtu kuingia madarakani. Pili maandalizi ya timu zetu ni hafifu mno tunaandaa timu bado wiki mbili za mashindano kwa hali hiyo huwezi kuwashinda wachezaji ambao wako kambini mwaka mzima. Tatu serikali haijatoa kipaumbele katika michezo wanaona ni kupoteza muda. Nne wachezaji wetu wanachukuliwa wakiwa wameshakomaa na baadhi wanavuta bangi, zaidi ya hayo ni wachovu na wananjaa kali wananunulika kirahisi ninaweze kuandika kutwa nzima. Wakati nchi hii ilikuwa ianfanya vizuri katika tasnia hii ya michezo watanzania walikuwa wanaipenda nchi yao walicheza kwa moyo wa uzalendo sio kwa fedha. nafikiri inatakiwa moyo wa uzalendo usiishie kwenye masuala ya kisiasa iwe mpaka kwenye michezo. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ni mawazo mazuri sana uliyoyatoa kwani kuna vitu vingine vinakuwa vya kijinga kiasi cha kutamani kuwapiga makofi kama lile swala la yanga unafikiri tutakuja kuendelea kweli. halafu bado wana mambo yakizembe kama kwenye mechi ya mwisho ya azam fc unaambiwa kibali kimetolewa muda ulishakwenda sana ukiuliza sababu ya kuchelewesha hakuna.

  nimeipenda hii sentensi.
   
 5. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ipo siku kila mtu ataamini kuwa TFF inanufaika na Stars kufanya vibaya katika kila mechi muhimu halafu nyepesi.
   
 6. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Asilimai kubwa ya wachezaji wetu wa kulipwa wanacheza mechi kidogo sana huko walipo. Kwa ujumla nia afadhali ya kuwajumuisha wengi wa nyumbani kuliko hao ambao wamekuwa watazamaji tu huko Ulaya na kwingineko. Lakini pia home nako kumeingilia maana wacahezaji wengi walio bora katika ligi ya kwetu wanatoka nje. jamani kazi tunayo.
   
 7. ipogolo

  ipogolo JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 4,058
  Likes Received: 2,939
  Trophy Points: 280
  Madaraka hakuna timu inaya michezo wa aina yoyote inayoweza kukaa kambi mwaka. hizo ligi nyingine watacheza lini? ni Kweli brazili wanakaa kambi mwaka mzima? mbona wachezaji wao yunawaona katika mechi mbalimbali za ligi duniani?
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Wasimamishe kama wanakuangusha@@
   
 9. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,082
  Trophy Points: 280
  kwani unashangaa au kusikitika kitu gani!!?? ...Taifa Stars waliingia kwenye haya mashindano wakiwa na malengo (namaanisha Tanzania maana ni timu yetu sote) na moja ya malengo ni lile la siku zote yaani "mmetufunga lakini chenga twawala", na ndio maana tulivyoshinda tu mchezo wa kwanza tulikuwa tumepita malengo na ikaamuliwa kabisa kuwa timu iende Ikulu na Bungeni kueleza na kushukuliwa kwa heshima waliyokuwa wameliletea taifa kwa kushinda mechi moja.
  Kwani Ipogolo ulikuwa na malengo mengine zaidi ya hapo!?
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mmmmmmhhhhhhh...
   
Loading...