Taifa Stars:- Aibu Tupu

Apr 27, 2006
26,588
10,375
TAIFA STARS
DRC
mshambuliaji hatari wa kongo alain kaluyituka dioko
ambaye kaiua taifa stars leo kwa kufunga mabao yote mawili. kijana huyu mwenye umri wa miaka 25 anaichezea T.P Mazembe ya Kinshasa

MABINGWA WA KOMBE LA CHAN TIMU YA TAIFA YA KONGO IMEITUNGUA TAIFA STARS 2-0 KATIKA MCHEZO WA KIMATAIFA WA KIRAFIKI KWENYE WANJA JIPYA LA NESHNO HAPA DAR.


MFUNGAJI WA MABAO YOTE NI HUYO KALUYITUKA DIOKO AMBAYE ALIFUNGUA UKURASA KWA BAO SAFI DAKIKA YA DATO YA MCHEZO NA LA PILI ALILIFUNGA KWA KUMTUNGUA KIPA WA STARS JUMA DIHILE KWA KIKI KALI. NA MPIRA UMESHAMALIZIKA.

UMATI ULIOJITOKEZA KUANGALIA MCHEZO HUU UZALENDO ULIWASHINDA MARA BAADA YA STARS KUPIGA BAO LA PILI MAANA SIO TU WANAWASHANGILIA CHUI WA KABILA KWA NGUVU ZOTE BALI PIA WANAMZOMEA KOCHA WA STARS MARCIO MAXIMO.

LAKINI WANAMUONEA TU MAXIMO, JAMAA MPIRA WANAUJUA NA KOCHA WAO AMEKIRI KWAMBA HII INATOKANA NA MAADALIZI TOKA TIMU ZA VIJANA NA MASHULENI.

KOCHA MAXIMO AMESHUKURU MUNGU KWA KUZOMEWA NA AMESEMA WALIOMZOMEA LEO MWAKA UJAO WATAMPIGIA MAKOFI, NA KWAMBA KONGO SI TIMU NDOGO, NI BINGWA WA CHAN HIVYO9 MECHI ILIKUWA NGUMU SANA. AMEFURAHI KWAMBA WACHEZAJI WAKE WAMEPATA UZOEFU NA PAMOJA NA KUFUNGWA AMEWAPONGEZA WACHEZAJI WA STARS NA KUSEMA TIMU YAKE NI NZURI NA BAADA YA MUDA MATUNDA YATAONEKANA.
KOCHA WA KONGO SANTOS MUNTUBILE AMESWEMA WAO WANA UZOEFU WA WACHEZAJI KUWA PAMOJA KWA MUDA MREFU, NA AMESEME MECHI ILIKUWA NZURI KWA UPANDE WAO KWANI IMEDHIHILISHA WAO NI MABI NGWA WA CHAN. AMEWATAKA MASHABIKI WASIMKATISHE TAMAA MAXIMO ILA WAFANYE SUBIRA WAMUACHE AFANYE KAZI YAKE, KWANI MPIRA SI
 
Hana jipya huyo Maximo, ni mnafiki na kama mbongo tu, majungu kibao, tumuulize kwa nini Tinoco na Artamar waliondoka, kocha gania mbishi km P, Inabidi asepe na mwenzanke Wenger tumechoka watanzania na wapenzi wa arsenal kufungwa fungwa.
Jitu
 
Kwa Maximo kusema DRC wana uzoefu ni kujichanganya mwenyewe kwa sababu yeye hawataki wachezaji wenye uzoefu. Haitakuwa ajabu hata hawa anaowaremba sasa hivi akaja kuwatupia virago kama ilivyotokea kwa Chuji kipenzi chake miaka miwili iliyopita. Hatufai huyu kwani keshafikia ukomo wa ujuzi na maarifa yake katika soka. Lakini kwavile ni nyenzo mojawapo ya kampeni ya 2010 kwa Juma Kilaza hatuna jinsi ila kuula wa chuya hivyohivyo
 
Mbona Arsenal wanapigwa bao kila siku na Wenger anasema anajenga timu
 
Haya mjadala wa Maximo anafaa au hafai tunaomba ulejee upya.
Lakini bado anaimalisha kikosi kwa kuwafukuza walio pata mafunzo Brazili ufukweni kule na kuleta wadogo nao wakomaae.
 
Alafa huyo Kaliutuka Dioko na Mputu tunawaleta Jangwani pale Simba tumewaachia Ben Mwalala mtakiona cha moto.
 
Nadhani uwezo wa maskio (maximo) umefikia hapo. Sasa anaanza ku-rudisha nyuma c.v. ya taifa stars. Maximo ni mpuuzi anawasifia wachezaji kwa mpira gani? Mimi naamini bado anawahitaji Boban na Chuji na wenziwe. Timu hii ni changa na ukianza kuwalinganisha na Brazil anakosea. Utovu wao wa nidhamu hauingii kwa watanzania kwani wao ni wafanyakazi na wanarekebishika. Maximo ni yule mtu wazaramo wanasema "dihonyeka" (hasikii).
 
Back
Top Bottom