Taifa linahitaji damu changa - Sitta

Taifa linahitaji damu changa - Sitta

Filipo

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
9,347
Reaction score
5,553
Mh Samweli Sitta ameyasema hayo wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt. Teresia jimbo kuu katoliki Arusha. Amesema kuwa Mh Nyalandu na Mh Lema ni vijana ambao taifa linawahitaji na wao kama wazee wameshaanza kuwaridhisha uongozi wakiwa na matumaini makubwa kuwa watatufikisha kwenye nchi ambayo baba wa taifa alitamani tufike!

Nawasilisha
 
lema , anaingia sasa......, kadokezwa na sita "lema wewe si tajiri, ukianza tuuu ufisadi , kwishwaaaaaaaaaaaaaaaa", Lema anaingia sasaa
 
Ha ha ha ukweli umeanza kukubalika eeh
 
Mh Samweli Sitta ameyasema hayo wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt. Teresia jimbo kuu katoliki Arusha. Amesema kuwa Mh Nyalandu na Mh Lema ni vijana ambao taifa linawahitaji na wao kama wazee wameshaanza kuwaridhisha uongozi wakiwa na matumaini makubwa kuwa watatufikisha kwenye nchi ambayo baba wa taifa alitamani tufike!

Nawasilisha


Mbona siku hizi watu wanakimbialia makanisani kuchangisha michango? Mzee six na Lema? Naanza kuona kama maono nikiwa kwenye lindi la usingizi nahisi kitu au ni maluwe luwe ama ni upofu? Hakuna kitu hapa kweli?
 
Siku hizi harambee zimekuwa jukwaa la siasa.Kila mtu akialikwa atupa kijembe chake.
 
Tupo pamoja mr filipo wasi wasi wangu sasa madhabahu ya bwana yamegeuka majukwaa ya siasa kwa sababu mgeni rasmi anayoyaongea siyo yaliyompeleka hapo na viongozi wengine waalikwa wanasema siasa tu siyo mambo ya harambee tena
 
Mzee Sitta amesema ukweli. Vijana tunahitaji kumuunga mkono, kuna tatizo gani kufanya hivyo?
 
ukitaka kukubalika kisiasa kimbilia kuwazungumzia vijana. kete hii hata Lowassa anaitumia.
 
HATA VIJANA NAO WAKINAWA VEMA HURUSIWA KUSHIRIKI MLO MEZA KUU NA WAZEE: DR SLAA KAZI YAKO CHADEMA IMETAMBULIKA KWA VIJANA!!

"Hata kijana akinawa vizuri na vile vile kuonekana kusafisha mikono yake vema katika jamii yake inayomzunguka, kuna uwezekano mkubwa akakaribishwa meza kuu na kushiriki mlo kwa pamoja na Wazee," mwisho wa kunukuu toka kwa Profesa Chinua Achebe, (katibu chake cha 'Jamii Msambaratiko').

Vivyo hivyo, ni wazi kwamba malezi ya utaifa na ujasiri katika vijana hasa wa CHADEMA umemgusa Mhe Kasi na Viwango.

Kamanda Lema kama ulikua hujui, msimamo wako thabiti wa kutetea pasipo kurudi nyuma dhana ya heshima kwa '
UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA'ni dira hiyo nzito ambayo hadi sasa inawafanya MAFISADI viti kutokukalika na amani kwao kutoweka baada ya kuuona uungwaji mkono unavyopatikana toka kwa vijana wote nchini bila kujali itikadi.

Mhe Dr Slaa, hongera sana kwa uongozi thabiti na malezi bora kwa vijana wa CHADEMA wakiwa na dira ya kueleweka na mtazamo wa kitaifa zaidi.

Ni ukweli usiopingika kwamba hadi sasa umeweza kuwapa vijana kuanzi Mhe Mbowe, Zitto Kabwe, Regia, Halima Mdee, Kiwelu, Tundu Lissu, Ben, Heche, Wenje, Mushi, John Mnyika na wengine wengi ulwe mwelekeo hdimu ya
KUZUNGUMZA NA KUISHI SIASA ZA KITAIFA ZAIDI (Vijana CHADEMA kwao chauvinist politics hupewa kisogo) kuliko zile siasa za vitongojini na zile za 'Maslahi ya Chama Chetu'.

Hakika mtu akitazama saaaana atagundua kwamba mafunzo ya uongozi imara toka kwa Dr Slaa kwa Ma-Kada wa CHADEMA huenda ikawa kwao wao umewaambia kwamba siri ya mafanikio kisiasa kwa kipindi kirefu zaidi ni kuendeleza SIASA ZA KUTETEA TU MASLAHI YA UMMA.

Mh Samweli Sitta ameyasema hayo wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la Mt.

Teresia jimbo kuu katoliki Arusha. Amesema kuwa Mh Nyalandu na Mh Lema ni vijana ambao taifa linawahitaji na wao kama wazee wameshaanza kuwaridhisha uongozi wakiwa na matumaini makubwa kuwa watatufikisha kwenye nchi ambayo baba wa taifa alitamani tufike!

Nawasilisha
 
kete hii ilitumiwa pia na wanamtandao akiwemo Sitta na Lowassa katika uchaguzi mkuuwa mwaka 2005 kwa kuwa walifanikiwa kuiteka jamii na kaulimbiu hii naona wamerejea tena kwa mtindo uleule.
 
Lowasa anawakamata vijana wenye tamaa, kwa sababu vijana hawa kwa tamaa zao wapo tayari kutekeleza watakayotumwa ilimradi wamelipwa.
 
Lowassa anakimbilia makanisani na Sitta anakimbilia makanisani mengi tutayaona kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. inaonekana lile bifu la Sitta na Lowassa limetoka bungeni na kuingia makanisani kutafuta kuungwa mkono. Atakayekuja kuwa Rais kati ya hawa wawili mmoja atamtia ndani kwanza mwenzeke kwa majaribio ya kuonja mahabusu
 
Lowassa alikuja na somo la vijana ni bomu la kesho. Sitta amekuja na somo la tuwape uongozi vijana.
 
kama yanatoka moyoni ni heri kwa taifa letu lakini kama yanatoka ili kukidhi haja ya kufikia uongozi wa juu kuliko wote kitaifa haitawasaidia vijana wetu.
 
Naona leo anamkubali G. Lema kiaina lol.... Ila Lema akianza kuwarushia misumari ya ukweli pale Bungeni huwa wote wanasimama na kuomba miongozo! Sasa vijana tujipange....Big up Lema and 6
 
Back
Top Bottom