Taifa limekalia bomu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa limekalia bomu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 28, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Zima moto iko hoi
  [​IMG] Hakuna maandalizi  [​IMG]
  Zimamoto


  Mfululizo wa majanga yanatotokea nchini na kudhihirika udhaifu wa uwezo wa kuyakabili ni mambo yanayohatarisha usalama wa uhai na mali za raia, NIPASHE imethibitisha.

  Hali inaonyesha kuwa vyombo vya ulinzi na usalama havijaandaliwa kimfumo na kinyenzo katika kukabiliana na majanga kwa wakati.

  Mfano wa hilo ni jinsi ambavyo imekuwa ikishuhudiwa kwa askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wakifika na magari yao kwenye maeneo ya majanga kwa mbwembwe nyingi, lakini mara nyingi yanakuwa yana ama maji kidogo au hayana kabisa maji ya kuzimia moto.

  Pia gari la Zimamoto hutokea likawa halina nguvu ya kurusha maji au likawa na mipira ambayo haina uwezo wa kufika katika eneo la janga na kurusha maji.

  Kadhalika, katika maeneo mengi ya watu wengi, kama maofisini; misikitini; makanisani; hakuna vifaa vya kuzuia moto (fire extinguisher), hali inayoweza kusababisha moto kusambaa zaidi.


  KAULI YA KIKOSI CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

  Akizungumzia hali hiyo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha, alisema wamekuwa wakishindwa kumudu vyema kazi zao kutokana na kukabiliwa na tatizo la rasilimali, ikiwamo vitendea kazi na fedha.

  Alisema hadi sasa wana magari 95 ya kukabiliana na majanga nchini kote ambayo hayakidhi mahitaji.

  Nyambacha alisema gari moja la kawaida la zimamoto na uokoaji linauzwa Sh. milioni 700. Lililokamilika lenye ngazi ya kuwezesha kufikia kilele juu au chini kwenye hatari, linauzwa Sh. bilioni 2. wakati bei ya magari ikiwa hivyo, mavazi kamili ya askari wa zimamoto ya kazi yanauzwa Sh. milioni 2.

  “Uwezo wa nchi ni mdogo. Hivyo, kazi yetu siyo nzuri,” alisema Nyambacha.

  Hata hivyo, alisema serikali imeliona tatizo hilo na inalifanyia kazi na kwamba, hivi sasa wameanzisha utaratibu wa wananchi kuchangia huduma zinazotolewa na zimamoto.

  Alisema hivi sasa wanafanya ukaguzi kwenye majengo, maduka, magari na viwandani kubaini wasiokuwa na vifaa vya kudhibiti moto.

  Nyambacha alisema kila atakayebainika hana kifaa hicho, atafikishwa mahakamani kuomba aamriwe kulipa faini.

  JESHI LA POLISI

  Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Advera Senso, alisema pindi janga linapotokea, kazi kubwa ya jeshi hilo ni kuangalia aina ya janga, kujua kama wahusika wanazo taarifa ili kuhakikisha raia wote pamoja na mali zao wako salama.

  Alisema hatua ya pili ni kutahadharisha wananchi na kuimarisha ulinzi kwa raia na mali zao.

  Hata hivyo, Senso alisema jukumu la kukabiliana na majanga, si suala la taasisi moja pekee, bali linahusisha taasisi nyingi kutegemeana na janga.

  JUKUMU LA OFISI WAZIRI MKUU
  Kuhusu tatizo hilo, Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, David Kirway, anasema Ofisi ya Waziri Mkuu hupokea taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zinazohusu uwezekano wa kutokea janga.

  Alisema mara tu wanapopata taarifa kama hizo, huiarifu mikoa husika ili kamati za maafa zichukue hatua.

  Hatua hizo, ni pamoja na kutoa tahadhari, kujiandaa kukabili maafa (kama yatatokea), kuzuia au kupunguza makali ya maafa na kurudisha hali.

  Pia alisema zipo kamati za kushughulikia maafa yanapotokea. Kamati hizo huundwa kuanzia ngazi ya mkoa na wilaya.

  Alisema kamati hizo zina majukumu mbalimbali, ikiwamo kuratibu, kuelekeza, kuidhinisha na kudhibiti shughuli zote za menejimenti ya maafa katika maeneo yao.

  UJENZI HOLELA

  Tatizo lingine, ni kutokuwapo kwa viwango vya ujenzi, zikiwamo kuta mbalimbali na majengo marefu. Pia kutokuwapo udhibiti wa ujenzi holela mijini na kwenye majiji nchini.

  Hali hiyo imekuwa ikisababisha ugumu wa kazi ya uokoaji kufanyika kikamilifu au kutofanyika kabisa kutokana na maeneo yaliyokumbwa na majanga kushindikana kufikika.

  KAULI YA BODI YA MAKANDARASI (CRB)

  Msajili wa Bodi ya Makandarasi (CRB), Mhandisi Boniface Muhegi, alisema katika kipindi cha miaka miwili, wamefungua mahakamani kesi 42 dhidi ya makandarasi binafsi wanaotuhumiwa kukiuka sheria katika ujenzi.

  Alisema CRB imekuwa ikiwashauri watu, hususan wawekezaji wanaotaka kujenga majengo makubwa, kuhakikisha kabla ya kuanza ujenzi wanachagua makandarasi wenye uwezo.

  “Wasiokuwa na uwezo tunawapeleka mahakamani,” alisema Mhandisi Muhegi.

  Alisema katika sekta binafsi ndiko kulikokithiri matukio ya majengo kuanguka kutokana na kujengwa chini ya kiwango na hivyo kusababisha maafa.

  “Majengo mengi yanayoanguka ni ya watu binafsi,” alisema Mhandisi Muhegi.

  Alisema tatizo hilo linatokana na sheria ya manunuzi kutokuwapo katika sekta hiyo tofauti na serikalini na kwenye mashirika ya umma.

  Serikalini na kwenye mashirika ya umma kuna zabuni maalum za kununua vifaa (material) vya ujenzi vinavyokidhi viwango na ubora uliopendekezwa na wataalamu (wahandisi).

  Tofauti na kwenye sekta binafsi ambako ushirikishaji wa wataalamu ni mdogo au haupo kabisa kwa vile hawana uwezo wa kuwalipa.

  Alisema sababu nyingine ni makandarasi wengi kutotumia wataalamu waliosajiliwa na CRB kama sheria ya usajili ya makandarasi inavyotaka.

  Mwongozo wa Taifa wa Kudhibiti Maafa uliotayarishwa na Idara ya Kudhibiti Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Toleo la kwanza), umeweka bayana kuwa Tanzania inaathiriwa na maafa mengi kwa sababu mipango ya kushughulikia maafa hayo imekuwa haitoshelezi na hivyo, kusababisha athari kwa watu na uchumi kuongezeka siku hadi siku.

  Hilo linathibitishwa na kitendawili kuhusu hatma ya ripoti ya tume iliyowahi kuundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la ghorofa la Chang'ombe Village, eneo la Keko, Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, mwaka 2006.

  Ni zaidi ya miaka mitano sasa tangu jengo hilo la ghorofa hilo liporomoke na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia kutokana na kufunikwa na kifusi.

  Tume hiyo haijulikani ilipoishia. Ripoti yake ya uchunguzi haijawahi kusikika ikitolewa hadharani. Kana kwamba 'imeyeyuka'!

  TUME YA MAJENGO YA LOWASSA

  Wakati kizungumkuti hicho kikitafakariwa, Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kirway anasema aliye katika nafasi ya kutoa maelezo kuhusu hatima ya 'Tume hiyo ya Lowassa', ni Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, kwani suala hilo lilikabidhiwa kwa halmashauri hiyo.

  Ofisa Uhusiano wa Halmashauri hiyo, Joyce Msumba, alipoulizwa kuhusiana na tume hiyo, hana majibu. Badala yake, alisema mwenye mamlaka ya kuzungumiza suala hilo ni bosi wake ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri (DED), Margareth Nyalile, ambaye hata hivyo, anaeleza kuwa yuko safarini.

  “Samahani. Mkuu (Mkurugenzi) amesafiri, akirudi nitamwelezea,” anasema Msumba.

  DED ILALA

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime, anasema jukumu la kwanza la halmashauri katika kushughulikia majanga, ni kuwaarifu wananchi na kuona kama wana uelewa wowote juu ya janga lililotokea.

  Alisema jukumu la pili, ni kuangalia namna ya kupeleka misaada kwa waathirika wa maafa.

  “Kikubwa ni kuwa na timu ya uwajibikaji na kuituma haraka. Na ukiweza kupredict (kukisia) mapema unaweza kuokoa,” alisema Fuime.

  DED KINONDONI
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Fortunatus Fwema, alisema wanayo mikakati mingi ya kukabiliana na maafa yanayoweza kuwapata wananchi kutokana na majanga.

  Baadhi ya mikakati hiyo, anaitaja kuwa ni pamoja na kupima viwanja vya kutosha kwa ajili ya kuwasaidia wananchi walioathiriwa na majanga.

  Pia kutoa elimu kwa umma ili waepuke kujenga katika maeneo hatarishi.

  Hata hivyo, alisema yapo majanga, kama vile tsumani, ni tatizo la asili ambalo serikali haina uwezo wa kulizuia.

  “Inachoweza kufanya ni kutahadharisha watu dhidi ya namna gani wakabiliane na tatizo hilo,” anasema.
  Hakuna Mkurugenzi aliyeweza kusema kwa uhakika kamati ya ukaguzi wa majengo iliyoundwa na Lowassa iliishia wapi na ripoti yake iko wapi.

  CHANZO: NIPASHE

   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mabomu nchi hii ni mengi sana yakianza kulipuka moja baada ya jingine hapakaliki hapa.
   
 3. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 1,750
  Trophy Points: 280
  Ubabaishaji tu, hii nchi ujanja ujanja ndio mwingi! tumeingiza siasa kwenye utaalamu!
   
 4. kidadari

  kidadari JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2015
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 2,352
  Likes Received: 1,222
  Trophy Points: 280
  Siasa Tu
   
 5. Isanga family

  Isanga family JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2015
  Joined: Feb 25, 2015
  Messages: 4,786
  Likes Received: 3,763
  Trophy Points: 280
  Moto ni moja ya ajali ambazo zinaangamiza sana Watanzania lakini tunachukulia Mzaha..huyo kwenye picha izo nguo zenyewe ni moto akazime moto..
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2015
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Serikali ya CCM chini ya JK ilinunua magari kibao kabla ya uchaguzi kwa ajili ya kuwadhibiti wananchi wake mfano yale mawashawasha!! By the way hivi tangu yaje yamefanya kazi gani!!?

  I hope JPM yeye hatahangaika kupigana na wananchi wake bali kuwapa maendeleo na mahitaji muhimu!!
   
 7. M

  MjasiriaMali2030 Member

  #7
  Dec 8, 2015
  Joined: Oct 4, 2015
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kweli lakini jpm hakua chaguo la wananchi
   
 8. Benz Petrol

  Benz Petrol JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2015
  Joined: Nov 22, 2012
  Messages: 502
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 45
  CP Chagonja ndiyo kateuliwa kushika uongozi wa Zimamoto, tusitegemee maajabu yeyote...
   
Loading...