Taifa lenye NGUVU ni hili hapa.

Taifa lenye NGUVU ni hili hapa.

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
407
Reaction score
638
1. FAMILIA ZENYE NGUVU.

Kivipi?
Ili uwe na taifa lenye nguvu lazima lianzie kwenye familia ndogo hadi taifa lenyewe.
Hivyo ni lazima kuweka sheria kanuni taratibu na muongozo mzuri wa kulinda maadili ya watu na vizazi vyake na hatimae kuwepo na familia zenye maadili na taifa lenye nguvu kwa ujumla.

Leo hii vijana wengi wa kiume na wa kike ni wahuni kupitiliza na hawana muda na kujenga familia. Je, ni nini hatima ya taifa la kesho? Serikali imelikalia suala hili kimya bila kufanya chochote kila kusimamia maadili ya taifa letu la Tanzani.

Kuna haja ya kulitazama vyema suala la maadili maana bila kizazi chema basi hatutakuwa na taifa lenye nguvu bali wahuni tu wenye kuliangamiza taifa.
 
Back
Top Bottom