Taifa ambalo watu wake wanaandaliwa au wanajiandaa kuajiriwa tu ni Taifa litakalojiangamiza lenyewe

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,542
3,451
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana licha ya kuwa sehemu ya waajiriwa ambao tumekuzwa na mfumo wa hatari sana uliotuandaa kujenga imani ya kusoma kwa bidii ili kupata ajira nzuri badala ya kusoma kwa bidii ili kuzalisha ajira nzuri.

Nakiri kwa dhati kabisa kuwa mfumo huu umeua ubunifu kwa kiasi kikubwa na kukuza uvuvu, ulalamishi,upotezaji muda na uwajibikaji duni kwa wengi. Siyo jambo la ajabu mtu kuwa elimu ngazi ya digirii moja au mbili na bado akawa anasubiri ajira.

Mfumo wetu wa elimu umetujenga zaidi kuamini hata kama hatuwajibiki. Haishangazi kusikia mtu akisema soma kwa bidii ili uje uajiriwe sehemu nzuri na upate mshahara mzuri. Thamani ya mshahara leo imepewa ukubwa kuliko thamani ya elimu kwa sababu tunashindwa kutambua kusudi la elimu hasa ni lipi na je tunaandaliwa kuwa watu gani ukiachilia mbali kule kuamini tu kuwa ulisoma kwa bidii na kufauli vizuri utaajiriwa na upata mshahara mzuri.

Ni kawaida kabisa leo kusoma siyo kwa lengo la uelimika ila kwa lengo la kuajiriwa tu. Hali hii ni kiashiria cha hatari kubwa kwa Taifa lolote lile.
 
Ukiangalia comments na posts za wanaccm juu ya sera ya Lissu ya kuongeza ubora wa elimu yetu ili watoto wetu wapate ujuzi na maarifa badala ya vyeti tu wanavyopata kwa sasa ndo utaona na kujua hawa watu wana Nia gani na nchi hii.
 
Ukiangalia comments na post za wanaccm juu ya sera ya Lissu kuongeza ubora wa elimu yetu ili watu wetu wapate ujuzi na maarifa badala ya vyeti tu wanavyopata kwa sasa ndo utaona ndo utajua hawa watu wana Nia gani na nchi hii
Ccm walishachoka kuongoza hili taifa, na huyu mwenyekiti wao waliyempata kwa sasa basi anawaburuza kama gari bovu.

Kila anachowaambia wao kazi yao ni kukubali tu, watammisi sana Mzee Mkapa maana alikuwa na ujasiri wa kukosoa Profesa Magufuli
 
Wawekezaji wa ndani ni zao la mfumo bora wa elimu unaowaandaa watu siyo tu kuajiriwa au kujiajiri ila kuwaajiri wengine. Elimu yetu inapaswa ilitamke hili bayana na kwa dhati kabisa.
Tunaweza tukaanzisha viwanda, tukaanzisha na mitaji halafu tunaishia kuajiriwa.....ratrace tragedy".
Bado hatujachelewa tunachohitaji ni nia thabiti na utayari utakaoambatanana kulipa gharama.
 
Ni kweli mkuu. Mfumo wa elimu ndo chanzo kikuu cha umasikini wa watanzania na graduates wengi ajira hakuna.

Inashangaza mtu kutumia miaka17 ili uje kuajiriwa tu ulipwe milioni2.
Miaka yote hiyo hajui kwanini anasoma sababu elimu ni ya kukariri ili afaulu apate ajira, haina tofauti na elimu ya mkoloni.

Haukufanyi uwe na uwezo wa kutumia ubongo wako vizuri zaidi ya kukariri ili ufaulu upate kazi baada ya miaka kadhaa unastaafu unasubiri kifo.

Mfumo huu wa elimu hauzalishi wavumbuzi na watu wanaojitambua bali wavivu wa kufikiri wasioweza kuona fursa zilizojazana duniani zaidi ya kuajiriwa.

Unazalisha watu waliojaa Negative. Chochote yeye ni negative na kisichowezekana. Ajira tu ndo imetawala kichwani.

Nashauri huu mtumo waubadirishe ili kuendana na kasi ya tech na dunia kiujumla ili Tz na Africa inyanyuke.
 
Na hata ukitazama waajiriwa wengi ndani ya taifa hili, ni wale waliosoma kwa kukariri na kisha kupewa makaratasi ya ufaulu.. Wengi hawana ubunifu, wavivu, wapokea maelekezo, wasio na maono ya kuziendeleza taasisi na hivyo kama nchi inaishia kupiga makitaimu kimaendeleo. Ifanyike review kubwa ktk mfumo wa elimu.
 
Graduate akisubiri ajira inakuwa nongwa akijiajiri kuuza matunda, bodaboda au kuwa machinga anaonekana amekosa mwelekeo.​
Akionekana kufanya kitu nje ya taaluma yake wanajua alifeli shule.​
Wengine wanaambiwa wanakaa kijiweni kuota jua kama taa za solar za mchina.​
Vijana wanapitia mengi Sana awamu hii.​
 
Ukitaka kujua tunajiandaa kutawaliwa angalia elimu inavyotuandaa.. jiulize wangapi tunajiandaa au kuandaliwa kuja kuajiri wengine?

Kama watu wanaoandaliwa kuajiriwa ni wengi kuliko wanaoandaliwa kujiajiri,kuajiri na kubuni ajira basi tambua hiyo ni taa ya hatari kwa Taifa.

Kwa maana nyingine ni kwamba taifa linaandaliwa kuwa na watu wasioona mbali zaidi ya mshahara na kutawaliwa.

Natamani kizazi kijacho kisipite kabisa kuna ninayoipitia kwa maana imenifanya kuamini badala ya kutenda, kuogopa badala ya uthubutu. Mawazo yetu yanazunguka ndani ya uzio wa ajira iliyotafsiriwa tofauti na uhalisia.

Natamani Mwanangu nimfundishe ajiandae kuja uajiri wengine ili atoke nje ya uzio uliogharimu na unakigharimu kizazi chetu cha leo. Tutalalamika sana,tutailaumu serikali sana lakini tatizo ni mfumo wa elimu uliotuandaa umetuandaa kuwa watengenezaji wa matatizo na siyo watatuzi.
 
Pamoja na hayo yote itoshe kusema kuwa sio wote Lazima tujiajiri, wengine tubaki kuajiriwa... Wengine tujiajiri, wengine tuwaajiri watu wengine... Na pia tuajiriwe huku tukiwa tumejiajiri

Hizo kazi mnazosema tusiajiriwe nani atazifanya? Mashine/roboti ama?

Ni sawa na kusema kila mtu duniani awe na pesa, sasa nani atamsaidia mwenzake? Au mizania itatoka wapi? Na ndio maana kuna masikini na matajiri... Haiwezekani wote tukawa matajiri na pia masikini wote kwa wakati mmoja

Mfumo/sera za elimu ya Tanzania kuja kubadilika sio leo na hata ukibadilika lazima kuna watakaojiajiri na waajiriwa

Kwanza angalia mifumo ya shule za serikali na za binafsi/kimataifa utagundua "Gepu" kubwa sana
 
Back
Top Bottom