TAHLISO waionya Chadema

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) wamekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kutokana na tabia yake ya kupinga mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali hata kama yana manufaa kwa wananchi na Taifa kwa jumla.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, leo, Rais wa Jumuiya hiyo Frank Nkinda amesema kwa kipindi kirefu, chama hicho kimejijengea tabia mbaya ya kutafuta uungwaji mkono hata katika masuala yasiyo na maslahi kwa Taifa na kupinga mapendekezo yenye dhamira ya kuwaweka watanzania pamoja.

Akitolea mfano wa baadhi ya mambo hayo ikiwemo ripoti ya kikosi kazi iliyokabidhiwa juzi kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa imesheheni mapendekezo mbali mbali yenye tija kwa taifa letu. Nkinda alisema wao kama wasomi wa Elimu ya juu hawaoni sababu yeyote ya Chadema kuipinga ripoti hiyo

“Sote tulisikia muhtasari wa kile kilichowasilishwa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi, Prof. Rwekaza Mukandala kwa Mhe. Rais, kwakweli dhamira yake ni njema. Sasa tumeshangaa kakikundi kamoja kamekuja juu na kusema mapendekezo haya hayafai na kwamba ni matumizi mabaya ya fedha za umma, lakini ikumbukwe kwamba watu hawa waliitwa kutoa maoni yao wakakataa, sasa wanataka hata yale yaliyotolewa na watanzania wengine kwa uhuru na haki watu wayapinge ”alisema Nkinda

Aliongeza kuwa TAHLISO kama Taasisi inayolea nguvu kazi ya Taifa, kimsingi wana mamlaka ya Kuonya, kukemea na kushauri mambo mbalimbali katika Kuchochea maendeleo ya Taifa.

" Tumesikitishwa na kauli ya Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika ya kuita ripoti hiyo kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kuwa tu wao walikataa kuwasilisha maoni kwenye kikosi kazi cha Rais" alisema Nkinda

Alisema mtu au taasisi yoyote ya kiungwana ilipaswa kupongeza dhamira iliyoonyeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutafuta maridhiano ya kitaifa kwa kupata maoni ya wadau juu ya njia gani za kupita kabla ya kufikia hitimisho na siyo kulalamika mbele ya vyombo vya habari suala alilosema halina msingi wowote.

Aliongeza kuwa Watanzania wameipokea ripoti hiyo kwa mikono miwili na wanawapongeza wadau wote walioshiriki kutoa maoni kwenye kikos...
 
E99vW0kXoAIkPDR.jpg
 
Kilikuwa chama Cha siasa ila kwa sasa ni chama kupinga kilakitu aka Pinga Pinga
Unaweza hapa kunitaji maana ya chama cha upinzani/oposition party na chama tawala/rulling party?
je unaweza kuelezea na kutofautisha kimantiki kazi za kila kimoja kwenye siasa za nchi husika kwa wakati husika?
kwa akili zako za kawaida kupinga ni ninini na kukubali ni ninini?
asante
 
VIJANA WA TANZANIA KUANZISHA JUKWAA LAO HURU, NDIYO JIBU LA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKISHWA KTK NGAZI YA MAAMUZI KITAIFA

Duniani ni vijana wa vyuo vikuu ndiyo wanaoongoza kuchagiza mageuzi

Historia inaonesha mara baada ya uhuru wa kwanza kupatikana ktk mtaifa mbalimbalii iwe kwa mtutu wa bunduki au maandamano ya kuondoa wakoloni, baadaye kulifuatia msuguano wa wananchi wenyewe kwa wenyewe kwa kutoridhishwa na wale waliochukua utawala toka kwa wakoloni.

Sababu mbalimbali zilizua msuguano ktk nchi huru kama udiktekta, tawala kamdamizi ya chama kimoja, utawala mbovu, ubaguzi wa kielimu mfano mtoto aliyesoma shule za kata / st. Kayumba anadanganywa kuwa akihitimu chuo kikuu atakuwa na nafasi sawa na mwenzake aliyesoma St. Mary's akamaliza elimu ya chuo kikuu pia anayekimanya kiingereza / kispaniola vizuri zaidi na wajomba wake wapo ktk nafasi za kiutawala n.k

Vijana wengi pamoja na umasikini wa familia zao wanashawishiwa kwenda vyuo vikuu kwa kuchukua mikopo wakiwa na matumaini ambayo ni hadaa kuwa kwa kumaliza elimu ya juu watakuwa sawa na wale watoto wa tabaka la watawala anasema kiogozi wa vuguvugu la wanafunzi wa chuo kikuu wa Chile kamanda Gabriel Boric mwaka 2017.

Hapo ndipo Wanafunzi waliopo ktk nchi kama Sudan, Chile, Cuba, Afrika ya Kusini, Kenya walishiriki kudai mageuzi ili kuondokana na tawala zilizomgoa mkoloni.

Tanzania vijana hawajishughulishi kuhoji mambo yasiyowaridhishs wananchi kama matumizi mabaya ya kodi za wananchi, tozo ziluxokifu wananchi, demokrasia kubinywa, katiba kandamizi n.k

Chile nchi iliyo na kiongozi kijana Gabriel Boric ambaye ndiye rais kijana kabisa wa kuchaguliwa amezaliwa 11 February 1986 ambaye alichukua madaraka ya urais tarehe 11 March 2022 baada ya kushinda uchaguzi mkuu nchini Chile tarehe 19 December 2021 kwa kupata asilimia 60% ktk uchaguzi wa urais.

Gabriel Boric on the Chilean student movement 14 June 2017

Gabriel Boric on the Chilean Student Movement

Likes
59,554
Views
2017
14 Jun
In a presentation at the School of Public Policy on June 7, 2017; Gabriel Boric offers a historical perspective and reflects on lessons learned. He focuses especially on the role of social movements in a well-developed democracy and provides insights on how to sustain collective action over an extended period of time. He speaks also about his transition from being a member of a political movement to being a member of Parliament. Gabriel Boric is a Chilean parliamentarian, and a former leader of the national student movement. He was the president of the Student Federation of the Universidad de Chile, one of the most important student unions in the country. Boric currently represents the Magallanes and Antarctic Region in Chile’s Chamber of Deputies. He was elected as an independent candidate and is not associated with either one of the two political coalitions that have traditionally dominated politics in Chile. Source:

Department of Public Policy at CEU​

Mwanafunzi wa chuo kikuu toka familia masikini anazama ktk mkondo wa madeni ya fedha za mkopo wa elimu ya juu huku akiwa na matumaini potofu ya kupata ajira au kuwepo mazingira hewa ya kujiajiri.


Vijana vyuo vikuu na mijini pia vijijini badala ya kumezwa na ukiritimba wa UVCCM na ahadi kuwa ni viongozi wa kesho huku watoto wa vigogo wa CCM wanapewa nafasi sasa na siyo kesho wanatakiwa kuunda chombo chao kipya cha kutambulika kama mdau muhimu anayehitaji kuonekana katika majukwaa ya siasa pia ktk vituo vya redio, televisheni na mitandao ya kijamii kuchagiza mabadiliko na mageuzi ikiwemo pia kupewa nafasi nje ya mfumo wa vyama ili wagombee nafasi za kuchaguliwa na wananchi.


Gabriel Boric - The 100 Most Influential People of 2022 - TIME

time.com › collection › gabriel-boric

gabriel boric presidente from time.com
23 May 2022 · He is making Chile the social, economic, and political laboratory of the world once again. Stiglitz is a Nobel Prize–winning economist
 
Kilikuwa chama Cha siasa ila kwa sasa ni chama kupinga kilakitu aka Pinga Pinga

Sipati picha siasa za majukwaani zikianza tena, matamko yatarudi tena. Na ninahisi Katazo la mikutano latarudi tena, maana hili Katazo haramu la mikutano, mlengwa alikuwa CDM. Hakuna namna CCM watakubali CDM wafanye siasa kwakuwa wao ndio wanaokubalika zaidi na wananchi, hasa vijana.
 
hahahaha
wasomi wetu hao.... enhe CHADEMA Ni CHAMA CHA SIASA WAO WANAWAONYA KAMA NANI VILE?
Kosa kubwaa la chadema ni hii yakujiona watakatifu mda wote, na ndio hawahawa chadema kuchakutwa nikutaka eti kuwepo na uhuru wa mawazo. Wao wanataka uhuru wa mawazo iwe kukosoa chama kinginee ila Kwa wao chadema iwenikusifiwa tuuu. Chadema kubalini kukosolewa ndio demokrasia inataka hivyoo. Pokeeni na mawazo kinzani kwenu, kwani yapo yanayowajenga na nyiee pia.
 
Sipati picha siasa za majukwaani zikianza tena, matamko yatarudi tena. Na ninahisi Katazo la mikutano latarudi tena, maana hili Katazo haramu la mikutano, mlengwa alikuwa CDM. Hakuna namna CCM watakubali CDM wafanye siasa kwakuwa wao ndio wanaokubalika zaidi na wananchi, hasa vijana.
Chadema kubalini kusikia na mawazo kinzani kwenu pia, hiii ndio demokrasia sahihi. Nyinyi ndio vinala wa kutaja uhuru wa mawazo na kukosoa, Kwa Nini nyinyi hampendi kukosolewa??. Au nyinyi furaha yenu kikosolewe chama kinginee tuuu Kwa kuwa nyinyi ni malaika? La hasha, pokeeni kukosolewa ndio itakuwa sababuu ya kukua kwenu chadema
 
Chadema kubalini kusikia na mawazo kinzani kwenu pia, hiii ndio demokrasia sahihi. Nyinyi ndio vinala wa kutaja uhuru wa mawazo na kukosoa, Kwa Nini nyinyi hampendi kukosolewa??. Au nyinyi furaha yenu kikosolewe chama kinginee tuuu Kwa kuwa nyinyi ni malaika? La hasha, pokeeni kukosolewa ndio itakuwa sababuu ya kukua kwenu chadema

..CCM ingekuwa inapenda uhuru wa mawazo na kukosolewa isingezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
 
Hii TAHLISO nayo ni jumuiya ya ccm kumbe?
Mamlaka ya kuonya wameitoa wapi?
Wasomi gani wasioheshimu uhuru wa maoni?
Sensa ya watanzania walioipokea ripoti kwa mikono miwili waliifanyia wapi?
Ile ripoti ni hadaa kama hadaa nyingine za ccm. Ni delaying tactics za ccm kutucheleweshea katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
Hii TAHLISO nayo ni jumuiya ya ccm kumbe?
Mamlaka ya kuonya wameitoa wapi?
Wasomi gani wasioheshimu uhuru wa maoni?
Sensa ya watanzania walioipokea ripoti kwa mikono miwili waliifanyia wapi?
Ile ripoti ni hadaa kama hadaa nyingine za ccm. Ni delaying tactics za ccm kutucheleweshea katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

..TAHLISO kama wasomi walipaswa kupangua hoja za Chadema kwa kutumia vielelezo mbalimbali na sio kuwatishia na kuwaonya wasitoe maoni yao.

..Wakati Mnyika akitoa maelezo kukosoa ripoti ya kikosi kazi alikuwa akifanya rejea ktk kazi na utafiti uliofanywa na Tume ya Warioba.
 
Back
Top Bottom