Wasomi mbalimbali katika vyuo vikuu vya mkoa wa Morogoro wamelaani vikali tamko lililotolewa na Mkiti wa Jumuiya ya vyuo vikuu vya elimu ya juu nchini Amon Chakushemeire kwamba CHADEMA kinachochea migogoro kwenye vyuo vikuu nchini.
Wakizungumza kwa hasira wanafunzi kadhaa na viongozi wa wanafunzi walisema hawakuwahi kushirikishwa katika tamko hilo walilodai ni la kipuuzi kuwahi kutolewa na kiongozi wa TAHLISO.
Tayari tamko hilo la Mkiti wa TAHLISO limewagawa wanafunzi kote chini katika makundi mawili.Lile kundi kubwa la wafuasi wa Chadema na lile dogo la wafuasi wa CCM.Tamko hilo lililotolewa dhahiri lilikuwa likikishambulia Chadema bila kueleza uhalisia wa vurugu katika vyuo vikuu.
Wanafunzi hao wamemtaka Mkiti huyo wa TAHLISO kufuta mara moja tamko lake na kuliomba radhi Taifa kwa kusema uwongo.
Source:Tanzania Daima Jumapili.