Taharuki ya fidia bagamoyo-serikali yawageuka wananchi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Ama kweli ngo'mbe wa maskini hazai wahenga walinena.
Baada ya maneno matamu matamu kutoka kwa mbunge wa bagamoyo bwana Kawambwa yaliolenga kuwashawishi wakazi wa bagamoyo kukubali kupisha utanuzi wa bandari na kuahidiwa kulipwa fidia nono hatimaye Serikali kupita waziri wa viwanda na biashara ametanabaisha kuwa wakazi wa bagamoyo wamepigwa changa la macho kama sio kuingizwa choo cha jinsia tofauti.

Kigoda amesema fidia itakayotolewa italingana na jengo lililopo kwenye kiwanja na si vinginevyo.Tukumbuke 'mijengo mingi ya bagamoyo ni mbavu za mbwa!
Kigoda hajaweka wazi ni ipi fidia ya mashamba walimozikwa wazee wa bagamoyo .....ama kweli ccm walaghai!

Kawambwa aliwahi kuwatia moyo watu wa bagamoyo kuwa fidia itakuwa zaidi ya mara mbili ya kile kilichopo kiasi cha kumuwezesha mwananchi kununua kiwanja na kujenga sehemu nyingine.

Leo hii Kigoda kakata maini ya wakwama,wakwere na wazaramo.

Inatarajiwa wiki hii mwishoni kutaanza kufanyika kwa tathmini ya awali ya viwanja na mali zilizoorodheshwa na wakazi kwa ajili ya fidia.

Oooh!poleni wakazi wa bagamoyo...Tukumbuke wakazi wa kusini walivyowamwagia mitusi watu wa bagamoyo kuwa wanapendelewa kumbe waapi bwana maumivu ya uwekezaji hayachagui kabila au kanda...mkoloni mweusi ni yule yule ccm.


KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Back
Top Bottom