Taharuki: Wananchi waua simba tisa Serengeti

Taharuki: Wananchi waua simba tisa Serengeti

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,321
SIMBA WAULIWA.jpg

Simba hao waliuawa kwa sumu baada ya kuvamia katika makazi ya wananchi na kuua ng’ombe ndipo ikatokea hatua ya kulipiza kisasi kwa kutia sumu hivyo kusababisha vifo vya simba.

Mbali na kulishwa sumu, mmoja alikatwa miguu, mkia, ngozi ya juu ya mgongo na kuchukuliwa baadhi ya viungo vyake.

Kutokana na vifo hivyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ameagiza Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Serengeti kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Kigwangalla alisema mauaji hayo hayavumiliki kwa kuwa yana athari kubwa kiikolojia, kiutalii na uchumi wa taifa kwa ujumla.

"Bahati mbaya sana ni kuwa anapouawa simba kwa sumu hafi peke yake, inakufa familia nzima ya simba na mara nyingi wanakufa pia wanyamapori wengine wanaodowea nyama na wanaokula mizoga. Walipouawa simba wa Ruaha hivi karibuni walikufa zaidi ya fisi 70 na zaidi ya ndege mbeshi 100, achilia mbali wadudu," alisema.

Alisema pamoja na faida kubwa za simba kwa taifa kiuchumi, Kijiji cha Nyichoka pekee walikouawa simba hao ni sehemu iliyofaidika na miradi ya ujirani mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

"Wanyama hawa jamii ya paka wakubwa ni muhimu sana kwa kuweka mizani ya ikolojia sawa maana wanadhibiti idadi ya wanyama wala nyasi kwa kuwala, bila hivyo hifadhi zote zinaweza kugeuka kuwa jangwa.

"Hakuna mtalii atakayekuja hifadhini asitamani kumwangalia simba, mfalme wa pori. Wanapouawa maana yake tunashusha hadhi ya hifadhi zetu kiutalii, hivyo kutishia kupoteza mapato yanayotokana na utalii," alisisitiza.

Alisema tukio hilo la kuuawa kwa simba wa ikolojia ya Serengeti si la kwanza kutokea nchini kwa kuwa mwishoni mwa mwaka jana, simba wengine watano waliuawa pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

IPP
 
Vipi hao Simba wangewala watu? Walikua wapi hao askari wa wanyapori wakati Simba wanaua mifugo ya watu? Nani kaingia anga za mwenzake, Simba au binaadam?
Huyo waziri hana busara hata chembe, anaongelea ekolojia inayodhibiti, wanyama walao nyasi vipi kuhusu ekolojia inayotishia uhai wa mwanadamu.
Stupid
 
Waafrika sijui tuna matatizo gani..unamwekea sumu SIMBA MMOJA unategemea atakufa unaemtaka!! Si utakuwa umesababisha mauwaji ya wanyama wengi wakiwemo lion's family, akina fisi, mbwa mwiru n.k.... Kuna mijitu mingine haiogopi dhambi kwa Mungu au pengine ni mipagani tu.
 
Kutokana na vifo hivyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, ameagiza Kikosi Kazi Dhidi ya Ujangili cha Taifa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Serengeti kuwasaka watu waliohusika na mauaji hayo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Na kama watu hao wangeuawa, je simba wangekamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria?
 
Kwahiyo hicho kikosi kazi kinahusika na usalama wa wanyama tu sio? ng'ombe sio mnyama?
Binadamu sio mnyama. Tunatumia rasilimali kulinda wanyama wanao haribu mali za watu, kisa wanaingia fedha za kigeni kupitia utalii?

Mawaziri wa aina hii, watakuja kulipa haya. Wana uhakika gani kuhusu usalama wa watu wao, kama ng'ombe wanaoishi nao wanavamiwa na simba, na bado waziri anaona simba kafanya poa, ila binadamu kwa kujilinda kutokana na baada ya ng'ombe ni wao, wanapelekwa mahakamani simba je?

Sifa na njaa hizi, mnsuweka utu mfukoni, eti ndo viongozi wakubwa kabisa watarajiwa, lo! kwa roho hizi?!
 
Hivi lile tamko la waziri Kigwangwala la wahamiaji wa kinyarwanda kuondolewa huko mto kagera limeshafanyiwa kazi kweli?

Hata ningekuwa mimi hao simba wangekula mikuki ya sumu tena fasta tu, hivi inakuja akilini wananchi wamevamiwa na simba halafu wawachekee tu wakati uhai wao uko hatarini na ng'ombe wao wanaliwa na hao simba.

Kesi ya ujangili haina mashiko dhidi ya hao wananchi tena wakipata lawyer mzuri atawatoa lupango fasta tu.

Tena Hifadhi ya serengeti itatakiwa kulipa fidia ya ng'ombe waliouawa.

Hongereni sana warrior men kutoka warrior tribe kwa kuwawahi hao simba.
 
Waafrika sijui tuna matatizo gani..unamwekea sumu SIMBA MMOJA unategemea atakufa unaemtaka!! Si utakuwa umesababisha mauwaji ya wanyama wengi wakiwemo lion's family, akina fisi, mbwa mwiru n.k.... Kuna mijitu mingine haiogopi dhambi kwa Mungu au pengine ni mipagani tu.

Kwahiyo unataka Simba waachwe waendelee kutafuna mifugo ya watu na mwisho wa siku wawatafune watu kabisa.
 
Vipi hao Simba wangewala watu? Walikua wapi hao askari wa wanyapori wakati Simba wanaua mifugo ya watu? Nani kaingia anga za mwenzake, Simba au binaadam?
Huyo waziri hana busara hata chembe, anaongelea ekolojia inayodhibiti, wanyama walao nyasi vipi kuhusu ekolojia inayotishia uhai wa mwanadamu.
Stupid
Juzi kati tembo aliuwa mtu huko ruvuma serikali ikatum jAmaa flani msibani akawachana ukweli wananchi kuwa wanajitakia wenyewe vifo kwa kusogerea hifadhi
Yule jamaa anajiamini mno waombolezaji walibAki kimyaaa
 
Kwahiyo unataka Simba waachwe waendelee kutafuna mifugo ya watu na mwisho wa siku wawatafune watu kabisa.
We jamaa embu acha upoyoyo, umemuelewa lakini ...tatizo sio kuua simba ..tatizo njia waliyotumia kuulia hao simba ni hatarishi ....sumu aliyokula simba ,itakua wanyama wanaokula hiyo simba kama mzoga ,na ndege pia ..pia kumbuka kuna wanadamu pia huwa wanalimda so anaweza kuta ndege huyo aliyekula mzoga wa simba ...akamtega na akategeka so akaenda..kumtumia kama chakula sumu ikamdhuru...
 
Upoyoyo ndio nini, unashindwa kuchangia bila kutoa maneno ya kejeli?
 
Back
Top Bottom